SAHABA KWA SUNNI
1. Katika uk. 30 wa kitabu chake, Sheikh M. al-Khatib amesema hivi kuhusu sahaba: Ahlil sunnah wanaafikiana juu ya kuwahishimu na kuwaombea radhi za Mungu...
Majibu: Hata Shia ni vivyo hivyo; na ushahidi wa hilo ni ile dua waliyonayo wao ya kuwaombea Mwenyezi Mungu sahaba wa Mitume wote kwa jumla, na wale wa Mtume Muhammad s.a.w.w. hasa, ambayo tafsiri yake ya Kiswahili ni kamaifuatavyo:
"Ewe Mola! Wabariki wafuasi wa Mitume yote na wale wenye kuwasadikisha katika mambo ya ghaibu —miongoni mwa wakaazi wa dunia hii —wakati wapinzani wao wanapowapinga kwa kuwakadhibisha hali wao wana hamu ya (kuwaona) Mitume kwa imani ya kweli, katika kila wakati na zama ambapo ulituma Mtume na ukawasimamishia watu wake dalili —kuanzia kwa Adam mpaka kwa Muhammad s.a.w.w. —ya maimamu wa uongofu na viongozi wa wacha-Mungu, amani iwe juu yao wote. Tafadhali wakumbuke (wote) hao kwa maghfira na radhi zitokazo Kwako.
Ewe Mola! Wabariki na sahaba wa Muhammad hasa, ambao waliandamana naye kwa wema, na ambao walipigana kishujaa katika kumnusuru, wakamsaidia na kufanya haraka katika kuunga mkono ujumbe wake na kuuitikia mwito wake, waliomwitikia mara tu alipowasikilizisha hoja za ujumbe wake, wakajitenga na wake (zao) na watoto (wao) katika kulidhihirisha neno lake, wakapigana na baba (zao) na watoto (wao) katika kuthibitisha utume wake, na wakanusurika kwaye.
Wabariki na wale waliozama katika kumpenda yeye, waliokitarajia biashara isiyoweza kuharibika ya mapenzi (yao) kwake.
Wabariki na wale ambao jamaa zao waliwahama pale waliposhikamana na makubadhi yake, na (wale ambao) akraba (zao) waliwakimbia pale walipokaa chini ya kivuli cha akraba zake.
Basi usisahau, ewe Mola, yale waliyoyaacha kwa ajili Yako katika Njia Yako. Wape radhi Zako kwa kuwakusanya viumbe Vyako katika (dini) Yako, na kwa kuwa walinganaji Wako pamoja na Mtume Wako, (waliolingania watu) Kwako. Uwalipe kwa kuyahama majumba ya watu wao kwa ajili Yako, na kwa kutoka kwenye maisha
12
ya ufanisi na kuingia katika yale ya dhiki, na kwa mateso mengi yaliyowapata katika kuitukuza dini Yako.
Ewe Mola! Uwafikishie bora ya malipo Yako wale waliowaandama wao kwa wema, ambao walikisema: Mola wetu, tusamehe sisi na ndugu zetu waliotutangulia katika imani —walioamua kufuata njia yao iliyo wazi na kuelekea mwelekeo wao, wakafuata nyayo zao; ambao shaka haikuwatoa katika dini yao wala haikuwababaisha katika kuzifuata njia zao na kuongoka kwa uongozi wao. huku wakiwasaidia na kuwatia nguvu; waliofuata dini yao na kuongoka kwa kiongozi wao, wakawafikiana nao bila ya kuwatuhumu katika yale waliyowafikishia.
Ewe Mola! Warehemu na waandamizi wa masahaba, kutoka siku yetu hii mpaka Siku ya Malipo. (Uwarehemu) na wake zao, vizazi vyao, na wale waliokutii Wewe miongoni mwao, kwa rehema ambazo kwazo utawakinga na kukuasi Wewe, utawakunjulia bustani za Pepo Yako, utawakinga Kwazo na vitimbi vya Shetani na kuwasaidia katika mema waliyokuombea msaada, utawakinga na vituko vya usiku na mchana isipokuwa kituko kiletacho kheri, uwapelekee kwazo kuwa na imani ya kutarajia mema Kwako, kuwa na tamaa ya yaliyoko Kwako, na kuacha kutuhumu yaie yaliyomo mikononi mwa waja Wako ili uwarejeze katika kujipendekeza Kwakc na kukuogopa, (na ili) uwafanye waupe mgongo ufanisi wa dunia hii na kuwapendekezea kuiendea mbio Akhera na kujitayarisha kwa yaliyoko baada ya mauti, (ili) uwafanyie jepesi kila zito litakalowazunguka siku ya roho kutoka miilini mwao, uwaafu na makatazo yote yale ambayo huletwa na mitihani, (uwaafu) na mateso ya Moto na kubaki humo milele, na (ili) uwapeleke kwenye amani ya makaazi ya wacha-Mungu."
Jee, Sunni wanayo dua kama hiyo? Kama wanayo, tutafurahi kuijua. Kama hawana, basi vipi Sheikh M. al-Khatib ataweza kujigamba kuwa wao peke yao ndio wanaowaheshimu sahaba na kuwaombea radhi za Mwenyezi Mungu? Jee, baada ya kuisoma dua hiyo na kuielewa, bado unaweza kufikiri kwamba Sunni peke yao ndio wanaowaheshimu sahaba na kuwaombea radhi za Mwenyezi Mungu?
Kama wataka kukiona Kiarabu cha dua hiyo, tafadhali tazama uk. 52-50 humu; na kama wataka kuzijua dua nyingine ambazo Shia huziomba, pata kitabu kiitwacho Sahifa Sajjadiyya.
Sahaba wote ni waadilifu?
2. Akaendelea kusema (katika huo huo uk. 30) kwamba ni imani ya Sunni kuwa:
...wao (yaani sahaba) ni waadilifu wote...
Majibu: Hapo ndipo penye hitilafu baina ya Sunni na Shia; maana Shia hawaamini hivyo.Waaminivyo wao ni kwamba baadhi tu ya sahaba ndio waadilifu, na baadhi nyingine si waadilifu; na kwa hilo wana ushahidi wa mambo yaliyofanywa na sahaba hao ambayo kwayo,kwa mtu yeyote
13
atumiaye akili yake, hawawezi kubaki kuwa waadilifu. Na hapa chini tunataja mifano michachetu kuthibitisha hilo:
(i) Qudama b. Madh'un: Huyu ni miongoni mwa Waislamu wa mwanzo mwanzo. Alihama hijra mbili, akawahi hata kupigana katika Vita vya Badr. Lakini pamoja na yote hayo aliwahi kushikwa amelewa, zama za Ukhalifa wa Umar b. al-Khattab, akapigwa haddi! Jee, sahaba huyu bado ni mwadilifu? (Taz. al-lsaba, Juzuu ya Tatu, uk. 219-221; na al-lsti'ab, iliyo chini ya al-lsaba, Juzuu ya Tatu, uk. 247-251)
(ii) Abdulrahman (al-Awswat) b. Umar b. al-Khattab: Huyu, kama jina lake lionyeshavyo, alikuwa ni mtoto wa Khalifa wa Pili, na alikuwa ni sahaba vile vile. Yeye naye alikamatwa amelewa, na babake akampiga haddi! Hata inasemekana kwamba alikufa kwa kipigo hicho. (Taz. uk. 405-406 wa Juzuu ya Pili ya al-lsaba; na uk. 395-396 wa Juzuu ya Pili ya al-lsti'ab, iliyo chini ya al-Isaba) Jee, na huyo naye atakuwa ni mwadilifu? Kwa kipimo gani?
(iii) Abu Mihjan: Huyu ni sahaba mwingine aliyekuwa akinywa pombe sana na kuzini; hata imeeelezwa kwamba Khalifa Umar b, al-Khattab aliwahi kumpiga viboko mara saba au nane kwa hilo! Akawahi hata kumfunga! (Taz. al-lsaba, Juzuu ya Nne, uk. 173-175; na uk. 181-187 wa Juzuu ya Nne ya al-lsti'ab iliyo chini ya hiyo al-lsaba.) Jee, sahaba kama huyo vipi huendelea kuwa mwadilifu?
(iv) Nu'aiman b. Amr. Huyu ni sahaba ambaye amepigana jihadi vita vyote. Lakini pamoja na hivyo, alikuwa mlevi! Mara nne Mtume Muhammad' s.a.w.w. alimkamata sahaba huyo amelewa! Kati ya hizo, mara tatu alimpiga haddi! Mara ya nne, ndipo Umar b. al-Khattab alipotaka akatwe kichwa chake, lakini Bwana Mtume s.a.w.w. hakumkubalia. (Taz. chini ya jina la Marwan b. Oais al-Aslami katika uk. 384 wa Juzuu ya Tatu ya al-lsaba; na pia juzuu hiyo hiyo, uk. 540-541, chini ya jina la huyo Nu'aiman. Vile vile taz. Usudul Ghaba, Juzuu ya Nne, uk. 199 - 200, na Juzuu ya Tano, uk. 36 - 37.) Haya! Jee?
(v) Samura b. Jundub: Huyu ni mmoja ya wale watu watatu walioambiwa na Bwana Mtume s.a.w.w. kwamba, wa mwisho wao kufa, ataingia Motoni. Yeye alikiuza pombel(Taz. chini ya Hadith Na. 61 katika uk. 82-84 wa Mujallada wa Kwanza wa Silsilatul Ahadithidh Dhaifa Wa/ Mawdhu'a ya Muhammad Nasiruddin ai-Albani.) Bado huyo ni mwadilifu?
(vi) al-Walid b.Uqba: HuyundiyeyuleambayeMwenyeziMungu
14
amemwita fasiq katika Sura 32:18 na Sura 49:6. Isitoshe; na ndiye yeye, pale alipokuwa Gavana wa Kofa zama za Ukhalifa wa Uthman b. Affan, aliyeswalisha watu swala ya asubudhi rakaanne, na huku amelewa! Kisha akatapika kibulani, akatoa salamu na kuwauliza walioswali naye: Jee, niwaongezee? Kwa hivyo akapigwa haddi na kuondolewa kwenye Ugavana!
Kuhusu Sura 49:6, amesema Ibn Abdilbar kwamba hakuna hitilafu baina ya wanazuoni kuwa aya hiyo iliteremshwa kwa ajili yake (ai-Walid b. Uqba). Hayo utayapata katika uk. 601 wa Juzuu ya Tatu ya al-lsaba. Na katika ukurasa huo huo, wa kitabu hicho hicho, amesema Ibn Hajar al-Asqalani: 'Kisa cha yeye kuswalisha watu asubuhi rakaa nne, ni mashuhuri; na kisa cha kuuzuliwa kwake baada ya kuthubutu kwamba amekunywa pombe, ni mashuhuri vile vile, na kimetolewa katika Sahih Mbili (yaani Bukhari na Musliml. Na Uthman alimwuzulu Kofa baada ya kumpiga viboko, akamtawalisha Said b. al-As (mahali pakeh' Jee? Huyo naye pia ni mwadilifu?
Hiyo basi ni mifano michache tu ya baadhi ya masahaba wa Mtume Muhammad s.a.w.w. na maasia yao! Na vyote visa vyao hivyo tumevitoa katika vitabu vya Kisunni; hapana kitabu hata kimoja cha Kishia hapo! Sahaba kama hao ndio ambao Shia hukataa kuwa ni waadilifu; na ni sahaba kama hao ndio ambao Sunni hushikilia kuwa ni waadilifu kwa sababu kwao, kama alivyosema Sheikh M. al-Khatib, sahaba wote ni waadilifu! Sasa mambo yakiwa ni hivyo, upi kati ya misimamo miwili hiyo ndio wa sawa? Wa kuwa sahaba wote ni waadilifu; au wa kuwa sio wote ni waadilifu? Jiamulie mwenyewe, ewe ndugu yangu.
Hapa napenda ijulikane kwamba kuna visa vingine k.w.k., vinavyowahusu masahaba wakubwa wakubwa, ambavyo nimeviacha kwa makusudi. Na sababu ya kutovitaja ni kwamba ninaamini kuwa wengi sana wa wasomaji wa maandishi haya hawajawa tay&ri kupokea visa hivyo! Hata hivyo, kama nitala-zimishwa, sitakuwa na budi isipokuwa kuvieleza: japokuwa shingo upande.
Utabiri wa Mtume s.a.w.w. kuhusu sahaba
Na sio kwamba sahaba walifanya maasia tu, kama tulivyokwisha kuona hapo juu, bali Bwana Mtume mwenyewe (s.a.w.w.) alikwisha kutabiri, kabla ya kutawafu kwake, kwamba baadhi ya sahaba zake watazua mambo katika dini hii na kuibadilisha. Na yote hayo yamo katika vitabu vinavyotegemewa sana na Sunni! Hapa chini tunakutajia machache tu (sio yote) yaliyomo katika Sahih Bukhari na Sahih Muslim:
15
(i) Imepokewa kwa Anas kwamba Mtume s.a.w.w. amesema: Watu miongoni mwa sahaba zangu watanijia kwenye Hodhi1. Nitakapowaona, na watakapokuwa waletwa kwangu, watazuiwa ili wasinifikie. Hapo nitasema: Sahaba zangu, sahaba zangu! Nami nitaambiwa: Wewe hujui walizua nini baada yako.
Hadith hiyo utaiona katika Sahih Muslim, 'Kitabul Fadhail', Mlango wa 'Hawdhu Nabiyyina s.a.w.w. Waswifatuhu.' Kwa Kiingereza ni Hadith Na. 5706 kwenye uk. 1239 wa Juzuu ya Nne.
Hali kadhalika, Hadith yenye maneno karibu kama hayo yaweza kuonekana katika Sahih Bukhari, 'Kitabur Riqaq', Mlango wa 'al-Hawdh'. Na kwa Kiingereza, ni Na. 584 kwenye uk. 381 wa Juzuu ya Nane.
(ii) Imepokewa kwa Abu Hazim kwamba amemsikia Sahl (b. Sa'd) akisema kwamba amemsikia Mtume s.a.w.w. akisema: Mimi nitawatangulia nyinyi kwenye Hodhi. Atakayekuja, atakunywa. Na atakayekunywa, hatasikia kiu abadan. Na watanijia watu ninaowajua, na wao wananijua. Kisha pata-ingiwa kati baina yangu na wao.
Abu Hazim asema: Nu'man b. Abi Ayyash akanisikia nikiitoa Hadith hii. Akasema: Hivyo ndivyo ulivyomsikia Sahl akisema? Nikasema: Ndio. Naye akasema: Na mimi nashuhudia kwamba nimemsikia Abu Said al-Khudri akisema vivyo hivyo, lakini yeye alizidisha kwamba (Mtume s.a.w.w.) atasema: Hao ni (watu) wangu. Naye ataambiwa: Wewe hujui walifanya nini baada yako. Hapo nitasema: Ole wake! Ole wake, mwenye kuibadilisha (dini yake) baada yangu.
Hadith hiyo imo katika Sahih Bukhari, 'Kitabul Fitan', Mlango wa Kwanza. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 174 iliyoko uk. 144 wa Juzuu ya Tisa. Na katika Sahih Muslim utaipata katika 'Kitabul Fadhail', Mlango wa 'Hawdhu Nabiyyina s.a.w.w. Waswifatuhu.' Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 5682 iliyoko uk. 1236 wa Juzuu ya Nne.
(iii) Imepokewa kwa Abdullah kwamba Mtume s.a.w.w. amesema: Nitawatangulia kwenye Hodhi; na watu miongoni mwenu watainuliwa (niwaone). Kisha watazuiwa (kunifikia). Hapo nitasema: Ewe Mola wangu! Ni sahaba zangu (hao). Nitaambiwa: Wewe hujui walizua nini baada yako.
Hadith hiyo imo katika Sahih Bukhari, 'Kitabur Riqaq', Mlango wa 'al-Hawdh'. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 578 iliyoko uk. 378 - 379 wa Juzuu ya Nane.
1. Makusudio yaHodhihapaniuleMtoKawthar uliotajwa katika Sura108:1
18
(iv) Amesema Abduliah kwamba Mtume s.a.w.w. amesema:Mimi nitawa-
tanguliakwenyeHodhi(ambapo)watumiongonimwenuwatainuliwa
(niwaone).Nitakapotakakuwafikia,wataondelewa(nisiwafikie)!Hapo
nitasema: EweMolawangu!Nisahabazangu(hao).Nayeatasema:
Wewe hujui walizua nini baada yako.
Hiyo ni Hadith ya pili katika 'Kitabul Fitan' ya Sahih Bukhari. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 173 iliyoko uk. 144 wa Juzuu ya Tisa.
(v) Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: Umma wangu utanijia kwenye Hodhi; nami nitafukuza watu (siku hiyo) kama mtu anavyofukuza ngamia wa watu (asichanganyike) na ngamia wake. (Waliokimsikiliza) wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, utatujua? Akajibu: Ndio, mtakuwa na alama ambayo mtu mwingine yeyote asiyekuwa nyinyi, atakuwa hana. Mtanijia na paku jeupe juu ya mapaji yenu ya uso, na alama nyeupe juu ya miguu yenu kwa ajili ya athari za udhu. Lakini kundi kati yenu litazuiwa kunifikia. Nami nitasema: Ewe Mola wangu! Hao ni sahaba zangu. Malaika atanijibu kwa kusema: Jee wajua walizua nini baada yako?
Hiyo ni Hadith ya 'Kitabut Twahara', Mlango wa 'lstihbabu Itwalatil Ghurrati Wat Tahjili Fil Wudhui' katika Sahih Muslim. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na.480 iliyoko uk. 156-157 wa Juzuu ya Kwanza.
(vi) Imepokewa kwa Abdullah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: Mimi nitawatangulia kwenye Hodhi; na nitawatetea watu lakini nitashindwa. Hapo nitasema: Ewe Mola wangu! Sahaba zangu, sahaba zangu. Na patasemwa: Wewe hujui walizua nini baada yako. Hiyo ni Sahih Muslim, 'Kitabul Fadhail', Mlango wa 'al-Hawdh'. Kwa Kiingereza, ni Hadith Na. 5690 iliyoko uk. 1238 wa Juzuu ya Nne.
Mpaka hapa tumeona Hadith sita (nyingine tumeziacha!) zinazotutahamisha kwamba kesho Akhera, wakati Bwana Mtume s.a.w.w. atakapokuwa kwenye Hod'ni, baadhi ya sahaba zake watazuiwa kumfikia yeye; na atakapokumb-usha kwamba hao ni sahaba zake, ataambiwa kwamba yeye hajui sahaba hao walizua nini baada yake! Hivyo ni kusema kwamba kuna baadhi ya sahaba amoao, baada ya Bwana Mtume s.a.w.w. kufariki dunia, walizua mambo kinyume cha dini yake; ndiyo sababu wasiruhusiwe kumfikia hata
17
baada ya yeye mwenyewe kukumbusha kwamba hao walikuwa sahaba zake! Jee, sahaba wa aina hiyo bado wangali waadilifu? Jee, aliye mwadilifu hutengwa na Bwana Mtume s.a.w.w.? Huambiwa 'ole wake', kama ilivyo kwenye Hadith Na. (ii) hapo juu?!Neno ole!huambiwa mtu mwema au mwovu?
Kutokana na Hadith hizo basi, ni wazi kwamba sio sahaba wote ni waadilifu. Na vivyo hivyo ndivyo inavyoeleweka kutokana na aya k.w.k. za Qur.'ani Tukufu.
Hata dur'ani Tukufu yasema vivyo
llitusijetukakifanyakirefusanakitabuhiki,hapachinitunatajaaya chache tu zinazoonyesha kwamba si sahaba wote waliokuwa waadilifu:
(i) Mwenyezi Mungu s.w.t. amesema (Sura 9:43): 'Mwenyezi Mungu amekusamehe. Kwa nini umewapa ruhusa? (Ungengoja) mpaka wale wanao-sema kweli wakupambanukie, na uwajue waongo.'
Jee, kutokana na aya hiyo2, si wazi kwamba miongoni mwa sahaba kulikuwa na wakweli na waongo? Ikiwa wakweli ni waadilifu, jee na hao waongo pia huwa waadilifu kwa sababu tu ni sahaba?
(ii) Amesema tena (Sura 8:15-16): 'Enyi mlioamini! Mnapokutana vitani na wale waliokufuru, basi msiwageuzie migongo. Yeyote atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo —isipokuwa kama amegeuka ili kushambulia, au amegeuka ili kuungana na sehemu nyingine (ya jeshi lake) —basi huyo atastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na makaazi yake ni Jahannam. Napo ni marejeleo mabaya'.
Hizo ni aya mbili zilizowaonya sahaba wasikimbie vitani. Maana yeyote miongoni mwao atakayefanya hivyo, isipokuwa kwa nyudhuru mbili zilizotajwa hapo, bila shaka atastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mugu, na makaazi yake ni Jahannam!
Sasa hapa maswali yetu ni haya. Jee, katika historia ya Uislamu, hawa-kupatikana sahaba waliokimbia vitani? Bila shaka walipatikana. Kama ni hivyo, si wazi basi kwamba sahaba hao walistahiki ghadhabu za Mwenyezi Mungu, na makaazi yao ni Jahannam —kama inavyoelezwa katika aya hizo? Jee, mtu anayeghadhibikiwa na Mwenyezi Mungu na kutiwa Jahannam, bado ni mwadilifu?
2.Taz. para ya pili na ya mwisho ya maelezo ya Sheikh Abdullah Saleh al-Farsy ya aya hiyo, yaliyoko uk. 257 wa Tafsir yake, uone anavyosema.
18
(iii) Akasema tena (Sura 9:56): 'Na wanaapa kwa (jina la) Mwenyezi Mungu kwamba wao ni miongoni mwenu, wala wao si miongoni mwenu. Bali wao ni watu wanaoogopa.'
Wazi kabisa hapo kwamba kulikuwa na watu, waliokuwa pamoja na Bwana Mtume s.a.w.w., waliokidhihirisha Uislamu na kuficha kinyume chake! Jee watu aina hiyo huwaje wote waadilifu? Bila shaka hao ni wanafiki, kama tuelezwavyo katika aya ifuatayo:
(iv) Amesema Mwenyezi Mungu s.w.t. (sura 9:101): 'Na miongoni mwa mabedui wanaokaa pambizoni mwenu, mna wanafiki; na katika wenyeji wa Madina (pia). Wamebobea katika unafiki. Wewe huwajui; (lakini) Sisi tunawajua...'
Hapa Mwenyezi Mungu anatweleza wazi wazi kwamba miongoni mwa wale waliokuwa pamoja na Bwana Mtume s.a.w.w. (ambao ndio hao 'sahaba') walikuwamowaumininawanafiki.Nakwambahao wanafiki,yeye Bwana Mtume s.a.w.w. hakiwajua!Aliyekiwajua ni Yeye Mwenyewe s.w.t. Kwa hivyo, baadhi yao waliendelea kuwamo miongoni mwa sahaba mpaka Bwana Mtume s.a.w.w. akafariki dunia.
Hilo, kwa mfano, ii dhahiri mno kutokana na kisa kimoja tu; kisa cha Vita vya Uhud. Imam at-Tabari (katika uk. 504 wa Juzuu ya Pili ya Taarikh yake) na Ibn Hisham (katika uk. 17 wa Juzuu ya Tatu ya as-Siratun Nabawiyya) wamesema kwamba wakati Bwana Mtume s.a.w.w. alipotoka Madina na jeshi lake kwenda Uhud, alitoka na sahaba elfu moja. Lakini Abdullah b. Ubayy b. Salul alimkimbia Bwana Mtume s.a.w.w., akarejea Madina na watu miatatu^. Watu mia tatu hao ni kina nani? Hakuna mahali tulipotajiwa majina yao isipokuwa hilo moja tu la kiongozi wao! Kwa hivyo tuna hakika gani kwamba wanafiki hawamo miongoni mwa hao sahaba tunaoambiwa na Sheikh M. al-Khatib kwamba wote ni waadilifu?
KutoKana na ushahidi mchache tulioutoa hapo juu kutoka katika Qur'ani na Hadith na historia, itadhihiri kuwa si sahaba wote waliokuwa waadilifu, wala si sahaba wote waliokuwa si waadilifu. Kunabaadhi yao waliofikia kilele cha ucha Mungu.Kuna na baadhi waliokuwa wakweli, lakini hawakuwa
3. Pia taz. uk. 229 wa Muhammad Rasulullah ya Muhammad Ridhaa.
19
waadilifu. Kuna na baadhi nyingine ambao hali zao hazikijulikana; na wengine wakijulikana hasa kwamba walikuwa na mambo ya kimatata matata! Na hiyo ndiyo imani ya Kishia. Maana kushikilia tu kuwa sahaba wote ni waadilifu ni kuwatoa katika ubinadamu!
Pia ikumbukwekwambahapahatukugusia wale walioritadi4baada ya Bwana Mtume s.a.w.w. kufariki dunia.Ya hao tumeyaeleza uk.36 humu.
Maafa ya imani hii
MbaYi na kwamba n) kinyume na Qur'ani Tukufu, Hadith za Swana /Vftume s.a.w.w., na hata matukio ya kihistoria, imani hiyo ya kwamba sahaba wote ni waadilifu imeiletea dini yetu ya Kiislamu maafa mawili makubwa:
Kwanza, imeugawanya umma wetu; si katika mambo ya akida tu, bali hata yale ya ibada na va maingiliano (mu'amalaat)5.
Kwa kuwa sahaba wamekuwa na kauli tofauti tofauti juu ya mambo hayo, na wakati mwingine kauli zinazogongana hasa; na kwa kuwa inatakikana iaminiwekwambawoteniwaadilifu,tumelazimikakuyakubaliyote yanayotokana na wao bila ya kupinga!Bali bila ya hata kutumia akili zetu! Hivyo tunajikuta wengine tunaamini kwamba Mwenyezi Mungu haonekaniS; wengine aonekana7! Wengine tunaamini Mwenyezi Mungu yuko juu ya Arshi Yake iliyoko mbinguni huko8; kwa wengine Mwenyezi Mungu hayuko mahali maalum9.Wengine tunaposwali tunafunga mikono10; wengine hatufungpi, na kadhalika12. Na kila kundi linaamini kuwa loo peke yake ndilo lililomo katika haki!
4.Kuritadi ni kutoka katika dini (Uislamu).
5.Inshallah ni nia yetu, tutakapopata wasaa, kuandika kitabu cha kueleza jinsi
madhehebu yalivyozuka na kuenea, na jinsi mingine yalivyokufa.
6.k.v. Shia na Ibadhi.
7.k.v. Sunni na Wahabi. Wao waaamini ataonekana kesho Akhera.
8.Hao ni Wahabi.
9-Hiyo ni imani ya Shia, Sunni na Ibadhi.
10.k.v. Hanafi, Shafi na Hanbali.
11.k.v. Shia. Maliki na Ibadhi.
12.Mmoja katika masultani wa Kiislamu alrtaka kuchagua baina ya madhehebu ya
Shafi na ya Hanafi.Mwanachuoni mmoja akampendekezea ya Shafi kwa kusali
rakaa mbili Kishafi - kwa nguzo, sharuti na sunna zake zote.Kisha akasali rakaa
20
Pili. imesababisha dini yetu kutukanwa na kudharauliwa kwa sababu ya vituko vituko na maajabu ajabu yaliyomo katika vitabu vyetu vya Hadith, kama tulivyoona (kwa mfano) katika uk. 16-32 wa kitabu chetu, Shia na Hadith.
Kwa kuwa Hadith kama hizo zimesimuliwa na masahaba; na kwa kuwa tunalazimishwakuaminikwambasahabawoteniwaadilifu,huwa haturuhusiwi, bali hatuthubutu kamwe, kuwa hata na shaka na Hadith kama hizo—tusije tukatoka Uislamuni!Matokeo yake ni nini? Ni kuziamini na kuzitetea, potelea mbali tuwe vichekesho!
Hatari kubwa!
Pengine, katika kumalizia nukta hii, ingekuwa vyema kama ningedokezea hatari kubwa inayoweza hata kutikisa moja ya misingi mikubwa ya Uislamu, kama watu wataendelea na 'imani ya kwamba sahaba wote ni waadilifu. Maana imani hii ndiyo iliyozalisha ile imani ya kwamba 'kila kilichomo katika Bukhari ni sahihi', kama tulivyoona katika uk. 17 wa kitabu chetu , Shia na Qur'ani.
Kama tutaamini hivyo (na hivyo ndivyo inavyotakiwa Sunni wote waamini) itabidi tuamini kwamba kitabu hicho hakina kosa! Kwa hivyo itabidi, tutake tusitake, tuamini kuwa ki sawa na Qur'ani Tukufu! Maana ni imani ya Waislamu kwamba kitabu, kilicho sahihi chote, ni Qur'ani peke yake. Sasa, kama tutaiongeza na Bukhari, haitakuwa tumeiwekea Qur'ani mwenzake? Jee, hivyo ni sawa? Twataraji tutaelezwa.
mbili nyingine vile inavyoweza kujuzu Kihanafi: 'Alivaa ngozi ya mbwa iliyodibighiwa (iliyotiwa rangi); akaichafua roboo yake kwa najisi. Akatawadha kwa nabidhi (aina ya pombe).Na ilikuwa katikati ya kaskazi, jangwani. Nzi na rnbu wakamkusanyikia
Udhu iwake) ulikuwa kinyumenyume. Kisha akaelekea kibla. Akafunga swala bila ya nia. Akapiga takbiri kwa Kifursi. Kisha akasoma aya kwa Kifursi. Kisha 'akadona' midono miwili kama ile ya jogoo bila ya kusita, na bila ya kurukuu. Mwishowe akasoma tahiyaiu na kujamba pasi na (kirtoa) salamu' Kisha akasema: Ewe Suttan! Hii ndio swala ya Abu Hanifa. Sultan akamwambia: Kama hii sio swala yake, nitakuua. Maana yeyote mwenye dini hawezi kuiruhusu swala kama hii.
Hanafi wakakataa kuwa hiyo ni swala ya Abu Hanifa. Yule mwanachuoni (jina lake ni al-Oaffal) akaagiza viletwe vitabu vya makundi mawili hayo. Sultan naye akamwamrisha mwandishi mmoja wa Kikristo avisome. Naye akayasoma yote madhehebu mawili. Ikaonekana kwamba swala katika madhehebu ya Abu Hanifa ni kama alivyoeleza al-Oaffal. Sultan akayaacha madhehebu ya Abu Hanifa, akafwata ya Shafi! (taz. uk. 174-175 wa Taarikhul Fiqhil Islamiy ya Dkt. Umar Suleiman al-Ashqar)
21
Jee, ni mambo ya ijtihadi?
3. Akaendelea kusema (katika huo huo uk. 30) kwamba Sunni huzingatia:
tafauti zote zilizozuka kati mwao (yaani sahaba) kuwa ni mambo ya ijitihadi13 ambayo walifanya kwa ikhlaswi...
Majibu: Shia hawazingatii hivyo! Wao huzingatia jambo kuwa ni ijtihadi pale tu linapokuwa halipingani na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya
Mtume Wake s.a.w.w.Linapopingana na mojawapo ya vitu viwili hivyo, au vyote viwili,basi jambokamahilo'kwaShia)huwanikosa mojakwa. moja —hata liwe limefanywa na nani!Na hivyo ndivyo msimamo wa Chir'ani Tukufu ulivyo14.
Maana kama tutazingatia kila lililofanywa na sahaba, katika tofauti zao, kuwa ni ijtihadi —hata kama iinapingana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Bwana Mtume s.a.w.w. —na tuogope kusema ni kosa, bila shaka tutakuwa tumefanya sahaba ndio wanaoitawala Qur'ani na Sunna, badala ya Ckir'ani na Sunna kuwatawala wao! Jee, hivyo ni Kiislan u15? Jee, wale wanaomsaidia kazi Sheikh M. al-Khatib wataweza kututh ibutishia, kwa Ckir'ani na Sunna, kwamba (i)sahaba wamepawa uwezo wa kufanya ijtihadi kinyume na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na/au Sunna ya Bwana Mtume s.a.w.w.; na (ii) kwamba Waislamu hawaruhusiwi kukosoa masahaba iwapo imewadhihirikia kwamba ijtihadi zao hizo ni kinyume na hicho Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume Wake s.a.w.w.? Kama wataweza, wanakaribishwa!
Hata hivyo, tunapopekua pekua vitabu (sio vya Kishia!) tunaona misimamo iliyo kinyume na madai ya Sheikh M. al-Khatib.Tunaona kwa mfano, baadhi
13Ijtihadi ni 'kitendo cha kutumia rai katika kutoa hukumu ya kisheria pamojaa
kutoitia maanani nassi iliyopo kinyume chake'
14AmesemaMwenyeziMungu:NaapakwaMolawako;hawawiniwenye
kuamini mpaka wakufanye wewe (Muhammad) hakimu katika yale wanayozozana.
Kishawasioneuzitonyoyonimwaojuuyauliyoyahukumu,nawasalimuamri
kikamilifu (Sura4:65)
Akasema tena: Haimfalii mu'mini mwanamume wala mu'mini mwanamke, Mwenyezi Mungu na iVStume Wake wanapoamua jambo. kuwa na hiari katika jambo lao (hilo). Na mwenye kumwasi Mwertyezi Mungu na Mtume Wake, basi hakika amepotea upotevu ulio wazi. (Sura 3336)
^5 Ajabu r.jpa ni kwamba miongoni mwa wanaoona uzito kuwakosoa sahaba, hata wanapokuwa wanapingana na Qur'ani na Sunna, ni Wahabi —kama Sheikh M. al Khatib —japokuwa wako tayari kuwakufurisha wengine, na hata kuwafanya washirikina. wanapofanya kama hivyo!
22
ya marnbo yaliyofanywa na baadhi ya sahaba, katika tafauti zao, yaliyokataliwa kuwa ni ijtihadi iliyofanywa kwa ikhlaswi! Mengine haya-kufanywa kamwe na sahaba, lakini kwa kuwa yamefanywa na wanaopendwa na Sheikh M. al-Khatib na wenziwe, tunakatazwa kuyakosoa kwa kisingizio cha 'ijitihadi' na 'ikhlaSwi'. Kwa maneno mingine, wasio sahaba wamepawa'usahaba wa heshima'!
Misimamo yenyewe ni kama ifuatayo:
(i)tunaposoma al-Faslu Fil Milali Wan Nihal (uk. 161 wa Juzuu ya Nne) tunamwona Imam !bn Hazm anasema kwamba yule aliyemwua Ammar b. Yasir, yaani Abdul Ghaciiya16, alifanya hivyo kwa ijtihadi ingawa alikosea! Kwa hivyo atapata ujira17mmoja! Kisha akaongeza kusema: 'Lakini huyo si kama wale waliomwua Uthman (r.a.).Maana wao hawana nafasi ya ijtihadi katika kumwua!'
Na vivyo hivyo ndivyo alivyosema Ibn Hajar al-Haytami katika uk. 215 wa as-Swawaiqul Muhriqah!
Sasa, kama yule aliyemwua Ammar alikuwa sahaba; na kama wale waliomwua Uthman b. Affan nao vile vile walikuwa sahaba, kwa nini tukaambiwa kwamba yule aliyemwua Ammar18tu ndiye aliyefanya hivyo kwa ijtihadi na ikhlaswi (kwa hivyo atapata malipo!), lakini sio wale waliomwua Uthman b. Affan?! Hilo dai la Sheikh M.al-Khatib hapo juu limekuwaje? Au kuna sahaba na sahaba; wengine wana ruhusa ya kufanya ijtihadi, na wengine hawana? Tungependa tujulishwe.
Hilo ni la sahaba. Sasa tuangalie ya wasio sahaba!
(ii) tunapotazama uk. 484 wa Juzuu ya Kumi ya al-Muhalla, tunamwona
16.Jina lake kamili ni Yisar b. Sabu'i al-Juhani. Yeye ni miongoni mwa waliomsikia
Mtume s.a.w.w. akisema:Hakika damu zenu na mali zenu ni haramu...' Hivyo sahaba
walikistaajabu sana kuwa mtu kama huyo, baada ya kusikia maneno kama hayo kwa
Bwana Mtume s.a.w.w., alijitolea kumwua Ammar b. Yasir! (taz. uk. 150 wa Juzuu ya
Nne ya al-lsaba)
17.Ujira maana yake ni 'malipo'.
18.Ukumbuke Ammar huyu ni yule ambaye Sura 39:9, 6:52, 16:106, 6:122, na 28:61
ziliteremshwa kwa ajili yake pekee au pamoja na wenziwe wengine. Mbali zile Hadith za Bwana Mtume s.a.w.w. zisemazo kuwa Ammar amejaa imani —tangu utosini hadi kwenye kidole gumba, na kwamba imani imechanganyika na nyama yake na damu yake, na kwamba ni haramu Moto kula au kuigusa damu yake, na kadhalika (taz. uk. 22 - 28 wa Juzuu ya Tisa ya al-Ghadir).
23
tena Ibn Hazm akitwambia kwamba yule aliyemwua Imam Ali a.s., yaani Abdulrahman b. Muljam, alifanya hivyo kwa ijtihadi!
Subhanallah! Vipi itakuwa hivyo hali Ibn Muljam hakuwa sahaba kamwe19? Au kwa kuwa aliyeuawa ni Imam Ali a.s., ambaye Shia wanamtambua kuwa ndiye Imam wao wa kwanza, ndio mwuaji huyo akapawa usahaba wa heshima20?
Ikumbukwe; Imam Ali a.s. aliuawa kwa upanga akiwamo ndani ya swala, kibulani!
(iii) tukija kwenye uk. 9 wa Juzuu ya Kumi na Tatu ya Taarikh Ibn Kathir, twamwona AbdulKhair as-Shafi'i21akisema kuwa Yazid alikuwa 'imamu
19.Taz. uk. 67-68 wa Maisha ya al-lmam Aly ya Sheikh Muhammad Kasim Mazrui
uone jinsi huyo Ibn Muljam alivyohadawa na mwanamke, kwa kusalitika naye, hata
akajitolea kumwua 'Mpenzi wa Mwenyezi Mungu'!
20.Linganisha heshima hiyo anayopawa aliyemwuaImam Ali a.s., na hukumu
zifuatazo zilizotoiewa kwa wanaomtukana tu Abubakar na Umar ndipo utakapoelewa
chuki inavyofanya kazi:
Katika uk. 23 wa Juzuu ya Pili ya Mis'bahudDhwalaam amesema al-Jurdani kwamba wanazuoni wengi wanasema kwamba anayemtukana Abubakar na Umar huwa kafiri.
Ibn Kathir naye anasema (uk. 324 wa Juzuu ya Kumi ya Taarikh yake) kwamba Isa b. Ja'far b. Muhammad aliuawa kwa amri ya al-Mutawakkil al'Allah kwa kumtukana
Abubakar, Umar, Aisha na Hafsa!
Na katika uk. 575 wa as-Swarimul Maslul ya Ibn Taymiya imeandikwa kwamba Kadhi Abu Ya'la aliulizwa kuhusu mwenye kumtukana Abubukar. Akasema: Kafiri. Akaulizwa: Asaliwe? Akajibu: La! Akaulizwa afanyweje naye asema 'Laa ilaaha illallah?' Akajibu: Msimguse kwa mikono yenu. Msukumeni kwa ubao mpaka mumtumbukize shimoni mwake!
Ukumbuke, ewe ndugu Mwislamu, kwamba Abubakar mwenyewe alipotukanwa mbele za Bwana Mtume s.a.w.w., Bwana Mtume s.a.w.w. hakutoa hukumu hiyo iliyotolewa na mashekhe hao, bali alitabasama tu! (taz. uk. 436 wa Juzuu ya Pili ya Musnad Ahmadl. Bali yeye mwenyewe Abubakar alipotukanwa na mtu, na Abu Barzatal Aslami akataka kumwua mtu huyo, alimkaripia na kumwambia: Hilo (la kuuawa mtu kwa kutukana mtu) si la yeyote baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w.! (taz. uk. 109-111 wa Juzuu ya Saba ya Sunanun Nasai)
Basi vipi mashekhe hao wanatutolea hukumu zao kinyume na ile ya Bwana Mtume s.a.w.w., na hata ya Abubakar mwenyewe? Au kwa nini wanamwacha aliyemwua Imam Ali a.s. katika hukumu zao? Jiulize.
21.Huyualikuwani mufassir,naalikisomeshakatikaChuochaNidhamiya, Saghdad. Alifariki mwaka 590H.
24
mujtahid'! Lakini ujue kwamba Yazid mwenyewe hakuwa sahaba! Yeye alizaliwa baada ya Bwana Mtume s.a.w.w. kufariki dunia; na kama vitabu vya historia vinavyoeleza, alikuwa mlevi, hasharati, mcheza na mbwa, na sifa nyingine rnbaya mbaya! Yeye ndiye aliyetuma watu kumwua Imam Husein a.s.22baada ya babake, Muawiya b. Abi Sufyan, kumtawalisha23 juu ya Waislamu kimabavu!
•Hiyo basi ni mifano miwili ya wasio sahaba tunaoambiwa kwamba walifanya waliyofanya kwa ijtihadi na ikhlaswi.Mbali ya wale waliompiga vita Imam Ali a.s. wakasababisha Waislamu wengikufa24!Kuna na wale waliomlaani imamu huyo juu ya mimbari2^ na kuwaua waliokataa kumlaani!Sikwambii 22.Katika kueleza jinsi Imam Husein a.s. alivyouawa. Sheikh Abdullah Saleh Farsy, katika uk. 37 - 38 wa Maisha Ya Sayyidnal Huseyn amesema hivi: 'Alipowajibu kwa yakini kuwa hakubali kwenda kuuawa na Ubeydillah na kudhalilishwa. wanaume na wanawake na watoto waiiwazunguka darmadar wasiwe na njia ya kupenya na kukimbia.Wakakosa maji na chakula tangu hapo mwezi nane Mfunguo Nne, 61 mpaka mwezi kumi 61H; hapo wakaingia kuwapiga baada ya kuwa hawajifai kwa njaa na kiu. Wakapigana kwa ushujaa mkubwa kabisa usiokuwa na mfano. Wakaua zaidi ya idadi ya hao kuwaua wao ... Na Sayyidnal Husein anawalinda wanawake na waliotaka kuwashambulia au kuwafanya mambo mabaya.Kisha wakamzingira kila upandekwakumpigakwamishare,mikukinapanga mpakaakaangukachini wakamkata kichwa.Na qawli mashuhuri kuwa aliyemkata kichwa ni Shimr bin
Dhiljawshan —baba yake alikuwa sahaba.' Sheikh Farsy akamalizia:Pesa na kutaka ukubwa kunafanya kazi.'
23.!. Taz. uk. 18 - 29 wa Maisha Ya Sayyidnal Huseyn uone jinsi Sheikh Abdullah Saleh Farsy alivyoeleza kwa tafsili vile Muawiya b. Abi Sufyan alivyombandika mwanawe, Yazid, kimabavu juu ya Waislamu.
24.K.m. inakisiwa kwamba wale waliokufa katika Vita vya Siffin peke yake ni baina
ya 70 000 na 110 000, wakiwamo miongoni mwao sahaba 25 waliowahi kupigana
katika Vita vya Badr pamoja na Bwana Mtume s.a.w.w. (taz. uk. 404 - 405 wa Juzuu ya
Pili ya Murujudb Dhahab).
25.Wa kwanza ni Muawiya b. Abi Sufyan.Yeye ndiye aliyeanzisha jambo hilo.
Alikimlaani Imam Ali a.s. katika hotuba yake ya kila Ijuman juu ya mimbari.Na ili
watu waweze kuisikia laana hiyo siku za Idd, mtu huyo aliibaiilisha sunna ya Bwana
Mtume s.a.w.w.Badala ya hotuba kuwa baada ya swala, akaiweka kabla ya
swalai
Wengine ni kama vile Busr b. Artwaat. Mughira b. Shu'ba, Marwar b. al-Hakam. Ziyad b. Sumayya,nawengi wengineo.
Desturi hii ya kumlaani Imam Ali a.s. iliendelea kwa miaka -ningi sana —tangu pale alipouawa mwaka 40H mpaka Umar b. Abdulaziz aliposhika Ukhalifa mwaka 99H. Yeye ndiye aliyeipiga marfuku desturi hiyo; akaiondoa hiyo laana, na badala yake akaiweka Sura 16:90 ambayo husomwa hadi hii leo katika hotuba zote za misikiti ya Sunni.
25
waliomwua Imam Hasan a.s., mjukuu wa Bwana Mtume s.a.w.w., wakasherehekea kifo chake na kuzuia2^ asizikwe karibu na babu yake! Jee waliomwua Hujr b. Adiy27? Waliomwua Malik b. Nuwaira28? Waliomwua Muhammad b. Abubakar29, mtoto wa Khalifa wa Kwanza? na wengi wengineo! Jee, wote hao walifanya hivyo kama Sheikh M. al-Khatib atakavyo tuamini, kwa ikhlaswi? Kama walioua, waliua kwa ikhlaswi, nini hukumu ya waliouliwa? Nani hapo amemdhulumu mwenzake? Au wote wawili —walioua na waliouliwa —wamedhulumiwa? Amua mwenyewe, ewe ndugu Mwislamu.
Kwa hivyo anaposema Sheikh M. al-Khatib kwamba Sunni huzingatia tofauti zote zilizozuka kati ya masahaba kuwa 'ni mambo ya ijtihadi' ambayo waliyafanya 'kwa ikhlaswi', amekusudia mambo kama hayo tuliyoyataja hapo juu. Kwa maneno mingine, shekhe hapo anatwambia kwamba Sunni wanaamini kuwa hao walioua wenzao watapata malipo mawili, kama wamewaua kwa haki! Na kama walikosea, basi watapata malipo mamoja! Kwa nini? Kwa sababu walifanya hivyo 'kwa ijtihadi na ikhlaswi'!
Ewe ndugu Mwislamu!Kama wewe ni Sunni, jee unakubaliana na Sheikh M. al-Khatib hapo? Au unakubaliana na msimamo wa Shia kwamba lazima
26.AJiyezuiahivyoniMarwanb.al-Hakamambayewakatihuoalikuwa
ameshauzuliwa. Alifanya hivyo ili kumfurahisha Muawiya! (taz. uk. 13 -14 wa Juzuu
ya Kumi na Moja ya al-Ghadir ya Sheikh Abdulhusein Ahmad al-Amini).
27.Hujr alikuwa ni sahaba wa Bwana Mtume s.a.w.w. aliyesifiki kwa wema mtupu.
Yaye, pamoja na sahaba wengine kumi na moja. walikataa kumlaani Imam Ali a.s.
walipoamrishwa kufanya hivyo na Muawiya na vibaraka wake.Sita kati yao
wakauawa;mmoja,aliyekiKwaAbdulrahmanb.Hasanal-'Anziy,aliuliwakwa
kuzikwa mzima mzimal
28.Malikb.NuwairaaliuawanaKhalidb.al-Walidambaye,sikuhiyohiyo
aliyomwua alimwoa mjane wake aliyekuwa mzuri sana!Jee, tusemeje na hao ni
sahaba?
29.Huyu ni mtoto wa Khaiifa Abubakar. Kwa sababu alikuwa upande wa Imam Aii
a.s., aliuawa kinyama.Sheikh Muhammad Kasim Mazrui anatwambia, katika uk. 66
wa Maisha Ya al-lmam A/y: 'Baada ya kumtesa, walimkata kata viungo kimoja kimoja
mpaka akakata roho!Na yote hayo yu kimya, hapigi kelele wala halalaiki mpaka
akafakishujaa!Baadayaukatilihuo.wakamtiakatikakiribachapunda,
wakamchoma motol'
26
kesi za watu hao ziamuliwe kufuatana na Ckir'ani na Sunna ya Bwana
Mtume s.a.w.w.30?
Haifai kujenga mashjngo31
4. Akaendelea kusema:
...na hali walizozifanyia ijtihadi zimekwisha wala haifai kwetu kujenga mashingo juu
ya tafauti hizo, yakawa yatadumu kwa vizazi vyenye kuendelea. Majibu: Ni kweli; hali ambazo sahaba walrfanyia ijtihadi zao zimekwisha. Lakini athari yake ingaliko hadi leo, na itaendelea kuwako maadam baadhi ya Waislamu wanazifumbia macho ijtihadi hizo na kukataa kuzikabili kiume, na kuzitolea hukumu za Kiislamu kama ilivyoamrishwa katika Sura 4:59.
Maadam baadhi ya Waislamu wanakataa uamuzi wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake s.a.w.w. kwa sababutu uamuzi huo unakubaliwa na wapinzani wao, basi bila shaka chuki itaendelea kati yao hadi kwa vizazi vinavyofuatia. Isipokuwa, labda, hao wapinzani wao nao wakubali kuutupilia mbali huo uamuzi wa Mwenyezi Mungu na Bwana Mtume s.a.w.w.!Na hilo ni muhali. Maana kama watakubali kufanya hivyo, kwa kweli kutabaki Uislamu?
Hebu tutazame mifano miwili mitatu tu ya sunna sahihi za Bwana Mtume s.a.w.w. ambazo wasio Shia wanashauriwa kuziacha kwa sababu tu Shia wanazifuata!!
(i) Katika kueleza 'kushabihiana na rawafidh3^, Ibn Taymiya amesema hivi
katikauk. 142waJuzuuyaPiliyakitabuchakekiitwachoMinhajus
Sunnah:
'Kutoka hapa ndiyo wanazuoni wa fiqhi wakafikia kuacha baadhi ya
sunna zinapokuwa ni alama yao.Maana, ingawa kuziacha (sunna) hizo si wajibu, lakini zinapodhihirishwa, huwa ni kushabihiana nao.Hivyo
30.Kwa kufanya hivyo —yaani kuwahukumu sahaba kwa mujibu wa Our'ani na
sunnah, na kutangaza hukumu hizo - ndipo inaposemwa kuwa Shia wanatukana
sahaba!
31.Mashingo maana yake ni 'chuki".
32.Hilinijinaambalowalewapinzaniwao,hupendakuwaitiaShia. LakiniShia
wenyewe hawalikubali jina hilo kwa sababu linaipotoa historia.
huwa hatambuliwi Sunni ni yupi na Rafidhi ni yupi. Na maslaha ya kupambanua baina yao, kwa ajili ya kujitenga nao na kuwa tofauti nao, ni makubwa kuliko maslaha va sunna hiil'
Haya! Huyo ni Ibn Taymiya ambaye, kwa wote wale wanaopinga bid'a, na kwa wale wasiomjua, ni Shaikhul Islam na Muhyis Sunna (Mfufuzi wa Sunna ya Bwdna Mtume s.a.w.w.)! Ikiwa yeye, na wote wale wanaomfuata, wamekuwa tayari kugombana33na watu ili sunna za Mtume s.a.w.w. zisiongezwe, vipi hapo wako tayari kuziacha kwa sababu tu Shia wanazifuata? Ndicho Kiislamu, au ndicho Wi-ansaarus sunnah? Ndiyo tuseme Waislamu wanapoona jambo jema linatendwa na wapinzani wao, waliache ili tu wawe tofauti nao?
Hasha! Mwenyezi Mungu ametukataza kuishiriki chuki kiasi hicho kwa kutwambia (Sura 5:8): 'Wala chuki dhidi ya watu (fulani) isiwapelekee kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. (Kufanya) hivyo ni karibu zaidi na ucha Mungu.'
(ii) SheikhMuhammadb.Abdulrahmanad-Dimishqiamesemakatika
kitabu chake kiitwacho Rahmatul Ummah Fikhtilafil Aimmah kilichochapwa
pambizoni mwa al-Mizan ya as-Sha'rani (uk. 99-100 wa Juzuu ya Kwanza):
'Sunna ya kaburi ni tastwih34.Hilo ndilo bora katika kauli yenye nguvu
katika madhehebu yaShafi.NaAbuHanifa naMalik naAhmad
wamesema:Tasnirr>35ni bora, maana tastwih imekuwa nialama ya Shia!
33. Ni jambo lihalojulikana kwamba kuna watu wanaowaita wengine makafiri au mushrikina kwa sababu tu wanatawasali, au wanasoma maulidi, talkini au hitima. au wanaweka nadhiri makaburini, na kadhalika. Watu hao huwakufurisha wengine hivyo kwa kuwa ati wamefanya jambo ambalo halikufanywa na Bwana Mtume s.a.w.w. Na katika kufanya hivyo,huwa wanamfuata huyo Ibn Taymiya tuliyemtaja hapo juu! Sasa lipi kubwa hapo? Kufanya ambaio halikufanywa na Mtume s.a.w.w., ingawaje hakulikataza, au kuliondoa lililofanywa na yeye?
34Tastwihnikuutandazamchangawakaburi,baadayakulifunika,likawa
tambarare.
35Tasnim ni kuukusanya mchanga wa kaburi, baada ya kulifunika, likawa na nundu
kama ya ngamia.
28
Ghazali naye, na Mawardi, wamesema: Kufanyia tastwih makaburi ndilo lililowekwa na sheria. Lakini, ilipokuwa Rafidha wame/ifanya ni alama yao, tumeliacha na kufanya tasnim!
Na mwandishi wa al-Hidaya ya Hanafi amesema: Lililowekwa na sheria ni kuvaa pete mkono wa kulia. Lakini, ilipokuwa Rafidha wameshikilia hivyo, tunaivaa mkono wa kushoto36!
Ewe ndugu Mwislamu! Hiyo ni mifano michache tu ya jinsi baadhi ya mashekhe walivyo tayari kuwaelekeza wafuasi wao (wa Kisunni) waache baadhi ya sunna za Bwana Mtume s.a.w.w. kwa sababu tu zinafuatwa na Shia. Ikiwa kwenye mambo madogo madogo tu, kama hayo ya makaburi na pete, wako tayari kwenda kinyume na Bwana Mtume s.a.w.w. watashindwa kufanya hivyo katika mambo yanayohusiana na utawala, na manufaa ya kidunia?Au yanayohusiana na uhai wao?
Hapo ndipo penye mushkeli. Chuki baina ya Waislamu haitaondoka kwa kukubaliana kwamba tuyanyamaze yale yaliyotendwa na sahaba; maana kufanya hivyo ni sawa na kukiri kwamba dhalimu na mdhulumiwa ni sawa. Chuki itaondoka, na hivyo itakoma kuendelea mpaka kwa vizazi vijavyo, pale tu Waislamu watakapokubaliana (i) kwamba hakuna sahaba wa Kisunni wala wa Kishia; sahaba wote ni wa Bwana Mtume s.a.w.w.; (ii) wote ni binadamu, wanaopata na kukosa; (iii) kila mmoja katika wao ni lazima ahukumiwe na Qur'ani na Sunna; (iv) yule ambaye matendo yake yamewafikiana na Qur'ani na Sunna, huyo amesibu, na atahukumiwa hivyo; (v) yule ambaye matendo yake yamekwenda kinyume na Qur'ani na Sunna, huyo amekosea, na atahukumiwa hivyo. Wakikubaliana hivyo, ushindi hautakuwa ni wa uDande mmoja dhidi ya mwingine ila utakuwa ni wa Haki; na Haki ni Mwenyewe Mola s.w.t. Na hayo ndiyo ambayo wanazuoni wa madhehebu mbali mbali walikutana kuyajadili kwa lengo la kutafutia njia za kuleta umoja na uelewan'o baina yao —jambo ambalo Sheikh M. al-Khatib, kwa bahati mbaya, alilitungia kitabu chake hiki tunachokijibu, kulipinga!