ArticleIDPicAddressSubjectDate
{ArticleID}
{Header}
{Subject}

{Comment}

 {StringDate}
 
 
 
 
 
 
 
ViewArticlePage
 
 
 
  • SHIA NA SAHABA (3)  
  • Sendtofriend
  •  
  •  
  • Sahaba hawana makosa?

    5. Akaendelea tena kusema (katika huo huo uk. 30):

    Kamwe wao ndio ambao Mwenyezi Mungu amesema kuhusu wao maneno Dora

    36.Tazama mambo hayo! Yakifika hapo, tusemeje?

    29


    ambayohakuyasemakwawatuwowote.Amewasifumahalikwingina akawakanushia makosa khaswa.

    Majibu: Ni kweli kwamba Mwenyezi Mungu amesema maneno bora na kuwasifu sahaba wa Bwana Mtume s.a.w.w. Lakini haya. ni kwa wale waliostahiki sifa hizo kati yao. Ama wale waliostahili kulaumiwa na kukaripiwa, kwa sababu ya vitendo vyao viovu, Mwenyezi Mungu hakuwaacha. Amewafichua37!

    Kuhusu Mwenyezi Mungu kuwakanushia makosa; hilo hatukumbuki limesemwa wapi katika Qur'ani Tukufu. J

    Hata hivyo, dai hilo si rahisi kukubalika tunapokumbuka ile mifano ya makosa mbalimbali yaliyofanywa na masahaba, na ambayo tumetangulia kuitaja katika kitabu hiki38. Mbali ile Hadith ya Bwana Mtume s.a.w.w., ambayo wanazuoni wengi wa Kisunni huitolea ushahidi, isemayo: 'Hakika mimi ni binadamu; hupata ha hukosea!'

    Kwa hivyo, ikiwa Bwana Mtume s.a.w.w. aweza kufanya makosa, vipi sahaba wake watakanushiwa hilo?

    Juu ya hayo, unapotazama uk. 32 wa kitabu chake (mstari wa 8-9 kutoka juu), utamwona shekhe wetu huyo anavyoona vigumu kuamini kuwa maimamu 'wamehifadhiwa na kukosa'. Ikiwa ni hivyo kwa maimamu, vipi anataka sisi tuamini basi kuwa sahaba wamekanushiwa makosa?

    Sahaba wasituhumiwe?

    6. Akamalizia maneno yake kuhusu msimamo wa Sunni:

    Basi haifai kwa yoyote kuwatuhumu baada ya sifa hizo.Wala halina maslaha hilo

    kwa yoyote.

    Majibu: Kama tulivyosema, sahaba walikuwa ni binadamu; na kama binadamu wote walivyo, hawakuwa daraja moja. Wako waliokuwa bora kuliko wengine39.Kuna na waliokuwa wacha Mungu na pia waliokuwa

    37.Tazama, kwa mfano, Sura ya at-Tawba na at-Munafiqun katika dur'ani Tukofu,
    utayaona hayo.

    38.Taz. uk. 14-20 humu. Pia kwa wale wanaojua Kiarabu, nawatazame uk. 82 (chini
    ya Hadith Na. 60) na uk. 83 - 84 (chir.i ya Hadith Na. 61) wa Juzuu ya Kwanza ya
    SilsilatulAhadithidh Dha'ifa WalMawdhu'a
    ^heikh iVuhammad Nasiruddin al-Albany
    ambaye ni mpinga bid'a mkubwa!

    39.Mwenyezi Mungu anasema:... Hawawi sawa miongoni mwenu wale waliotoa
    kabla ya kushinda na wakaendelea kupigana.Hao wana darajb kubwa zaidi kuliko
    wale ambao wametoa baadaye na wakapigana ...' (Sura 57:10)

    30


    walevi na wazinifu40.Jee, ni haki basi kuwachanganya wote hao asijulikane yupi ni yupi?

    Kwa mfano, inajulikana kwamba miongoni mwa sahaba wako waliomsingizia41Mw. Aisha, mke wa Bwana Mtume s.a.w.w. mambo machafu! Wako waliotoka msikitini, wakamwacha Mtume s.a.w.w. anahutubu juu ya mimbari siku ya Ijumaa, kukimbilia biashara42na pumbao! Wako hata waliomtuhumu43Bwana Mtume s.a.w.w. katika kugawa sadaka! Jee, wote hao, na wengine wengi kama hao, tuwapokee sawa na wale waliokaa na Bwana Mtume s.a.w.w.kwa wema, tangu mwanzo hadi mwisho? Jee, huo utakuwa ni uadilifu? Bila shaka la!

    Hapo basi ndipo penye hitilafu baina ya Sunni na Shia. Sunni waona, kama anavyopendekeza Sheikh M. al-Khatib hapo juu, kwamba sahaba wasituhumiwe kwa uovu hata kama wameufanya! Shia waona la! Aliyefanya uovu, na ikathubutu kuwa ni uovu, sio kosa kumtuhumu. Maana kwa kutofanya hivyo, tutakuwa tumemwachia nafasi sahaba huyo aonekane ni mwema hali si mwema! Na madhara yake msimamo huo wa kumfanya mwema asiye mwema u wazi mno; hauhitajii hata kuelezwa.

    Hata hivyo kuna upande mwingine wa suala hili, unaofanywa na Sunni, na ambao Sheikh M. Khatib yaonekana hakupenda kuutaja.Nao ni huu:

    Sheikh ametwambia hapo juu kwamba 'haifai kwa yeyote kuwatuhumu' sahaba. Lakini hakutukataza lililo kubwa zaidi; la kumpa cheo, sio aliyemtuhumu sahaba wa kawaida tu, bali aliyemtukana na kumlaani bora ya sahaba wote!

    Tunaposoma vitabu vya Kisunni tunaona watu waliokimtukana na kumlaani Imam Ali44a.s. zinapokewa Hadith zao, pamoja na wao wenyewe kuitwa

    40.Tazuk. 14.15 humu.

    41.Taz.Sura 24:11-20.

    42.Taz. Sura 62:11 na maelezo yake katika Tafsir ya Sheikh Abduilah Saleh al-Farsy.
    43.. Taz.Sura9:58-59.

    44.Imam Ali huyo, kama inavyoelezwa katika vitabu k.w.k., ndiye mwanamume wa kwanza kusilimu.Ndiye wa kwanza kusali pamoja na Bwana Mtume s.a.w.w. Ndiye yule ambaye Bwana Mtume s.a.w.w. alimteua kuwa wasii na khalifa wake baada yake, na sifa nyingi nyingine ambazo zinahitaji kitabu kizima lau tutazikusanya zote! Pia taz. uk. 37-42 humu.

    31


    thiqah (wenye kutegemeka au waaminifu)! Jee? Kama Sunni, sio kwamba hawawalaumu tu watu kama hao ambao imethubutu (katika vitabu vyao wenyewe!) kwamba walikimlaani Imam Ali a.s. (ambaye kwao ni mmoja kati ya 'Makhalifa Wanne Walioongoka'), bali wanawapa daraja hiyo ya u-thiqah, vipi Sheikh M. al-Khatib anazuia watu wasiwatuhumu wale waliothubutu kuwa ni waovu? Lipi lililo ovu zaidi hapo? Kutuhumu sahaba, au kumlaani? Kama kina Sheikh M. al-Khatib wako tayari kuwalaumu wale wanaotuhumu sahaba wa kawaida tu, kwa nini waogopa kuwalaumu wale waliokimlaani Imam Ali a.s. ambaye fadhila zake tushaziona uk. 37 humu? Jee hiyo ni insafi?

    Kwa faida ya wasomaji wetu, na wale wanaomsaidia kazi Sheikh M. a.l-Khatib, hapa chini tunatoa mifano miwili mitatu tu ya watu aina hiyo:

    (i>Hariz b. Uthman: Huyu, alipokuwa akisali msikitini, alikuwa hatoki mpaka amlaani Ali, Amirul Mu'minina, laana sabini kila siku!

    Amesema Ismail b. Ayyash: Niliandamana na Hariz kutoka Misr mpaka Makka, akawa anamtukana Ali na kumlaani. Akaniambia: Haya (maneno) yanayosimuliwa na watu kwamba Mtume s.a.w.w. amemwambia Ali: 'Wewe kwangu u daraja ya Harun kwa Musa45' ni kweli. Lakini aliyeyasikia amekosea! Nikamwuliza: (Sawa) ni vipi? Akasema: Ni 'Wewe kwangu u mahali pa Oarun46kwa Musa'! Nikamwuliza: Umemsikia nani? Akasema: Nimemsikia al-Walid b. Abdilmalik akisema hivyo juu ya mimbari! (taz. uk. 115 wa Juzuu ya Nne ya Taarikh Ibn Asakir, na uk. 268 wa Juzuu ya Nane ya Taarikhul Khatib.)

    Haya! Kisha mtu kama huyo Hadith zake zapatikana katika Sahih Bukhari, Sunan AbiDawud, Sunan Tirmidhi, na vinginevyo!

    (ii) Khalid al-Oash: Alikuwa 'nasibiy47, mwenye chuki, dhalimu mkubwa'. Hivyo ndivyo alivyoelezwa na Imam Dhahabi48

    Na katika uk. 20-21 wa Juzuu ya Kumi ya Taarikh Ibn Kathir imeelezwa

    45.Hii ni Hadith ambayo imepokewa katika vitabu vingi vya Hadith vya Kisunni k.v.
    Sahih Bukhari,Sahih Muslim,SunanTirmicJhi,Sunan Ibn Majah,Musnad Ahmad,
    Mustadrak, Majmauz Zawaid,
    na vinginevyo.

    46.Huyu alikuwa binami yake Nabii Musa a.s., lakini alikuwa akimpinga.Vipi
    atalinganishwa na Imam Ali a.s. ambaye, ingawa vile vile alikuwa binami yake Bwana
    Mtume 8.a.w.w., lakini alikuwa mstari wa mbele katika kumuunga mkono na
    kumtetea? Tazama chuki inavyofanya kazi!

    47.Nasibiy ni yule mwenye chuki na uadui na Imam Ali a.s. na wafuasi wake.

    48.Tai. uk. 633 wa Juzuu ya Kwanza ya Mizanul l'tidal.

    32


    kwamba 'alikuwa mtu mwovu aliyekimtukana Ali b. Abi Twalib.Mamake alikuwaMkristo,naye(huyoKhalid)alikituhumiwakatikadiniyake. Alimjengea mamake kanisa katika nyumba yake!'

    Mtu kama huyo ameitwa thiqah na Ibn Hibban!

    (iii) lshaq b. Suwaid al-Adawi al-Basri: Alikuwa akimshambulia Ali vikali sana. Naalikisema:Simpendi Ali49!

    Mtu kama huyo ameitwa thiqah na Imam Ahmad, Ibn Mu'in, na Nasai; na Hadith zake zimo katika Sahih Bukhari, Sahih Muslim, Sunan Abi Dawud, na Sunan Nasai! (taz. uk. 236 wa Juzuu ya Kwanza ya Tahdhihut Tahdhib ya Ibn Hajar al-Asqalani.)

    Jee, wale wanaomsaidia kazi Sheikh M. al-Khatib wanaweza, kwa upande wao, kutweleza maslaha ya kuacha kuwatuhumu watu kama hao ambao, bila shaka, misimamo yao ni kinyume na Qur'ani na Sunna ya Bwana Mtume s.a.w.w.?

    49.Ikiwa yeye asama hivyo, na Bwana Mtume s.a.w.w. asema kuwa asiyempenda Ali ni mnafiki (taz. Sahih Muslim), vipi mtu huyo atakuwa thigah? Jamani!

    33


    SAHABA KWA SHIA

    1. Amesema Sheikh M. al-Khatib, katika uk. 30 wa kitabu chake hicho, kwamba:

    Mashia wanaona kwamba maswahaba walikufuru baada ya kuondoka Mtume (s.a.w.) wasiokuwa watu kidogo katika wao hawapati idadi ya vidole vya mikono miwili.

    Majibu: Waliosema kwamba sahaba walikufuru baada ya Bwana Mtume s.a.w.w. kuondoka sio Shia. Aliyesema hivyo ni mwenyewe Mtume Muhammad s.a.w.w., kama ilivyoelezwa katika Sahih Bukhari, Sahih Muslim na Musnad Ahmad:

    1. Imepokewa kwa Ibn Abbas kwamba: Mtume s.a.w.w. alisimama kati yetu akasema: Hakika nyinyi mtakusanywa (kesho Akhera) miguu chini, uchi na mkiwa mazunga50... na kwamba watu katika umma wangu wataletwa wachukuliwe kushoto (yaani Motoni). Hapo nitasema: Ewe Mola wangu! (Hao ni) sahaba wangu. Na Mwenyezi Mungu atasema: Hakika wewe hujui walizua nini baada yako. Nami nitasema kama alivyosema mja mwema (Nabii Isa a.s.): Nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa miongoni mwao. Lakini uliponifisha, Wewe ndiwe uliyekuwa'Mlinzi juu yao; na Wewe ni Shahidi juu ya kila kitu. Kama utawaadhibu, wao ni waja Wako; na kama utawasamehe, basi Wewe ndiwe Mwenye nguvu, Mwenye hekima. (Sura 5:117-118) Hapo patasemwa:Hakika wao hawakuacha kurejea nyuma kwa visigino vyao51.

    Hadith hiyo utaipata katika 'Kitabur Riqaq', Mlango wa 'al-Hashr' katika Sahih Bukhari, na vile vile katika 'Kitabul Jannati Waswifati Na'imiha Wa Ahliha', Mlango wa 'Fanaud Dunya Wabayanul Hashri Yawmal Oiyamah' katika Sahih Muslim.

    50.Zunga ni mtu ambaye hakutahiriwa.

    51.Yaani, hao walirejea ukafirini!

    34


    Kwa Kiingereza ni Hadith Na. 533 iliyoko uk. 349 wa Juzuu ya Nane y; Sahih Bukhari; na Hadith Na. 6847 iliyoko uk. 1487 wa Juzuu ya Nne ya Sahih Muslim.

    2.Imepokewa kwa Asmaa bint Abubakar kwamba Mtume wa Mwenyezi
    Mungus.a.w.w.amesema:NitakuwakwenyeHodhiiliniwaonewale
    watakaonijia kati yenu.Lakini baadhi ya watu watazuiwa kunifikia.Hapo
    nitasema:Ewe Mola wangu!(Hao ni) wafuasi wangu na ni katika umma
    wangu.Patasemwa: Jee, watambua walifanya nini baada yako? Naapa kwa
    Mwenyezi Mungu, hawakufanya wema na walirejea (nyuma) kwa visigino
    vyao...

    Hadith hiyo imo katika Sahih Bukhari, 'Kitabur Riqaq', Mlango wa 'al-Hawdh'; na katika Sahih Muslim, 'Kitabul Fadhail', Mlango wa 'Hawdhu Nabiyyina (s.a.w.w.) Waswifatuhu'.

    Kwa Kiingereza ni Hadith Na. 592 iliyoko uk. 385-386 wa Juzuu ya Nane ya Sahih Bukhari; na Hadith Na. 5684 iliyoko uk. 1236-1237 wa Juzuu ya Nne ya Sahih Muslim.

    3.Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu
    s.a.w.w. amesema:Kundi la sahaba wangu litanijia Siku ya Kiyama, lakini
    watafukuzwa kwenye Hodhi.
    Hapo nitasema: Ewe Mola wangu!(Hao ni)
    sahaba wangu.Naye atasema: Wewe hujui walizua nini baada yako.Wao
    walirejea nyuma kwa visigino vyao.

    Hadith hiyo imo katika Sahih Bukhari,'Kitabur Riqaq',Mlango wa 'al-Hawdh'. Kwa Kiingereza niHadithNa. 6585 iliyoko uk. 382 wa Juzuu ya Nane.

    4.ImepokewakwaUmmuSalamakwambaMtumes.a.w.w.
    amesema:Miongoni mwasahaba wangu kuna ambaye sitamwona wala
    hataniona baada ya mimi kufa abadan...

    Hadith hiyo utaiona katika uk. 298 wa Juzuu ya Sita ya Musnad Ahmad.

    Tunapozitazama Hadith hizo tulizozitaja hapo juu, ambazo sio zote, tunaona kwamba kesho Akhera Bwana Mtume s.a.w.w. atakuwako kwenye Hodhi. Sahaba wake watataka kumwendea; lakini baadhi yao watazuiwa kumfikia! Bwana Mtume s.a.w.w. atawatapia na kusema kwamba hao ni sahaba wake; lakini ataambiwa kwamba, ingawa ni hivyo, yeye hajui sahaba hao walifanya nini baada ya yeye kufariki dunia! Wao waliritadi; walitoka katika dini ya Kiislamu! Hapo Bwana Mtume s.a.w.w. atajibari (atajitenga) nao kwa kusema,kamaatakavyosemaNabiiIsaa.s.atakapojibarinaWakristo

    35


    waliomwabudu hapa duniani, maneno yaliyomo katika Sura 5:117-118. Na hao bila shaka ndio hao aliosema kwamba yeye hatawaona, wala wao hawatamwona abadan.

    Kwa hivyo, kutokana na Hadith hizo, ni wazi kwamba kuna baadhi ya watu, kati ya sahaba wa Bwana Mtume s.a.w.w., walioritadi baada yayeye kufariki dunia.NahayoyamesemwanamwenyeweMtumeMuhammad s.a.w.w.; sio Shia. Lakini swali hapa ni: jee, walioritadi ni wengi au kidogo?

    Sahaba wengi waliritadi

    TunaposomaHadithifuatayo,tunamwonaBwanaMtumes.a.w.w. anatwambiakwambawatakaoritadinakutiwaMotoniniwengi! Wachache tu ndio watakaosalimika nao:

    5. Imepokewa kwa Abu Hureira kwamba Mtume s.a.w.w. amesema: Nilipokuwa nimelala, mara kundi (la wafuasi wangu likaletwa). Nilipowajua, alitoka mtu (malaika) akakaa baina yangu na yao. Akasema: Njooni. Nikasema: Wapi? Akasema: Motoni, Wallahi! Nikasema: Kwani wamefanya nini? Akasema: Wao walirejea nyuma kwa visigino vyao baada yako. Kisha mara kundi jingine (likaletwa). Nilipowajua, alitoka mtu (malaika) akakaa baina yangu na yao. Akasema: Njooni. Nikasema: Wapi? Akasema: Motoni! Nikasema: Kwani wamefanya nini? Akasema: Wao walirejea nyuma kwa visigino vyao baada yako. Basi sikumwona yeyote, miongoni mwao, aliyesalimika isipokuwa (wachache) mfano wa ngamia wasio na mchungaji.

    Hivyo ndivyo alivyosema Bwana Mtume s.a.w.w. kama ilivyo katika Sahih Bukhari, 'Kitabur Riqaq', Mlango wa 'al-Hawdh'.

    Kwa Kiingereza ni Hadith Na. 587 iliyoko uk. 383-384 wa Juzuu ya Nane.

    Tunapotazama maelezo ya Hadith hiyo, kama yalivyo katika uk. 475 wa Juzuu ya Kumi na Moja ya Fathul Bari, tunamwona Imam Ibn Hajar al-

    Asqalani anasema kwamba makusudio ya ngamia wasio na mchungaji ni 'wachache. Maana ngamia wakosao mchungaji ni kidogo ukiwalinganisha na wengineo.' Kwa hivyo, kutokana na Hadith hiyo, ni wazi kwamba watakaosalimika na Moto, kati ya sahaba, ni wachache mfano wa ngamia waliokosa mchungaji. Na aliyesema hivyo ni Bwana Mtume s.a.w.w.; sio Shia!

    Lakini jee, uchache wenyewe ni kwamba hawapati hata idadi ya vidole vya mikono miwili?

    36


    Neno kwa neno au majazi?

    Sheikh M- al-Khatib, katika kueleza imani ya Shia, amesema (uk.30) kwamba Shia wanaamini kwamba sahaba waliokufuru baada ya kuondoka Bwana Mtume s.a.w.w. ni 'kidogo... hawapati idadi ya vidole vya mikono miwili.'

    Majibu: Kama Sheikh M. al-Khatib hapo ametumia maneno: hawapati idadi ya vidole vya mikono miwili kimajazi52, majibu yetu ni: Ndio. Maana itakuwa ni sawa na kusema, kama alivyosema Bwana Mtume s.a.w.w., kwamba 'walikufuru wengi isipokuwa kidogo'.

    Lakini kama ameyatumia maneneo hayo ki-neno kwa neno, basi majibu yetu ni: La! Shia hawasemi wala hawaamini hivyo. Maana, kwa kuyatumia maneno hayo hivyo, itakuwa ni sawa na kusema kwamba Shia wanaamini kwamba sahaba wote walikufuru isipokuwa 'chini ya watu kumi'! Na hivyo sivyo... kwa sababu moja nzima, mbali nyinginezo. Nayo ni hii:

    Jinsi Shia watakavyokuwa tayari kuwakufurisha sahaba, ni muhali kwamba watakuwa tayari kuwakufurisha hata wale, miongoni mwao, waliopigana upande wa Imam Ali a.s. katika vita vyake dhidi ya Muawiya. Na hao, bila shaka, hawakuwa kumi. Walikuwa ni mamia, kama si maelfu. Kwa hivyo Shia hawawezi kusema, wala hawasemi, kwamba sahaba ambao hawakukufuru 'hawapati kumi'.

    Daraja ya Imam Ali

    2. Akaendelea kusema shekhe wetu (uk.31) kwamba Shia: wanamweka Aliy kwenye daraja makhususi kabisa...

    Majibu: Hilo ni kweli. Daraja ambayo Shia humpa Imam Ali a.s. hawampi yeyote kati ya sahaba wa Bwana Mtume s.a.w.w.; na hilo ni kwa sababu hivyo ndivyo alivyotukuzwa na mwenyewe Bwana Mtume s.a.w.w. kama Hadith ifuatayo inavyosema:

    Umar b. Maimun amesema: Nilikuwa nimekaa kwa Ibn Abbas. Mara akajiwa na viongozi tisa; wakamwarnbia: Ewe Ibn Abbas! Ama inuka utufwate, au waambie hawa waondoke watwache peke yetu. Ibn Abbas akasema: Nitainuka niwafwate. Hapo alikuwa angali mzima; hajawa kipofu. Wakazungumza, lakini hatujui walizungumza nini. Mara akarejea huku anakukuta nguo zake na kusema: Ole wao! Wanamtaja kwa ubaya mtu mwenye fadhila kumi ambazo hakuna yeyote mwingine mwenye nazo. Wanamtaja kwa ubaya mtu ambaye Mtume s.a.w.w. amesema:

    52.Kutumia neno 'kimajazi' ni kulhumia kwa maana isiyokuwa yake kikawaida

    37


    (i) Bila shaka (kesho) nitamtuma mtu ambaye Mwenyezi Mungu hatamhizi53abadan; ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanampenda yeye. Wakaitamani (fadhila) hiyo wenye kuitamani! (Mtume s.a.w.w.) akasema: Yuko wapi Ali? Mara akaja huku macho yanamwuma, haoni. (Mtume s.a.w.w.) akayapulizia macho yake. Kisha akaitingisha beremu54mara tatu; akampa. Ali akarejea55 na Swafia bint Huyay.

    Ibn Abbasakasema:

    (ii)Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. alimtuma mtu fulani56 kuwasomea (makafiri wa Makka) Sura at-Tawba. Nyuma yake akamtuma Ali, akaichukua kwake (huyo fulani). (Mtume s.a.w.w.) akasema: Hakuna wa kwenda nayo (sura hii) isipokuwa mtu anayetokana na mimi, na mimi nikatokana na yeye.

    Ibn Abbas akaendelea kusema:

    (iii) Mtume s.a.w.w. aliwaambia binami zake: Yupi kati yenu yu tayari kuwa rafiki yangu hapa duniani na Akhera? Ali, ambaye alikuwapo hapo, aliinuka akasema: Mimi nitakuwa rafiki yako hapa duniani na Akhera. Wale wengine hawakujibu kitu. (Mtume s.a.w.w.) akasema: Wewe ndiye rafiki yangu hapa duniani na Akhera.

    Ibn Abbas akasema tena:

    (iv) Ali ndiye mtu wa kwanza, baada ya Khadija57, kumwamini (Mtume Muhammad s.a.w.w.) Na vile vile:

    (v) MtumewaMwenyeziMungus.a.w.w.alichukuakishalichake, akamfunika Ali, Fatima, Hasan na Husein.Kisha akasoma: Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa Nyumba (ya Mtume), na kuwatakasa kikamilifu. (Sura 33:33) Akasematena Ibn Abbas: (vi) Ali aliiuza nafsi yake kwa kulala kitandani (mwa Mtume s.a.w.w.) na

    53.Hatamhizi maana yake 'hatamwaibisha' au hatamtweza.

    54.Buremu maana yake 'bendera'.

    55.Yaani, kutoka kwenye Vita vya Khaibar.

    56.Mtu wenyewe alikuwa ni Khalifa Abubakar as-Siddiq.

    57.Mw. Khadija r.a. ndiye mke wa kwanza wa Bwana Mtume s.a.w.w., na ndiye wa
    kwanza kumwamini.Kabla ye yeye kufariki, Bwana Mtume s.a.w.w. hakuoa mke
    yeyote mwingine.

    38


    kujifunika guo lake huku washirikina (wa Makka) wakimvurumizia mawe.

    (vii) Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alitoka (Madina), pamoja na watu wengine, kwenda kwenye Vita vya Tabuk. Ali akamwambia: Nikufwate? (Mtume) s.a.w.w. akasema: La! Ali akalia. Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. akamwambia: Jee, huridhiki wewe kuwa daraja yako kwangu ni kama ya Harun kwa Musa isipokuwa kwamba hakuna mtume baada yangu? HakikahaiwezekanimimikuondokanisikwacheweweKhalifawangu.

    (viii) Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia (Ali a.s.):Wewe ndiye mtawalia (mambo ya) kila mu'mini mwanamume na mu'mini mwanamke baada yangu.

    (ix) Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliifunga milango yote ya Msikiti (wake) isipokuwa mlango wa Ali. Ikawa huingia msikitini humo hali ana janaba. Hiyo ilikuwa ndiyo njia yake; hakuwa na njia nyingine isiyokuwa hiyo.

    (x) Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. alisema: Yeyote ambaye mimi^ nimemtawalia mambo yake,basi na Ali(pia)ndiye mwenye kumtawalia mambo yake.

    Imam al-Hakim, baada ya kuitoa hiyo Hadith ya mwisho, amesema: Hii ni Hadith ambayo sanad yake ni sahihi japokuwa (Bukhari na Muslim) hawakuitoa58. Na Imam Dhahabi naye ameitoa katika kitabu chake, Talkhis, nakusema: Nisahihi.

    Hadith hiyo, ambamo ndani yake Ibn Abbas amezidondoa hizo fadhila kumi za Imam Ali a.s. ambazo hakuna sahaba yeyote mwingine mwenye nazo, unaweza kuiona katika vitabu vifuatavyo vya Kisunni: uk. 502 wa Juzuu ya Pili ya al-lsaba ya Ibn Hajar al-Asqalani, chini ya jina ia Ali b. Abi Twalib; uk. 330-331 wa Juzuu ya Kwanza ya Musnad Ahmad; uk. 122-123 wa Juzuu ya Tisa ya Majma'uz Zawaid; uk. 132 wa Juzuu ya Tatu ya al-Mustadrak ya Imam Hakim; uk. 183 wa Juzuu ya Kwanza ya Tarikh Dimishq ya Ibn Asakir as-Shafi'i, chini ya jina la Ali b. Abi Twalib; na vitabu vinginevyo k.w.k.ambavyo tumeviacha kwa kuogopa kukirefusha kitabu hiki.

    Kutokana na fadhila zilizotajwa katika Hadith hiyo, na nyingine nyingi za kipekee ambazo inshallah tutazitolea kitabu chake maalum, nataraji itaelewekakwaniniShiawamemwekaImamAlia.s.'kwenyedarajs

    58. Hivyo ieleweke kwamba si lazima Hadtth iwemo katika Sahih Bukhari na Sahih Muslim ndiyo iwe sahihi. Kuna Hadrth k.w.k. zilizo sahihi, hata kwa kufuatana na masharti ya yeye Bukhari na Muslim, ambazo hawakuzitia katika vitabu vyao!

    39


    makhususi kabisa'.Kusema kweli, hilo lataka lifanywe na Waislamu wote; sioShia pekg yao.

    Imam Ali a.s. ni wasii

    3. Shekhe wetu akaendelea kusema (uk. 31):
    Wengine wanamwona kuwa ni wasii...

    Majibu: Nikweli;Shiawanaaminikwamba,kablayaBwanaMtume

    s.a.w.w.kufarikidunia,tayarialikuwaarneshamchaguaImamAlia.s.

    kuwa wasii wake.Na hilo li wazi kutokana na Hadith zifuatazo ziiizomo katika

    vitabu vya Kisunni: (i) Mwenyezi Mungu s.w.t. alipoteremsha Sura 26:214 isemayo:Waonye

    jamaa zako walio karibu (nawe),Bwana Mtume s.a.w.w. aliwaalika jamaa

    zake nyumbani kwa ami yake, Abu Twalib.Jumla walikuwa kiasi cha watu

    arobaini hivi ambao, miongoni mwao, walikuwamo Abu Twalib,Hamza,

    Abbas na Abu Lahab.Mwisho wa karamu hiyo, Bwana Mtume s.a.w.w.

    aliwahutubia waliokuwapo kwa maneno haya:

    Enyi wana wa Abdulmuttalib! Hakika mimi simjui kijana kati ya Waarabu aliyewaletea watu wake jambo bora kuliko lile nililowaletea mimi nyinyi. Hakika nimewaletea nyinyi kheri ya dunia hii na Akhera; na Mwenyezi Mungu ameniamrisha niwalinganie nyinyi kwenye (kheri) hiyo. Basi yupi kati yenu aliye tayari kunisaidia mimi katika jambo hili ili awe ndugu yangu, wasii wangu na Khalifa wangu miongoni mwenu? Wote waliokuwapo hawakujibu kitu isipokuwa Ali, ambaye alikuwa ndiye

    mdogo wao wote. Yeye alisimama akasema:

    Mimi, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nitakuwa waziri wako katika jambo hilo. Hapo Bwana Mtume s.a.w.w. akaweka mkono wake shingoni mwa Ali a.s.,

    akasema:

    Hakikahuyundiyenduguyangu,wasii wangunakhalifawangu miongoni mwenu. Basi msikilizeni na mumtii.

    Waliokuwapo wakainuka kuondoka, huku wakicheka na kumwambia Abu

    Twalib: Amekwamrisha umsikilize mwanayo na kumtii!

    Hadith hiyo, katika vitabu vya historia, utaipata katika uk. 319-321 wa Juzuu

    ya Pili ya Tarikh at-Tabari; uk. 62-63 wa Juzuu ya Pili ya Tarikh Ibnil Athir; uk.

    311 wa Juzuu ya Kwanza ya Siratul Halabiyya; na pia uk. 85 wa Juzuu ya

    Kwanza ya Tarikh Dimishg ya Ibn Asakir.

    40


    - -.-■-■■■- -^SS:^


    Katika vitabu vya Hadith, utaipata katika uk. 131-133 wa Juzuu ya Kumi na Tatu ya Kanzul Ummal; na Muntakhab Kanzil Ummal iliyoko pambizoni mwa uk. 41-42 wa Juzuu yaTano ya Musnad Ahmad.

    (ii) Imepokewa kwa Abu Ayub al-Ansari kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. alimwambia binti yake, Fatima: Jee hukujua kwamba Mwenyezi Mungu Aliyetukuka aliwatazama watu wa ardhi (hii),akamteua babako kati yao, akamfanya Mtume? Kisha akatazama mara ya pili, akamteua mume wako, akaniteremshia wahyi mimi, nikamwoza (wewe) na nikamfanya wasii (wangu)?

    Hadith hiyo utaipata katika Muntakhab Kanzil Ummal iliyoko pambizoni mwa uk. 31 wa Juzuu ya Tano ya Musnad Ahmad; na pia katika uk. 256 wa Juzuu ya Nane ya Majma'uz Zawaid.

    Na katika uk. 168 wa Juzuu ya Tisa ya Majma'uz Zawaid, katika Hadith iliyopokewa kwa Ali b. Ali al-Hilali, mna maneno haya: '...nawasii wangu ndiye bora wa mawasii, na anayependeza mno kwa Mwenyezi Mungu; naye ni mume wako...'

    ni\ utaiona katika Muntakhab Kanzil Ummal iliyoko pambizon/ mwa »3 J -zuu ya TanQ ya Musnad Ahmad.


    &fui3U)s its e^^^JZI^ZZJ^Zl^' ~Slr~~^


    LJ,'7,(t>,'^"5»e


    .\enye pap TalWewe utanilioia c/en( eai

    sauti yangu, na utawabainishia (la sawa) watakapohitalifiana


    (iii) Imepokewa kwa Abu Said al-Khudri kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: Wasii wangu, na mweka siri zangu, na bora ya nitakaowaacha baada yangu, mtekelezaji ahadi zangu na mlipaji deni zangu ni

    na uk. 486 wa Juzuu ya Pili ya Tarikh Dimishq ya Ibn Asakir

    (v) Imepokewakwa BuraidakwambaMtumes.a.w.w.amesema:Kila Mtume ana wasii na mrithi; na Ali ndiye wasii wangu na mrithi wangu.

    59.Yaani, utawafikishia ujumbe wangu.



    41


    Katika vitabu vya Hadith, utaipata katika uk. 131-133 wa Juzuu ya Kumi na Tatu ya Kanzul Ummal; na Muntakhab Kanzil Ummal iliyoko pambizoni mwa uk. 41-42 wa Juzuu ya Tano ya Musnad Ahmad.

    (ii) Imepokewa kwa Abu Ayub al-Ansari kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. alimwambia binti yake, Fatima: Jee hukujua kwamba Mwenyezi Mungu Aliyetukuka aliwatazama watu wa ardhi (hii),akamteua babako kati yao, akamfanya Mtume? Kisha akatazama mara ya pili, akamteua mume wako, akaniteremshia wahyi mimi, nikamwoza (wewe) na nikamfanya wasii (wangu)?

    Hadith hiyo utaipata katika Muntakhab Kanzil Ummal iliyoko pambizoni mwa uk. 31 wa Juzuu ya Tano ya Musnad Ahmad; na pia katika uk. 256 wa Juzuu ya Nane ya Majma'uzZawaid.

    Na katika uk. 168 wa Juzuu ya Tisa ya Majma'uz Zawaid, katika Hadith iliyopokewa kwa Ali b. Ali al-Hilali, mna maneno haya: '...nawasii wangu ndiye bora wa mawasii, na anayependeza mno kwa Mwenyezi Mungu; naye ni mume wako...'

    (iii) Imepokewa kwa Abu Said al-Khudri kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w.w. amesema: Wasii wangu, na mweka siri zangu, na bora ya nitakaowaacha baada yangu, mtekelezaji ahadi zangu na mlipaji deni zangu ni Ali b. Abi Twalib.

    Hadith hii utaiona katika Muntakhab Kanzil Ummal iliyoko pambizoni mwa uk. 32 wa Juzuu ya Tano ya Musnad Ahmad.

    (iv)Imepokewa kwa Anas b. Malik kwamba Mtume (s.a.w.w.) alitawadha, akaswali rakaa mbili na akamwambia: Mtu wa kwanza atakayekwingilia mlango huu ni kiongozi wa wacha-Mungu, bwana wa Waislamu, mlinzi wa dini, na mwisho wa mawasii... Mara akaingia Ali a.s., na Mtume s.a.w.w. akasimama na kumkumbatia kwa furaha huku akimpangusa jasho lililokuwako kwenye paji lake la uso, na kumwambia: Wewe utanilipia deni zangu, utawas-ikilizisha59(watu) sauti yangu, na utawabainishia (la sawa) watakapohitalifiana baada yangu.

    Hadith hii utaiona katika uk. 63 wa Juzuu ya Kwanza ya Hulyatul Aw/iyaa; na uk. 486 wa Juzuu ya Pili ya Tarikh Dimishq ya Ibn Asakir

    (v) Imepokewa kwa Buraida kwamba Mtume s.a.w.w. amesema: Kila Mtume ana wasii na mrithi; na Ali ndiye wasii wangu na mrithi wangu.

    59.Yaani, utawafikishia ujumbe wangu.

    41


    Hadith hii utaipata katika uk. 5 wa Juzuu ya Tatu ya Tarikh Dimishq ya Ibn Asakir; na uk. 178 wa Juzuu ya Pili ya ar-Riyadhun Nadhira.

    Hizo basi ni Hadith tano za Bwana Mtume s.a.w.w., tulizozitoa katika vitabu vya Kisunni, zionyeshazo kwamba Imam Ali a.s. alikuwa wasii wa Bwana Mtume s.a.w.w. Mbali zile zilizomo katika vitabu vya Kishia. Ndiyo ikawa Shia huamini hivyo.

    Ali a.s. hukuwa Mtume

    4. Akasema tena shekhe wetu (uk. 31): ...wengine wanamwona kuwa ni mtume...

    Majibu: Hilo si kweli. Maana kuamini hivyo, kwa Shia Ithnaashari, ni ukafiri. Kwa hivyo hakuna Shia Ithnaashari hata mmoja anayeamini hivyo. Kama wale waliokiswahilisha kitabu cha Sheikh M. al-Khatib wataweza kututajia kitabu kimoja tu (juzuu na ukurasa) cha Shia kisemacho hivyo, tutafurahi.

    Ali a.s. si Mungu

    5.Akasema tena (hapo hapo uk. 31):
    ...na wengine wanamwona kuwa ni Mungu!

    Majibu: Astaghafirullah! Uwongo! Wamesema wapi hivyo? Twaomba vile vile tutajiwe kitabu chao (juzuu na ukurasa) ambamo mmeandikwa maneno hayo ya kikafiri.

    Imam Ali a.s. na waliomkhalifu

    6.Shekhe akamaliza maneno yake kwa kusema (uk. 31):

    BaadayahivyowanawahukumuWaislamukwakulingananamsimamowao

    kukhusu Aliy.Yeyote aliyechaguliwa kuwa Khalifa kabla ya Aliy, basi mtu huyo ni

    dhalimu au ni kafiri.Na yoyote aliyemkhalifu Aliy kwa rai (fikra) basi mtu huyo ni

    dhalimu au ni kafiri au ni fasiki; na ni vivyo hivyo mwenye kuwakhalifu watoto wake.

    Majibu: Kama tulivyokwisha kuona humu, ni imani ya Shia kwamba kabla

    ya Bwana Mtume s.a.w.w. kufariki dunia alikwisha kuusia Ali a.s. awe'

    Imam baada yake. Kwa bahati mbaya, na kwa sababu ambazb hapa si mahali

    pake kuzieleza,hilo halikuwa!Pamoja na hivyo Shia hawamwiti kafiri mtu

    anayekataa kuamini hivyo.Husema tu kwamba mtu huyo si Shia.Maana

    imanihiyo,kwao,si katikamisingiyaUislamu;nikatikamisingiya

    kimadhehebu.Tazama,kwamfano,maelezo ya jambo hilo yaSheikh

    42


    Muhammad Jawad Mughniya katika uk. 158-159 wa Hawlal Wahdatil Islamiyya.

    Pia unapotazama uk. 126-127 wa Aslus Shia Wa Usuuluhaa utamwona Sheikh Muhammad al-Husayn Kashiful Ghitaa akisema kwamba linalomfanya mtu kuwa Mwislamu ni kuamini tawhidi, utume na Siku ya Malipo. Hapo utaona kwamba hakutaja Uimamu wa Ali a.s.

    Hali kadhalika, dkija kwenye uk. 23-24 wa al-Fusulul Muhimmah Fii Ta'lifil Ummah, utaona jinsi al-lmam Abdulhusayn Sharafuddin alivyozipanga Hadith, kutoka katika vitabu vya Kishia, zionyeshazo kwamba yeyote anayepiga shahada, akasimamisha swala, akatoa zaka, akahiji Makka na kufunga Ramadhan basi huyo ni Mwislamu ambaye, mbali na kwamba ni haramu kumwua, inaruhusiwa kuoana na kurithiana naye. Sasa basi, ikiwa mambo ni hivyo, vipi itawezekana Shia kuwa na msimamo huo wanaosingiziwa na Sheikh M. al-Khatib? Bila shaka, hata kama kutakuwako wenye mawazo kama hayo, hatuwezi kusema kwamba huo ndio Ushia. Tutasema tu kuwa hayo ni mawazo ya baadhi ya Shia yaliyo kinyume na mafunzo ya Ushia; kama vile ambavyo hatuwezi kuulaumu Usunni kwa mambo yanayotendwa na Sunni kinyume cha mafunzo yake.

    Mwisho

    Kutokana na majibu na maelezo yetu yaliyomo humu, tumeona kwamba:

    (i) kuna hitilafu baina ya Sunni na Shia kuhusu taarifa ya sahaba. Kwa kuwa Qur'ani Tukufu wala Sunna za Bwana Mtume s.a.w.w. hazikutwachia taarifa maalum, hatwezi kumwita kafiri yeyote kati yao asiyekubali taarifa ya mwenziwe;

    (ii) kinyume na inavyoaminiwa na Sunni, si kweli kwamba sahaba wote ni waadilifu. Maana kama tutaamini hivyo, itatubidi (Mungu apishe mbali) tuikadhibishe Qur'ani Tukufu, Sunna za Bwana Mtume s.a.w.w., na hata historia yenyewe kwa vile ambavyo vyote hivyo vimerekodi makosa, bali maasia hasa, yaliyofanywa na baadhi ya sahaba;

    (iii) hata hivyo, hilo halina maana kwamba sahaba wote si waadilifu. Hasha!Ni imani ya Shia kwamba wako sahaba waadilifu ambao wamesifiw-' hivyo na Mwenyezi Mungu s.w.t., na Mtume Muhammad s.a.w.w. pia;

    (iv) si imani ya Kishia kwamba Imam Ali a.s. alikuwa Mtume wala kwamba ni Mungu. Imani yao ni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mmoja asiye na mshirika, na kwamba Muhammad s.a.w.w. ni Mtume wa mwisho.Pia ni

    43


    imani ya Kishia kwamba yeyote asiyeamini hivyo ni kafiri. Hata hivyo, kwa kuwa Sheikh M. al-Khatib aliyaandika madai hayo bila ya kuyatolea ushahidi wa vitabu vya Kishia, tumewaomba wasaidizi wake watufanyie hivyo watakapotujibu ili nasi tuje na majibu yetu kwa ukamilifu.

    (v) Shia, kwa ushahidi uliomo katika vitabu vyao vya Hadith (na hata ule uliomo katika baadhi ya vitabu vya Kisunni), wanaamini kwamba Imam Ali a.s. alikuwa wasii wa Bwana Mtume s.a.w.w. Hata hivyo, hawaamini kwamba yeyote aliye- au anayemkhalifu si Mwislamu. Wao husema tu kuwa si Shia; na

    (vi) sio kweli kwamba Shia wanawachukia sahaba. Maana kama ni hivyo, wasingalikuwa wanawaombea Mwenyezi Mungu kwa ile dua tuliyoichapisha humu.

    Kwa hivyo, kama mambo ni kama hayo, kwa nini Sunni wazuiwe kukurubiana na kuelewana na ndugu zao, Shia? Kwa nini Wahabi wametuzukia na njama hii sasa ambapo twaona jinsi watesi wasio Waislamu wanavyozidi kutafuta njia za kusuluhiana? Tafadhali, ewe ndugu msomaji, yape maswali mawili hayo uzito yanayoustahiki.

    Inshallah, katika kitabu kijacho, tutatazama msimamo wa Shia juu ya taqiya.

    44