ArticleIDPicAddressSubjectDate
{ArticleID}
{Header}
{Subject}

{Comment}

 {StringDate}
 
 
 
 
 
 
 
ViewArticlePage
 
 
 
  • SHIA NA SAHABA (4)  
  • Sendtofriend
  •  
  •  
  • KIJALIZO

    Barua Na. 1

    6th November, 1989 Assalaam Alaykum,

    RE: MAJADILIANO

    Mzozo wa Ushia na Usuni umekuwa mkubwa na athari yake kwa wasiokuwa Islam itakuwa mbaya. Na nimefikiria mimi kutukuwa khatwa ya kusuluhisha mzozo huu.

    Tangu zamani fikra ya wengi katika sisi ni kuwa ITIKADI ya Shia haifungamani na mafunzo ya Qur'ani. Nasi tukiamini hiyo ni dini mbali; sasa kwa kuwa wewe, kwr. jitihadi yako, umetatukiwa kuwa ITIKADI ya Shia yalingana na nassi ya Our'an, nimeona ni bora kuwakutanisha maulamaa wa pande zote mbili, uweze kuwafahamisha uvumbuzi wako. Katika moja ya cassette zako umesema kuwa uko tayari kulifanya hilo. Na mimi niko tayari kuitisha mkutano huo.

    Nakuhakikishia mkutano huo utakuwa ni wa maulamaa wa pande zote mbili peke yao na makusudio ni kuwathibitishia masunni kwa nassi za Qur-an pekee maoni yako juu ya Ushia.

    Nakuhakikishia hakutakuwa na vitendo vyovyote vya kuleta uharibifu katika hafla hiyo.

    Ikiwa u tayari kwa hilo tafadhali niarifu niweze kuipanga mipango ya mkutano huo.

    Akhuk,

    MUNIR M. K. MAZRUI c.c. IMKL:

    Maimamu wote wa Msikiti (Mombasa)

    45


    Barua iSia.2

    17.11.198©

    Assalaamu Alaykum,

    Yah: MAJADILIANO

    Nakushukuru kwa barua yako ya 6.11.89 ambayo nasikitika sikuweza kuijibu

    kabla ya leo kwa sababu ya kuchelewa kuipata.Barua yenyewe ilifika Bilal

    Muslim Mission ya Mombasa baada ya kuwa nishaondoka kuja huku Nairobi

    ambako nimeletewa hivi juzi.

    Hata hivyo, kabla sijaijibu barua yako kwa urefu, nitashukuru kama utanipatia

    orodha na anwani za watu uliowapelekea nakala za barua yako hiyo ili nami

    niweze kuwapelekea nakala za majibu yangu.

    Tafadhali niachie orodha hiyo kwa sahibu yangu, Bashir M. Chandoo (dukani

    kwake), ambaye kwa nakala hii namjulisha kuipokea na kuniwekea mpaka

    nitakapokuja huko wiki ijayo inshallah.

    Wassalaam Alaykum.

    Nduguyo, ABDILAHI NASSIR

    n.k. Bw. Bashir M. Chandoo S.L.P. 84202 MOMBASA

    Barua Na. 3

    30th November, 1989 Assalaam Alaykum,

    MAJADILIANO Ahsanta kwa barua yako ya tarehe 17th November, 1989 ambayo nimeipata

    leo tarehe 30th November, 1989.

    Nakala za barua hiyo nimewapelekeya maimamu wote miskiti ya Mombasa na masheikh wafuatao.

    ShariffAbdallah Mohamed
    ,,Ahmed Badawy

    ,,Abdulrahman Ahmed Khitami

    SheikhNassor M. Nahdy Nassor Bin Khamis

    46


    SheikhAli M. Sheikh Islam Khiyar Ali Abdalla Khamis Hammad Moh'd Kassim.

    Anwani za wote hawa sina. Barua zilikwenda kwa mkono. Sina shaka kuwa Sheikh Bashir M. Chandoo aweza kufanya kazi hiyo maadam wote hao ni wakazi wa Mombasa.

    Akhuk, MUNIR M. K. MAZRUI

    c.c. Sheikh Bashir M. Chandoo

    BaruaNa417th December, 1989

    Assalaamu alaykum, Yah: MAJADILIANO

    Ahsanta sana kwa barua yako ya 30.11.1989 niliyoipata 2.12.1989. Hata hivyo nasikitika, kwa sababu ya shughuli na safari nyingi, sikuweza kukujibu kabla ya leo. Na hata hii jawabu ya leo sitadiriki kuitia sahihi kwa kuwa naondoka kwenda ng'ambo; kwa hivyo nimemwachia mwanangu aitie sahihi kwa niaba yangu.

    Katika barua yako ya 6.11.1989 ulieleza wasiwasi wako juu ya athari mbaya kwa Uislamu inayoweza kutokana na fitna iliyosababishwa na kampeni ya watu fulani kuwakufurisha Shia Ithnaashari. Fitna hii, kwa kweli, imetuhuzunisha sote; na nakubaliana nawe kwamba lazima hatua zichukuliwe kulisuluhisha tatizo hili, na'kuwafikiwa ni kwa Mwenyezi Mungu. Jambo ambalo siwafikiani nawe ni lile dai lako kwamba 'tangu zamani fikra ya wengi katika sisi ni kuwa itikadi ya Shia haifungama'ni na mafunzo ya Qur'ani. Nasi tukiamini hiyo ni dini mbali...' Hilo ndilo silikubali; maana ukweli wa mambo ulivyo ni kinyume cha hivyo!

    Kwa miaka mingi sana huku kwetu Afrika Mashariki, mbali sehemu nyingine za ulimwengu wetu, Shia Ithnaashari wamekuwa wakiishi pamoja na ndugu zao, Sunni, bila ya chuki. Pamoja na tofauti za kimadhehebu zilizoko, wamekuwa wakishirikiana kama ndugu Waislamu. Viongozi na mashekhe wakubwa wakubwa wa Kisunni walikihudhuria na kuhutubia hafla za Shia, na

    47


    Shia nao walikialikwa na wakihudhuria hafla za Sunni. Sunni walikiwatia mashaurini ndugu zao Shia, na Shia wakishiriki katika mashauri yote yanayowahusu Waislamu kwa jumla nchini, kama vile sharia za mirathi, ndoa na talaka n.k. Vile vile, katika halmashauri zote muhimu za mambo ya Kiislamu, k.m. Kamati ya Utangazaji Vipindi vya Kiislamu, iliyokuwa chini ya Kadhi Mkuu, na Kamati ya Kutunga Silabasi (man-haj) ya masomo ya dini shuleni, utawakuta Shia wakishirikiana na ndugu zao Sunni. Ukija upande wa vyama vya Kiislamu, utakuta vyama mbalimbali vilivyobuniwa, na vyengine mpaka leo, vyasimamiwa na Sunni pamoja na ndugu zao Shia. Mbali walioowana.

    Mpaka hivi majuzi tu palipozuka watu wanaofuata siasa za madola fulani yanayopingana na misimamo ya Kiislamu ya Jamhuri ya Iran, ndipo tulipobwagiwa shindo la 'ukafiri' wa Shia, kwa sababu tu viongozi na wengi wa raja wa Iran ni Shia Ithnaashari. Watu hao wamejaribu kutumia fikra ya kimakosa, waliyonayo baadhi ya Sunni na wenye ilimu chache, kuwa itikadi ya Shia Ithnaashari hailingani na misingi ya Uislamu, ili kuwachochea wawakufurishe hao ndugu zao, wapate na kuitenga Iran. llihali watu hao hao, mpaka hivi juzi na jana, ndio waliokuwa wakiwakufurisha Sunni kwa ajili ya baadhi ya itikadi za madhehebu yao walizozifanya ni shirk na kufr wakawagawanya makundi makundi, kila moja likilikufurisha lenziwe! Tulipoona athari mbaya itakayoufikia Uislamu na Umoja wa Waislamu kutokana na fitna hiyo, tulifanya wajibu wetu wa kuwakanya wale wenye kuieneza. Hilo li wazi ukizisikiliza/ukitizama kanda za darasa zangu za miaka ya nyuma. llipokuwa hawakukanyika, bali wakazidi kueneza bughdha baina ya Waislamu, ilitubidi tuwaeleze wale wasiojua hakika ya Ushia na hitilafu baina yao na madhehebu ya Kisunni ili wasiweze kutekwa na fitna hiyo. Ndio hivi majuzi nikaweka darasa mahususi na kuanza kuandika vitabu ili kuonyesha kuwa itikadi za Shia Ithnaashari zimetegemezwa Qur'ani na Sunna, na kuwa hakuna hitilafu kubwa hivyo baina yao na Sunni hata iwazuie kukurubiana na kuelewana. Kama nitafaulu kulithibitisha hilo, tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwa maslaha ya Waislamu wote, inshallah. Namshukuru Mwenyezi Mungu kuona kwamba wenzangu sasa waiona hatari ya jambo hili kutosuluhishwa. Kwa hivyo nakubaliana na wewe kuwa iko haja ya kuwaleta 'ulamaa wa pande zote mbili kulijad'li hilo ili kuepusha sui-tafahum baina ya makundi mawili haya ya Waislamu.Kwa upande wangu mimi, jii

    48


    tayari kufanya kila niwezalo kuufaulisha mkutano huo. Lakini kwanza nahitaji maelezo zaidi juu ya mambo haya yafuatayo kabla ya kukupa kauli yangu ya mwisho:

    1)Jee, mkutano ni wa ulamaa wa pande zote mbili, au ni baina yangu
    mimi tu na ulamaa wa Kisunni?

    2)Ikiwa ni wa ulamaa wa pande zote mbili, ni ulamaa walio humu humu
    nchini tu ama kuna mipango ya kuwaalika walio nje ya nchi pia?

    3)Ni nini hasa madhumuni ya mazungumzo yenyewe? Ni:

    a)kueleza msimamo wangu juu ya Ushia tu, au

    b)ni kujadiliana juu ya msimamo wangu na/au itikadi za Shia Ithnaashari?
    Au

    c)ni kuangalia jinsi ya kuleta uelewano na mkuruba baina ya Shia na
    Sunni?

    4)Ni jambo gani katika msimamo wangu kuhusu Shia Ithnaashari na/au
    itikadi za Shia Ithnaashari zenye mushkili, na mushkili wenyewe ni nini?

    5)Kanuni zitakazofuatwa katika mazungumzo/majadiliano;

    6)Watakaoshiriki, na idadi yao.
    Mwenyezi Mungu Ajaalie taufiki.
    Nduguyo,
    ABDILAHINASSIR

    n.k.

    Maimamu wa Misikiti (Mombasa).

    Mashekhe uliowataja katika barua yako ya 30.11.89

    49