ArticleIDPicAddressSubjectDate
{ArticleID}
{Header}
{Subject}

{Comment}

 {StringDate}
 
 
 
 
 
 
 
ViewArticlePage
 
 
 
  • Bismihi Ta'ala  
  • Sendtofriend
  •  
  •  
  • Mwenyezi munguanasema:(( Na tunataka kuwa neemeshawale ambao walifanywa kuwa wanyonge ardhini na kudhoofishwa, na kuwafanya kuwa viongozi na kuwafanya kuwa warithi)) wa ardhi hii.

    Tunatoa pongezi kwa waislaam wote ulimwenguni na wote wapenda hakina uadilifu kutokana na mazazi matukufu ya Imamul asri wazzamaanImam Mohammad binil Hassan al askari alie marufu kwa jinala Al- mahdy (a.s) na ambae kuzaliwa kwake ni ubashirio mwema kwa walimwengu, kwani yeye ndie mkombozi wa ulimwengu na walimwengu kutokana na dhuluma ya mustakbiriina na madhalimu, mazazi ambayo yalitokea tarehe13 mwezi wa shaaban mwaka 255 hijiria katika mji wa samarrah ulioko huko Iraq.na tunakutakieni furaha njema na maadhimisho mema katika mazazi haya matukufu.

    Bismihi Ta'ala

    WITO KWA WAISLAMU KUUENDEA UKWELI

    "Na katika haya imekujia HAKI na mauidha na ukumbusho

    kwa wale wanaoamini."(SuratulHud11:120)

    Makala No. 1

    ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

    MTUMEMOHAMMAD(S.A.W.W)ALIMTEUA

    IMAMALI (A.S.) KUWAKHALIFABAADA YAKE

    UTANGULIZI

    Tofautikubwailiyopo baina yaWaislamuwaKishiana Waislamu waKisunnini juuya imaniya UkhalifanaUimamubaada yakuondokakwaMtukufu MtumeMohammad(SA.W.W).Sisi waislamuwaKishiatunaaminikuwaImam AlibinAbi Talib (a.s)nikhalifana Imamwakwanzabaada yaMtume(S.A.W.W)ambapondugu zetuWaislamu wa KisunniwanaaminikwambaSeyidinaAbubakar ( r.a.) alikuwani khalifawa kwanza.

    IngawakunatofautinyinginendogondogozilizopobainayamadhehebumakubwayaKiislamu(Shiana Sunni)kwamfanokatikasheria(Fiqh)kamavilekukunjamikonowakatiwa kusaliaukuinyooshan.k.lakinihizini tofautindogo ndogosanaambazozinawezahatakupatikanandaniyamadhehebumanne yaKisunni (ImamShafi,Maliki,Hanafi naHanbali ).Masuala hayatutayajadili hapobaadayeInshaAllah.

    Mbalinatofautihiyokubwakunamamboyanayofananakatikaimani za WaislamuwaShiaIthna Ashariyana Waislamu wa Kisunni. Lakwanzani nguzo tano za Uislamu, yaani :

    (a)Shahada-Laa Ilaaha Illallah-MohammadurRasuulullah-Hakuna munguapasayekuabudiwa kwahakiisipokuwa Allah -na Mohammadni Mtumewamwisho wa Allah.

    (b)Sala tano za kila siku

    (c)Kufungamweziwa Ramadhan

    (d)Kuhiji katikanyumbatakatifuya Kaa'ba

    (e)Zakatkwaajili ya maskini.

    KwapamojaShia Ithna Asheriyyana Sunniwanaaminijuu ya kitabuchamwishocha Allah Qur'ankuwabado kipo vilevilebilamapunguzo au maongezo, na wanajaribu kufuata maamrisho yake bila kubakiza.

    KwapamojaShiaIthnaAsheriyanaSunniwanaichukuliaSunnahnaSiiraya Mtumekuwanimuongozo kwa Waislamukatikamaishayao ya kilasikunawanajaribukuifuatakwauangalifumkubwaili wapatekuokoka hapadunianinaAkhera.

    Ingawawapo watuwaharibifukatikajamiiambaokwamakosawanatushutumusisi ShiaIthnaAsheriyakwamadai mbalimbaliya uongokamavilekudaikuwaShiawana Qur'anyaoau madaikuwaeti Shiawanaamini juu ya Utume waImamAlibinAbitalib,n.k.Walewotewanaoutafutaukweli,wanatakiwa kuyatupiliambali madai(shutuma)hayamaovudhidi yetunatunawaombawatembelee misikiti namadrassahzetuambazomarazotezipowazikwaMwislamuyeyotekujakuthibitishaimani zetu.

    Kuna Shia zaidi yamillioni 250 dunianikoteambaowanaaminikuwa MtumeMohammad(s.a.w.w)ni Mtumewamwishonawanafuatamaamrishoya Qur'annaSunnaza Mtume(S.A.W.W)katikamaishayao ya kilasiku.KatikamanispaayaDodomapeke yake,sisiShiatunamisikiti miwili;Khoja ShiaMasjidnaMasjid ImamMahdi (A.S)na tunawaalika wauminiwotewaKiislamu kututembeleakatikamisikiti hiiili kupataushahidikwamachoyao kuhusiananaimaninamatendoyetukablayakuangukiakatikamtegowawaharibifuwanaotuzuliahabarizauongo.

    KWANINI SHIA WANAAMINI KUWAIMAMALI (A.S) NI

    KHALIFA WA KWANZA BAADA YA MTUME ?

    ShiaIthnaAshariyawanaaminikuwaImamAli binAbitalib ni Khalifana Imam wa kwanzabaada ya Mtume(S.A.W.W) kwakuzingatia sababumojarahisisanana iliyowazi.Sababuhii nikuwa;"ImamAlibinAbitalib(.A.S)aliteuliwakwaamri yaMwenyezi MungukuwaKhalifawakwanzawaWaislamu naMtumemwenyewekwaamri yaMwenyeziMungu(s.wt).Hiindiosababunahakunasababunyingine.

    Katika Qur'antukufu (59: 7)MwenyeziMunguanasema: "-----NaanachokupeniMtumebasipokeeninaanachokukatazenijiepusheninacho".

    Qur'an (33:36): "Nahaiwi kwamwanamunealiyeamini wala kwamwanamkealiyeamini,MwenyeziMunguna Mtumewakewanapokatashauri,wawenahiarikatikashaurilao.Namwenyekumuasi Mwenyezi Munguna Mtumewake,hakikaamepoteaupotevuuliowazi"'.

    Shia wanaaminikwambamaadamuMtume (S.A.W.W)mwenyewekwaamriya Mwenyezi MungualimteuaImam Ali (a.s) kuwaKhalifa, Waislamuhawanahiariyoyoteisipokuwakutii amri hii.

    MITUME NAMAIMAMU HUTEULIWANA

    MWENYEZI MUNGU TU NA SI VINGINEVYO

    Shiawanaamini kuwaniMwenyeziMungu (Allah)tundiyeanayewezakumteuamrithiwa Mtumena Imam waWaislamu,nakwambaUmmahwa Kiislamuhaunahiariyoyotekatikajambo hili.

    USHAHIDI KUTOKAKATIKAQUR'AN

    AyazaQur'anzifuatazozinathibitishakuwaMitumewotenaMaimamu waliteuliwana AllahMwenyewe.

    1)"Na Molawakohuumbaatakavyonahuchagua;Hawanahiari yakuchagua" (Qasas 28:68)

    2)"Mimi nitaletakhalifakatikaardhi".(Baqara 3:30)

    3)"EweDaud!Hakikatumekujaalia kuwakhalifakatikaardhi---- ". (Saad38 :26)

    4)"(Allah)alisemakwahakikanitakufanyawewe(Ibrahimu)kuwaImamwawatu (Ibrahimu); alisema Je na katika kizazi changu pia? Akasema (Ndio lakini) ahadiyangu haitawafikia waovu (madhalimu)". (Baqara2:124)

    5)"NatukawajaaliakuwaMaimamuwanaoongoza kwa amri Yetu".(Anbiya 21:73)

    6)"Na Unifanyie Waziri(msaidizi) katika jamaa zangu ........... ndugu yangu Haruni .......... Mwenyezi Mungu Akasema: Hakika umepewa maombi yako, ewe Musa". (Taha20: 29 - 36)

    7)"NahakikaMwenyezi Mungu alimchagua Adamu na Nuhu na kizazi cha Ibrahimu na kizazicha Imranijuu ya walimwengu wote.Nikizazi cha wao kwa wao; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenyekujua". (Al- Imran3:33 - 34).

    8)"MwenyeziMunguamemchagua (Taluti) juu yenu na amemzidishia wasaa wa elimu na kiwiliwili, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua". (Baqara2:247)

    9)"Akasema (Allah) : Ewe Musa! Miminimekuchagua juu yawatu wote kwa ujumbe wangu na kwa kusema nawe kwangu, basi pokea haya niliyokupa na uwe miongoni mwa wanao shukuru".(A'raaf 7:144)

    10)"Natukawafanyamiongonimwao Maimamuwanaoongozakwaamri yetu, waliposubiri na walikuwa wakiyakinishaaya zetu". (Sajdah32: 24).

    Ayazote zaQur'anzilizotajwahapojuu nanyinginenyingiambazohatukuzitaja zinathibitishakwambaMitume wotena warithi waowaliteuliwamojakwamojana MwenyeziMungubilahiari yaUmmah.

    USHAHIDI/UTHIBITISHO WAKIAKILI NAKIHISTORIA

    1)ADAYA MITUMEWALIOTANGULIA: Ada ya Mitume wote ilikuwanikuteuawarithi wao kwaamri ya Allahbila kuingiliwanaUmmah. Historiaya MitumehawahaitoimfanohatammojawamrithiwaMitumealiyechaguliwa kwakurazawafuasiwake. Hakunasababukwa ninilinapokujasualala mrithiwa Mtumewa Mwisho, Mohammad(s.a.w.w)sheriana kanunihii yaMwenyeziMunguibadilishwe.

    Mwenyezi Munguanasema: "Walahutapata mabadiliko katikakawaida ya Mwenyezi Mungu(Mwendo Wake na sunna yake)".(Ahzab33: 62)

    2)MIFANO YAWARITHIWAMITUMEWALIOPITA: Baadhiyamifano ya warithiwa mitumewalioteuliwa na Mitumewaliopita kwaamri ya MwenyeziMungu (s.w).

    a)NabiiAdamualimteuaShiith

    b)NabiiIbrahimalimteuaIsmail

    c)Nabii Ya'qubalimteuaYusuf

    d)NabiiMusaalimteuaYusho'binNuun

    e)NabiiIssaalimteuaSham'uun

    f)NabiiMohammad ( S.A.W.W)alimteuaImamAliIbnAbiTalib

    Qur'aninasema:"NawakumbukewajawetuIbrahimnaIs-haqnaYaqkubwaliokuwa wenye nguvu na busara. Hakika sisituliwachaguakwa lile jambo zurikabisala kuikumbukaAkhera. Na bilashaka walikuwambeleyetunimiongoni wa watu bora waliochaguliwa. Namkumbuke Ismaili na Alyasaa na Dhulkifli; na hao wote walikwa miongoni mwa watu bora".(Saad 38:45 - 48).

    Qur'an inasema:"Na hizindizohojazetu tulizompa Ibrahim juu ya watu wake. Tunamnyanyuakatika vyeo yule tumtakaye. Hakika mola wakondiye Mwenye hikima nandiye ajuaye, Natukampa (Ibrahim) Is-haq na Ya'quub, wote tukawaongoa. NaNuhu tulimwongoa zamani. Na katika kizazi chake Daudi na Suleimani na Ayyub na YusufnaMusa na Haruni. Na hivi ndivyo tuwalipavyo wafanyao mema. NatukamwongozaZakariana Yahyana Issa na Ilyasi wote (walikuwa) miongoni mwa watu wema. Na (tukamwongoza) Ismail na Al-Yasaa (Ilisha) na YunusinaLuti. Na wotetukawafadhilisha juuya walimwengu. Na (tukawaongoa) baadhi ya baba zao na vizazi vyaonandugu zao. Na tukawachaguana kuwaongozakatika njiailiyonyooka. Huu ni uongozi wa Mwenyezi Mungu. Kwa huo humwongoza amtakaye katika watu wake". (An-aam6:83 - 88).

    3)MTUMEHAKUFARIKI KABLA YA KUMTEUA MRITHI WAKE (WASII WAKE):

    4)

    5)Mitumewotewaliopitapamojana MtumeMohammad (s.a.w.w)hawakupata kuziacha Ummah zao japo kwa muda mfupibilakuachawatuwatakaoshikamahala pao (warithi). Hatawalipokuwawanatoka kwasafarifupiwalikuwawanaachawatu wakushikamahala pao (warithi). JeinawezekanakwaMtumeMuhammad (s.a.w.w)kuondokanakuuacha Ummah wake bila Wasiy(Mrithi).

    MtumeMuhammad alikuwaanajuakuwamudawakewa kuondoka duniani umekaribia, alijuakuwepokwawanafikikatika jamii ya waislam, alijua kuwepo kwa watu walioendekezatamaa yamadaraka katika mioyo yao, hivyo asingewezakuuacha Ummah wake bila wasii(mtu atakayeshika mahala pake). Alimteua ImamAli bin Abitalib kwaamri yaMwenyeziMungukuwamrithinamtuatakayeshikamahalapake baada yakuondokakwakehapaDuniani.

    4)SababuzinazofanyaulazimawaMitumekuteuliwa na Mwenyezi Munguni hizohizo zinazofanya ulazimawaWasii, ImamunaKhalifakuteuliwana Mwenyezi Mungu kwasababuwotewanateuliwakufanyakaziza Allah.

    5)IkiwaImam auKhalifa atateuliwaaukuchaguliwana watu, utii wakewa kwanzahautakuwa kwa Mwenyezi Mungubalikwawatu waliomchagua. Kwasababumsingi wamamlakayake itakuwani watu,marazoteatajaribukuwaridhishawatu,vinginevyoikiwawatapotezaimani juuyake,atapotezanafasiyake.Mtuwa ainahiihatawezakutekelezamajukumuyadini bilawogaauupendeleo, namachoyakedaimayatakuwakatikamtazamowakisiasa.

    6)HistoriayaUislamuina mifano tele ya maovuyaliyofanywanamakhalifawalioteuliwana wanadamu.Mfanobora kabisaniulewa YazidbinMuawiya binAbuSufiyanambayewaziwazikabisaalizipuuzasheria,alikunywapombekweupe,alimuuamjukuuwa MtumeImam Husayn (a.s)na alituma jeshiMakka ambalo liliichomanyumbatukufuya Al- ka'abanakufanyamaovumenginemengi. (TazamaTaarikhul Khulafaa cha Suyuti).

    7)Piani MwenyeziMungutundiyeanayejuahisianamawazoya ndaniyawanaadamu, hakuna mwingineanayeweza kujuaundani wa mtumwingine.Wakati fulani anawezakujifanyani mchaMunguna mwenyekumuogopaMwenyeziMunguili tukuwaonyeshawenzakeau ili apateumaarufuili achaguliwena wenzake kuwakiongozikwamanufaayakiulimwengu.

    Mifano ya aina hii si habakatikahistoria.TuchukuemfanowaKhalifaAbdulMalikbin Marwanambayealikuwaanamalizasikunzimamsikitiniakisalina kusomaQur'an. Sikumoja aliarifiwa juu yakifochababayakena kwambawatuwalikuwawanamsubiriili watoekiapocha utii kwake.AliifunikaQur'anna kusema :"Hukundio kuachanakwangumimi nawewe (Qur'an)".(YaanikupataUkhalifandio mwishowa kusomaQur'an). (TazamaTaarikhulKhulafaa yaSuyuti, Ukurasa217). Sifamuhimuza Imam , niMwenyezi Mungutu ndiyeanayezijua.

    8)MAASUM -KwamujibuwaShia,MaimamunaMakhalifalazimawawe Maasum-yaani waliotakasikakutokanana madhambina uchafu. HivyoMaimamuwote12 walioteuliwana MtumeMohammad(S.A.W.W) walikuwaMaasum (wasio na madhambi), nahistoria yaUislamu inashuhudiaumaasumu,uchaMungu, elimuna tabianjemazaMaimamu12waShia IthnaAshariyah, wakwanzawao akiwaImam Ali bin Abitalib (a.s.).Madahiiitajadili zaidi katikamakalayajayo.

    Ismah(kutakasika kutokananamadhambi )nisifakutokakwa Munguambayohaiwezikupatikana kwajitihadaya mtutu bilaridhaa ya Allah,hivyo Maimamuwanatakiwa wateuliwena Allah tu.Sababuzote zinazothibitishakuwaMitume lazimawaweMaasum piahizo hizozinathibitishakuwaMaimamuniMaasum.Maelezozaidi yatafuatia.

    9)MIUJIZA-Kwamujibuwa Shia, Maimamuwalioteuliwana Allah lazimawawenauwezo kutokakwa Allahwakuonyesha miujizakilaitakapohitajika ili kuthibishaUimamuwao kamawalivyokuwa wakifanya Mitume. Historia ya UislamuinathibitishatenakuwaMaimamu12walioteuliwana Allahwalionyeshamiujizanawaliwashindamaaduizaokatika swalalaukweli (haki). Makhalifawalioteuliwana watu huwahawanauwezowakuonyeshamiujiza, jamboambaloni muhimusana kwaMitumenaMaimamu.

    10) UBORA-Shiawanaamini kuwa,kamailivyokwa Mtume,Imamulazimaawazidiwale wote anaowaongozakatika sifa borakamavile elimu,Ushujaa, Ujasiri,Ucha Mungu,naUkarimu. Lazima awena elimukamiliya sheriaza MwenyeziMungu. Hapapia,sifahizi hazipatikanikwaKhalifa yeyotealiyechaguliwaaukuteuliwanawatu isipokuwa kwaMaimamu12 wa Shia Ithna Ashariya walioteuliwana Allah. Somamakalayatakayofuatakwa maelezo zaidi.

    Pointi zotehizizinathibitishawaziwazikuwawarithi,Makhalifana MaimamuwaMitume wotelazimawateuliwe na Allahtu. Maovu yote,kutokuwepokwaUmoja,Ujinga , Uvunjaji wa sheria za kiislamu n.k. yote hayayanatokananamakhalifawaliochaguliwana watuwaliopingaamriya AllahkupitiakwaMitume wakekuhusianana suala laukhalifa.

    Ili kupatauokovu, ukwelinautukufuwaislamuwanatakiwawarudina kufuataamri ya Allah (swt)kuhusiana na sualala Imambaada yaMtume,tunawaitakatikaukwelinahaki. Lakinini lini MtumeMohammad(S.A.W.W)alimteuaImamAli bin Abi Talib (a.s) kuwa KhalifanaImam? Jekunaushahidi wowote katika Qur'antukufu,Sunnahna historia ya Uislamu unaothibitisha uteuzi huu?

    Ili kupatamajibu ya maswali hayasoma makala Na. 2.

    SheikhMuslimBhanji

    TANZANIA ITHNA ASHARIYAH COMMUNITY (T.I.C.)

    Dodoma.

    June2001