ArticleIDPicAddressSubjectDate
{ArticleID}
{Header}
{Subject}

{Comment}

 {StringDate}
 
 
 
 
 
 
 
ViewArticlePage
 
 
 
  • UTETEZI WA SHERIA ZA KIISLAMU SEHEMU YA PILI  
  • Sendtofriend
  •  
  •  
  • (2)

    MUHTASARI JUU YA SHERIA ZA MIRATHI:*

    ANGALIA: Tuna furaha kufunga pamoja na huu muhtasari uliowasilishwa kwenye tume juu ya sheria ya mirathi iliyoteuliwa hivi karibuni na Serikali ya Kenya. Masharti ya rejea yakiwa, kufirikiria sheria zilizopo sasa zinazohusu ndoa, talaka na mambo yanayohusika pamoja na hayo na kupendekeza Sheria inayofanana ya kutumika kwa watu wote wa Kenya ikitoa kipaumbela kwenye hadhi ya wanawake kuhusiana na ndoa na talaka katika jamii huru ya kidemokrasia.

    Sekritariati hii ina wiwa na Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi mwanachuo mkazi wa Dar es Salaam, Muasisi na Mhubiri Mkuu, wa Bilal Muslim Mission of Tanzania kwa juhudi zake kubwa katika kuandaa muhtasari huu. Vile vile tuna viwa na Mulla Hussein A. Rahim M. B. E. wa Zanzibar, kwa muongozo wake wenye thamani.

    Tunaomba Allah ( S.A.W.) kwamba awalipe kwa wingi hapa duniani na kesho akhera.

    ASGHARALI M. M. JAFFAR, Mh. Katibu Mkuu, Halmashauri Kuu K. S. Ithna-Asheri P. O. Box 1085, MOMBASA

    *****

    1. Kwa niaba ya Jumuiya ya Shia Ithna-Asheri ya Kenya tunaomba ruhusa ya kutoa uwasilishaji huu kw aajili ya kufikiriwa na Tume.

    2. Maelezo yetu yanakomea kwenye Sheria za dini zinazohusika na wosia na Mirathi kwa mujibu wa madhehebu ya ki-Islamu ya Shia Ithna-Asheri, isipokuwa ambako palipokuwa na maana kutoa maoni ya madhehebu nyingine ili kuifanya nukta yetu kuwa wazi.

    3. Tayari tumewasilisha maswali yaliyotumwa na Tume yakiwa yamekamilishwa ipasavyo pamoja na mpangilio wa sheria za ki-Islamu (kwa Kiingerza) kwa mujibu wa Sheria ya Madhehebu ya ki-Islamu ya Shia Ithna-Asheri ihusianayo na Mirathi na Wosia miongoni mwa mambo mengine. Katika wasilisho hili tutajitahidi kueleza kanuni za msingi chini ya hukumu hizo.

    4. Tunaelewa kwamba tume hii itatoa kipaumbele kwenye hadhi ya wanawake. Tunajasiri kutumaini kwamba Sheria ya ki-Islamu inayotajwa kwa mujibu wa madhehebu ya Shia, itakuwa ya msaada mkubwa kwa Tume katika kazi yake juu ya suala hili.

    Haitakuwa nje ya sehemu (ya maudhui) kutaja kwamba mila ya ki-Arabu ya zamani ilikuwa na lengo moja la msingi katika mtizamo, yaani, uzuiaji wa kudumu wa mali katika familia. Pamoja na lengo hili katika mtizamo, urithi ulikomea kwa ndugu wa kiume pekee tu, na hata miongoni mwao ni kwa wale tu ambao walikuwa na uwezo wa kubeba silaha.

    Hatukusudii kushughulika sana juu ya nukta hii; itoshe tu kusema kwamba tabia kama hii, zaidi au kidogo ilikuwepo katika jamii zote katika wakati huo na imebakia katika jamii nyingi mpaka sasa. Uislamu ulitoa kwa kudhihirisha uwekaji wa sheria ya haki ya kurithi kwa wale ambao walienguliwa na taasisi za zamani. Moja ya matokeo ya faida ya sheria mpya ya Mungu ilikuwa kunyanyua hadhi ya wanawake katika mizani ya ustaarabu, kwa kunyanyua uchumi wao na nafasi ya kijamii, na kuwapa wajane, mama, mabinti na dada na ndugu wengine wa kike haki ya kurithi.

    5. Moyo huu umehifadhiwa katika Sheria ya madhehebu ya Shia ambayo, kwa kunukuu maneno ya mwanachuoni mkubwa Sayyed Amir Ali, “Ni ya wepesi mkubwa mno na haihusishi mjadala wowote kuhusiana na haki za ndugu wa kiume na wa kike - “Asabah na Zav-il-Arham”. Kisha aliendelea kusema kwamba “Tofauti kubwa, kusema kweli, kati ya Shia na Sheria ya mirathi ya Sunni iko katika suala la jinsia ya Kuumeni. Shia wanakataa kwa kupinga itikadi ya Taasib au jinsia ya Kuumeni; hatimaye uhusiano wa Kuumeni wa jinsia ya kiume, au inayoitwa “Asbah Sahihi” katika fikihi ya Sunni (Sheria ya Sunni), hawana upendeleo maalum wala hawafadilishwi kwenye kuunganisha mahusiano na marehemu kupitia wanawake. Kwa mfano, Shia wanaona ni kinyume cha uadilifu kuwatoa watoto wa binti kwa kupendela kizazi cha mbali cha kaka, kwa msingi wa kubunia kwa kuwa kwao kuungana na marehemu kupitia mahusiano ya kuumeni. (Mohameden Law, by Ameer Ali Vo. 2; P. 128).

    Kwa mfano:

    (a) Kama Muislamu Sunni akifa akiacha nyuma yake binti wa binti yake pamoja na mtoto wa kiume wa kaka yake, mtoto wa kiume wa kaka yake atachukuwa urithi wote kama ASABAH (ndugu wa kuumeni wa jinsia ya kiume). Kwakumuondoa mjukuu mwenyewe wa marehemu. Chini ya Sheria ya Shia Inthna-Asheri, mjukuu wa kike (anayezaliwa na binti yake) wa marehemu, kama mtoto kwa nasaba, huchukuwa mali yote kwa kumuondoa mtoto wa kiume wa kaka yake.

    (b) Kama Muislamu Sunni akifa, akiacha nyuma binti na kaka, binti huchukuwa mgao ulioainishwa, yaani moja kwa mbili za mwanaume na inayobakia huenda kwa kaka kama Asabah. Chini ya Sheria ya Shia Ithna-Asheri, huchukuwa mali yote, nusu kama kiainisho cha mgao wake, na nusu nyingine kwa itikadi ya kurudisha.

    6. Kanuni zinazoongoza zinaweza kuelezwa kwa ufupi katika maneno yafuatayo:-

    (a) Mrithi mwenye uhusiano wa karibu na marehemu hurithi kwa kumfadhilisha zaidi kuliko yule mwenye kufungamana naye kwa mbali;

    (b) Yeyote yule anayehusiana na marehemu kupitia mtu yeyote harithi wakati mtu yule anaishi;

    (c) Kaka na dada wa kuzaliwa mama mmoja, baba mmoja wanapendelewa kuliko kaka na dada wa kinasaba; lakini kaka na dada wa tumbo mmoja watarithi pamoja nao.

    (d) Wakati uhusiano ni sawa, mwanamume kwa kawaida hupata marudufu ya mgao wa mwanamke, isipokuwa katika hali ya warithi wanaohusiana kwa mama ambao kwa ujumla hugawanya urithi miongoni mwao kwa sawa sawa bila tofauti ya jinsia.

    Inaweza ikaulizwa kwa nini mgao wa mwanamke, kwa kawaida ni nusu ya ule wa mwanaume? Kusema kweli, ni yenye mantiki kabisa. Uislamu umemfanya mwanaume kuwajibika kwa ajili ya matunzo ya familia. Hakuna mzigo kama huo uliowekwa juu ya mwanamke. Hata mke tajiri anapasika kupata matunzo yake kutoka kwa mume wake ingawa anaweza akawa masikini. Kwa vile anatakiwa kubeba gharama zote, amepewa mgao marudufu karibu katika kila mirthi. Vile vile mwanamke hupata mahari ambayo hutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke. Hivyo uwiyano wa migao uliowekwa na Qur’an Tukufu ni wa haki zaidi.

    7. MAKUNDI NA TABAKA ZA WARITHI:

    Katika Shriat za Shia Ithna-Ahsri, warithi wamegawanywa katika makundi mawili, yaani, wale ambao hurithi kwa haki ya “Nasab” (nasaba); na wale ambao wanarithi kwa haki ya ‘Sabab’ ambao kwamba muhimu ni wa ndoa (kuoana). Makundi yote hurithi kwa pamoja.

    Kundi la kwanza yaani mahusiano ambayo yanapasika kurithi kwa sababu ya unasaba limegawanyika katika tabaka tatu:-

    (a) Tabaka la Kwanza: (i) Wazazi na (ii) Watoto (au katika kukosekana kwao, wajukuu-wowote kwenda chini-yaani: kilembwe, kitukuu na kuendelea).

      1. Tabaka la Pili:

    Kama hakuna mrithi kabisa katika tabaka la kwanza, basi wazazi na dhuria wa wazazi wa marehemu watarithi: Ina maana:

    (i) Babu zake marehemu (wowote kwenda juu). (ii) Kaka na Dada (au katika kukosekana kwao-dhuria wa kaka na dada).

    (c) Tabaka la Tatu:

    Kama hakuna mrithi aliyepo si katika tabaka la kwanza au la pili, basi dhuria wa mababu (wowote kwenda juu) watarithi. Ina maana: ndugu wa upande wa kiume na upande wa kike wa marehemu, ami, wajomba na shangazi wa marehemu (au katika kukosekana kwao, basi watoto wao kwenda chini).

    Kama ilivyoelezwa hapo juu mume au mke au wakeze marehemu watarithi pamoja na tabaka zote hizi.

    8. Dhul – Fardh na Dhul Qarabat:

    Ni muhimu kutaja kwamba, chini ya sheria ya Shia, warithi katika kundi au tabaka lolote watakalokuwa wamegawanywa katika mafungu matatu, kuhusiana na haki ambayo wanapasika wao kushiriki katika mirathi:-

    (1) DHUL-FARDH: wale ambao wana haki kwenye mgao ulioainishwa katika mirathi ni hawa:

    (a) Mama (b) Mume (c) Mjane au Wajane (d) Mtu au watu wanaohusiana kwa mama yuleyule tu.

    (2) DHUL-QARABAT: Wale ambao huchukuwa urithi kwa sababu ya uhusiano wao na marehemu, lakini ambao mgao wao hushuka na kupanda kwa kutegemea idadi ya warithi na mazingira. Hawa ni:-

    (a) Mtoto au watoto wa kiume

    (b) Kaka kamili au katika kutokuwepo kwao ndugu kwa upande wa baba (mama mbali mbali) (c) Mababu (d) Ami na Shangazi (e) Wajomba na mama wadogo.

    (3) DHUL – FARDH WAL-QARABAT; Hawa ni warithi ambao wakati mwingine hurithi kwa sababu ya uhusiano wao na wakati mwingine hutegemea migao yao iliyopangwa; hawa ni:

    (a) Baba ambaye hurithi mgao uliopangwa kama kuna mtoto wa marehemu; na huchukuwa kwa uhusiano kama hakuna mtoto wa marehemu.

    (b) Binti au Mabinti ambao hupata mgao wao uliopangwa bila kuwepo baba wa marehemu au kaka yake au kaka zao wenyewe; na wanachukua kwa ushusiano wakati wakiwa pamoja na yeyote kati yao.

    (c) Dada kamili au dadaze au katika kutokuwepo kwao, dada wa nasaba au dadaze, ambao hupata mgao uliopangwa wakati bila kuwepo babu au kaka, kakaze wa daraja moja kama wao wenyewe, na huchukuwa kwa uhusiano wakati wakiwa pamoja na yeyote kati yao.

    Angalia : Wakati kukiwa na mrithi mmoja tu, imma Dhul-Fardh au Dhul-Qarabat, au mwenye kupasika kwa sababu ya uhusiano maalum wa Sabab (kuoana-ndoa), mrithi kama huyo huchukuwa mirathi yote. Kwa mfano, binti pekee huchukua mgao wake uliopangwa, yaani, nusu moja na iliyobakia huenda kwake kwa kurudisha. Mtoto wa kiume pekee huchukua mali yote kwa haki ya Qarabat, hakuna mgao ulioainishwa uliowekwa kwake kwa Sheria. Wakati marehemu ni mwanamke na hakuacha nyuma yake jamaa anayehusiana na yeye isipokuwa mume, ambaye anahusika na kurithi kwa sababau ya ndoa, anachukuwa urithi wote kwanza kama mgao wake ulioainishwa, na uliobakia kwa kurudisha.

    9. MIGAO: Kwa kadiri migao inavyohusika iko sita kwa idadi, yaani:-

      1. Nusu moja (2) Moja ya nne (3) Moja ya Nane

    (4) Moja ya tatu (5) Mbili ya tatu (6) Moja ya sita.

      1. NUSU MOJA : Wafuatao wanapasika kwenye nusu moja ya urithi:
        1. Mume wakati mke hakuacha mtoto;
        2. Binti wakati hakuna mtoto wa kiume;
        3. Dada kamili kwa kukosekana warithi wengine ambao wametajwa mapema;
        4. Dada wa nasaba wakati hakuna kaka na dada kamili.
      2. MOJA YA NNE : Wafuatao wanahusika kwenye moja ya nne:
        1. Mume, wakati kuna nasaba ya dhuria ya mke;
        2. Mke, wakati hakuna nasaba ya dhuria ya mume;
      3. MOJA YA NANE : Hii huchukuliwa na mjane au wajane wakati kuna nasaba ya dhuria ya mume.
      4. MOJA YA TATU : Wafuatato wanapasika kwenye moja ya tatu:-
        1. Mama, wakati hakuna nasaba ya dhuria ya marehemu, wala hakuacha kaka wawili, au dada wanne au kaka mmoja na dada wawili.
        2. Kaka na dada tumbo moja, wakati wakiwa wawili au zaidi katika idadi.
      5. MBILI YA TATU : Wafuatao wanapasika kwenye mbili ya tatu:
        1. Mabinti wawili au zaidi, wakati hakuna mtoto wa kiume;
        2. Dada kamili wawili au zaidi wakati hakuna kaka kamili au hakuna kakaze (baba mmoja mama mabali mbali).

    (6) MOJA YA SITA : Moja ya Sita inachukuliwa na wafuatao:

      1. Wote baba na mama wakati marehemu ameacha nasaba ya dhuria.
      2. Mama, wakati wanakuwepo pamoja naye kaka wawili au zaidi wa damu kamili au kaka mmoja na dada wawili au dada wanne wa damu kamili (au kwa baba yule tu, baba yule akiwa yupo).
      3. Kaka mmoja au dada wa tumbo moja.

    10. MGAWANYO WA MALI: Wakati kuna mmoja tu wa warithi waliotajwa hapo juu akiwa mwanaume au mwanamke hupata mali yote. Kama ni Dhul-Qarabat, huipata kwa sababu ya uhusiano; kama ni Dhul-Fardh, kwanza anapata mgao wake uliopangwa, na kisha mabaki anapewa yeye kama kurudisha (Radd).

    Kama wako warithi wawili au zaidi, itagawanywa katika utaratibu ufuatao: Kwanza mume; au mke au wake watachukuwa mgao wao; kisha ndugu Dhul – Fardh watapata mgao wao; kisha mabaki yatagawanywa miongoni mwa warithi Dhul-Qarabat.

    Mfano: Kutoa mfano wa utaratibu wetu, ngoja nichukulie kwamba mtu anakufa anamuacha baba yake, mama, mke, watoto wanne wa kiume, mabinti watano, wajukuu watatu, babu, kaka watatu na shangazi wawili.

    Kwa vile ameacha wazazi na watoto wakiume na mabinti, ambao wanahusika na tabaka la kwanza la warithi, babu na kaka (ambaowanahusika na tabaka la pili) na mashangazi (ambao wanahusika na tabaka la tatu) wataondolewa kwenye urithi.

    Hali kadhalika, wajukuu wataondolewa kwa sababu ya kuwepo watoto, juu ya msingi wa karibu kuwaondoa wa mbali zaidi.

    Mfumo huu wa kuondoa hutuacha na warithi wafuatao: mke, Baba, Mama, Watoto wanne wa kiume na mabinti watano.

    Mke atapata 1/8 ya mali kwa sababu marehemu ameacha watoto; Baba na Mama wote watapata kila mmoja, moja ya sita 1/6.

    Kigawanyo cha kawaida cha 8 na 6 itakuwa 24. Hivyo mali itagawanywa katika migao 24 – ambapo kutoka hiyo mke atapata 3 (yaani 1/8), baba 4 (yaani 1/6) na mama vile vile 4 (yaani 1/6). Itaonekana kuwa baba ameshughulikiwa hapa kama Dhul – Fardhi, sio kama dhul – Qarabat, kwa sababu ya watoto wa marehemu, na mama kupata mgao pungufu (yaani 1/6 badala ya 1/3) kwa sababu ya mantiki hiyo hiyo.

    Vyovyote vile, baada ya kupunguza 3 + 4 + 4 (yaani 11/24) tumebakiwa na migao 13. Hii itagawanywa miongoni mwa watoto, mtoto wa kiume akipata marudufu ya mgao wa binti. Ina maana kwamba – kila mmoja wa watoto wanne wa kiume atachukuwa migao miwili (kufanya 8) na kila mmoja wa mabinti atapata mgao mmoja (kufanya 5). Hivyo migao yote imekwisha.

    11. DHUL-FARDH LAZIMA WAPATE MGAO WAO ULIOPANGWA: Katika mfano wa hapo juu, migao imelingana na mahitaji ya manfungu ya mirathi. Lakini kuna weza kuwa na hali wakati migao iliyopangwa yaweza kuzidi kigawanyo cha kawaida cha migao. Kwa mfano, kama mwanamke ataacha mume nyuma yake mabinti wawili na mama, migao yao kwa kuhusiana itakuwa moja ya nne, mbili ya tatu na moja ya sita. Kigawanyo cha kawaida 3, 4, na 6 ni 12, ambacho huwakilisha migao ambayo kwayo mali itagawanywa – 3 ikiwa mgao wa mume, 8 wa mabinti na 2 wa mama. Lakini 3 + 8 + 2 hufanya 13, sio 12.

    Masunni hugawa mali kwenye migao 13, na kuleta upungufu kwa wote. Lakini miongoni mwa Shia, Mama na mume, wao wakiwa ni dhul-Fardh, lazima wapate mgao wao kamili, yaani 3 + 2. Na mabaki yaani 7/12 yatagawanywa sawa sawa miongoni mwa mabinti, kwa sababu watoto vile vile ni miongoni mwa Dhul-Qarabat.

    Hivyo wakati wowote kunapokuwa na upungufu katika migao iliyopangwa, huangukia juu ya Dhul – Qarabat, ambao migao yao hupasika na kupanda na kushuka, sio juu ya Dhul- Fardh.

    12. IMAM : Mrithi wa Marehemu asiye na mrithi:

    Kama hakuna mrithi katika tabaka yoyote na makundi yaliyotajwa hapo juu, Imam atakuwa mrithi wake. Kwa vile Imamu wetu yuko kwenye ghaibu kwa wakati huu, Mujtahid atapokea mali ile kwa niaba ya Imamu na ataitumia katika utangazaji wa imani na unyanyuaji wa dini ya Jumuiya ya Shia kwa kupendelea zaidi katika eneo lile lile alilokuwa akiishi marehemu.

    Mtu ambaye hana mrithi isipokuwa Imamu, ameruhusiwa katika Sheria ya Shia kutoa kwa wosia mali yake yote ili mradi utoaji huo ni kwa ajili ya faida ya Shia Ithna-asheri masikini, Ithna - asheri mayatima au Ithna-Asheri wasafiri mafukara tu.

    13. KUONDOA KUTOKA MIRATHI :

    Hakuna mwandishi wa wosia mwenye haki yoyote ya kumzuiya yeyote katika warithi wake kutokana na haki yake ya mgao wa mirathi. Hata kama anafanya wosia kuhusu suala hili, utakuwa umetenguka na batili katika sheria. Lakini mrithi atazuiwa kutoka kwenye mirathi kama akitokea kuwa sio Mwislamu au kwa makusudi na kwa dhulma amemuua marehemu ambaye kwamba mali yake angerithi.

    14. HATI ZA WOSIA :

    Ufanyaji wa wosia unatambuliwa na kuhimizwa na Sheria ya Ki-Islamu. Wosia unaweza ukawa wa mdomo au katika maandishi. Mwandishi wa Wosia ameruhusiwa kurithisha mpaka theluthi moja ya mali yake halisi. Kurithisha kokote kunakozidi theluthi moja ni batili, vinginevyo mpaka ikubaliwe na warithi. Mpangilio ya hukumu juu ya suala hili unatolewa katika kitabu kilicho andamana “ISALAMIC LAW-Sheria za Ki-Islamu” na sio muhimu kueleza kwa kinaganaga hapa.

    15. ULIPAJI WA MADENI NA GHARAMA KUTOKA KWENYE MALI: Inaweza kuonyeshwa hapa kwamba katika hali zote, madeni ya halali yampasayo marehemu pamoja na gharama fulani fulani lazima yapewe umuhimu wa kwanza katika ulipaji wa urithi na migao ya warithi.

    Neno “Deni”, Maana yake madeni ya kawaida ailiyoyaingia mwenyewe au kwa niaba ya marehemu na hujumuisha vile vile madeni ya kidini kama Zakat (kodi ya maskini) Khumus (hutolewa moja ya tano) Kaffara (malipo ya kosa au fidia), Nazar (nadhiri) nk., na neno “gharama” hujumuisha wajibu wa kupeleka wakili kwa gharama za mali ya marehemu, kutekeleza Hija Makka kama ilikuwa wajibu juu ya marehemu na haikutekelezwa na yeye wakati wa uhai wake. Gharama za mazishi vile vile zinatakiwa kupewa umuhimu wakulipwa.

    Baada ya kulipa madeni yaliyotajwa na gharama na urithi ulioelekezwa na wosia wa marehemu kufikia mwisho wa theluthi moja ya mali halisi, mabaki yatagawanywa miongoni mwa warithi.

    16. Katika kuhitimisha, tungependa kurudia tuliyoyasema mapema mbele ya Tume juu ya Sheria ya mambo ya Ndoa. Tunahisi kwamba wazo la kutunga Sheria ya wote kuchukua mahali pa Sheria ya ki-Islamu iliyopo sasa sio makosa tu bali ni kufuru kwa mtizamo wetu wa kidini. Itakuwa ni sawa sawa na kuweka dini inayofanana juu ya wote ambapo litakuwa ni wazo lisilo na maana. Sheria za ki – Islamu ni sehemu ya dini yetu. Sheria hizi haziwezi kubadilishwa au kuvunjwa bila kupata hisia ya hatia na dhambi.

    17. Hukumu zinazohusu mirathi zimewekwa kwa usahihi wa juu mno na Qur’an Tukufu na zinaelezewa kiukamilifu kwa uwazi katika Hadithi za Mtukufu Mtume na Maimamu kumi na mbili na hakuna shaka hata kidogo kwamba hukumu hizi ni kwa mujibu wa kanuni pana ya undugu wa mtu ambao Uislamu unataka kuanzisha.

    18. Sheria ya ki-Islamu ya madhehebu ya Shia Ithna-Asheri ni kitu kilichofumwa vizuri. Hatuwezi kubadilisha au kurekebisha moja au mambo yake mawili bila kuharibu ufumaji mzima. Kwa mfano, katika Sheria ya Ki-Islamu mtu hawezi kutumia kitu chochote kilichopatikana kiharamu (katika maana ya kidini) amma kwa kidunia au kwa madhumuni ya kidini. Kama kwa mfano mabadiliko yanafanywa katika sheria ya mirathi, mtu fulani kwa maana hiyo kikawaida atapata zaidi kuliko haki ya mgao aliogawiwa na Qur’an Tukufu na pato hili la haramu litafanya maisha yake yote kuwa duni. Maisha yake ya kila siku yatakuwa ni orodha ndefu ya kuchupa mipaka; Sala zake, Hija yake, hata chakula chake na mavazi vitakuwa haramu, katika maana ya dini. Hivyo hawezi kutegemea amani katika maisha ya kesho akhera.

    3

    MUHTASARI JUU YA WARAKA WA TANZANIA JUU YA SHERIA YA NDOA INAYOFANANA (SAWA) KWA WOTE*

    ANGALIA: Muhtasari huu kwa kutoepukika imeunganisha baadhi ya ibara kutoka kwenye Muhtasari uliowasilishwa kwenye Tume ya Serikali ya Kenya.

    Kwa niaba ya Jumuiya ya Shia Ithna-Asheri ya Tanzania, tunachukuwa fursa hii ya kuwaslisha maoni yafuatayo kwa mapendekezo ya Serikali juu ya shria inayofanana kwa wote ya Ndoa (Waraka wa Serikali Na. 1 wa mwaka 1969).

    Madhumuni yaliyodaiwa na mapendekezo haya ni kuondoa hali iliyopo ambayo kwayo “Sheria zilizopo hazitambui Ndoa zote zilizofungwa chini ya Sheria tofauti kama zinazolingana sawa”.

    Lakini je, ni lazima kwa madhumuni haya kutunga sheria ya ndoa inayofanana kwa wote? Je, suala hili haliwezi kufikiwa kirahisi kwa kuleta pamoja Ndoa zote chini ya mamlaka ya kisheria ya mahakama moja chini ya rejesta moja?

    Katika mwaka wa 1964 “Taarifa mpya ya Sheria za ki-Islamu” ilipitishwa inayosema kwamba hukumu za sheria za ki-Islamu za Ndoa ziwekwe katika mpango ulio wazi. Sheria ndogo chini ya amri hiyo ilichapishwa kama nyongeza ya Gazeti Na. 34 la 27 Juni 1967. Hii ndio ilikuwa iwe ni awamu ya kwanza.

    Tunashangaa kwa nini sera hii haikuweza kuendelezwa, au angalau kupanuliwa kujumlisha tofauti za sheria za ndoa za kimila hali kadhalika na za ki-Baniani na za Kikiristo. Sheria hizi zingeweza kupangiwa kanuni na kuwekwa chini ya mamlaka ya kisheria ya Mahakama moja.

    Hapo, na hapo tu, sura yenye mambo mengi ingeweza kuongezwa kushughulikia migongano ya sheria; (ni) baadhi ya mifano ambayo kwamba imetolewa katika Waraka wa Serikali.

    Tunatambua kwamba matatizo mabalimbali ya jamii yanayojitokeza ya matumizi mabaya au tafsiri potofu za sheria za kimila au zakidini kwa ujumla hutoa sabau kwa Serikali kuhusika kwa makini. Serikali katika juhudi za kuwapatia watu wake ustawi katika suala hilo, inakabiliwa na jukumu la kutokomeza maovu ya kijamii.

    Juhudi yoyote katika muelekeo huu yafaa kuungwa mkono na kustahiki ushirikiano wote. Lakini tunahisi kwamba wazo la kutunga Sheria ya wote kuchukuwa mahali pa taarifa mpya ya shria ya Ki-Islamu sio sahihi.

    Hata desturi zakimila (zisizo na mamlaka ya ki-Mungu) ni ngumu kubadilisha. Hii huwa hatari mno zaidi katika suala la sheria ya ki-Islamu ambayo ni sehemu muhimu ya dini yetu. Sheria hizi haziwezi kuvunjwa bila kupata hisia ya hatia na dhambi.

    Kwa hiyo tunahisi kwamba njia nzuri ingelikuwa “kuacha mamia ya maua kuchanua.” Umoja wa kitaifa hauhitaji kwamba raia wote lazima wawe na lahaja inayofanana au imani ya dini inayofanana. Hivyo kwa nini inafikiriwa kwamba ni muhimu kuwa na Sheria ya Ndoa na Talaka inayofanana ya kutumika kwa watu wote wa Tanzania?

    Sheria zetu za Shia Ithna-Asheri hazikutegemezwa juu ya “Ra’i (maoni) au “Qiyas” (analojia). Zimetegemezwa kabisa juu ya Qur’an Tukufu na Hdithi za Mtukufu Mtume na Maimamu wetu Kumi na Mbili.

    Kwa vile waraka unahusika na mambo ya Ndoa, lazima tuonyeshe kwamba kanuni zetu za msingi za Ndoa na Talaka zimetegemezwa juu ya Qur’an Tukufu. Mambo ambayo hayako wazi katika Qur’an yanaelezwa katika Hadithi.

    Wanachuoni wetu ambao wanaitwa MUJTAHID hawatoi hukumu yoyote kwa maoni yao, analojia (Qiyas) au (kwa) ijimai. Hakuna mamlaka kama hayo yaliyotolewa kw ayoyote katika sheria ya madhehebu yetu. Wanaweza kutofautiana katika kutafsiri Hadithi fulani zinazohusu baadhi ya mambo madogo, lakini hata hivyo tofauti hiyo ni tofauti katika tafsir, sio ya maoni.

    Shia Ithan-Asheri hufuata katika mambo yote ya dini hukumu za Mujtahid mkubwa wa zama. Anachukuliwa kuwa yeye ni muwakilishi wa Imamu wetu wa kumi na mbili na ni mtu (mwanachuoni) wa mwisho juu ya mambo yote ya kidini.

    Kwake yeye mumewekwa ndani yake masuala fulani, uwezo wa ulezi wa watoto, ndoa na talaka, utekelezaji wa wosia na mali ya marehemu na mambo kama hayo.

    Sheria ya ki-Islamu ya madhehebu ya Shia Ithna-Asheri ni chombo kilichofumwa vizuri. Hatuwezi kubadilisha au kurekebisha moja au mbili ya mambo yake bila kuharibu ufumaji wote.

    Kwa mfano, hukumu za ndoa na talaka zinabeba uzito wa moja kwa moja juu ya uhalali wa mtoto; juu ya dhambi ya pamoja ya mwanaume na mwanamke katika haki ya wao kwa wao wenyewe ya mirathi na ile ya mtoto. Mbali na mambo mengine ya jamii na matatizo halai.

    Katika sheria ya ki-Islamu mtu hawezi kutumia kitu chochote kilichopatikana kiharamu (kwa maana ya kidini) amma kwa kidunia au kwa madhumuni ya kidini. Kwa hiyo, kama mabadiliko yanafanywa katika sheria za mirathi, kwa mfano, mtu fulani anapewa zaidi kuliko haki ya mgao wake kwa mujibu wa Qur’an Tukufu maisha yake yote yatakuwa duni. Maisha yake ya kila siku yatakuwa ni orodha ndefu ya kuchupa mipaka, Sala zake, Hija, chakula na mavazi vitakuwa haramu katika maana ya dini.

    Hivyo ni wazi kwamba mfumo wa Sheria ya ndoa, talaka na mirathi hauwezi kubadilishwa. Vinginevyo hii itaanzisha muingilio wa moja kwa moja katika dini yetu.

    Kuhusu haki ya mwanamke katika sheria ya ki-Islamu tunataka kuwakilisha kwamba:

    Katika sheria ya madhehebu yetu mwanamke anazo haki hizo, upendeleo na ulinzi kwa muda wa Karne Kumi na Nne zilizopita, nyingi ya hizo hazikufikiriwa katika jamii zisizo za ki-Islamu mpaka kwenye Karne iliyopita na baadhi ya hizo mbele ya inayoitwa zama ya kisasa.

    Uislamu kwa mujibu wa madhehebu ya Shia umempa mwanamke haki ya kufanya mkataba yeye mwenyewe katika ndoa kama ni mtu mzima na makanifu.

    Uislamu umempa Mwanamke kitambulisho cha kujitengemea. Mwanamke wa ki-Islamu anamiliki mali yake mwenyewe hata baada ya kuolewa, na mume hawezi kuiingilia.

    Mwanamke anaweza kumfungulia mume wake mashitaka, anaweza kutoa ushahidi dhidi yake. Anarithi kutoka kwa mume kwa haki na mwanaume kutoka kwa mwanamke. Haki hii ya wote pamoja ya mirathi (kurithiana) ilitolewa wakati hakuna jamii kamwe ilifikiria kuhusu haki hii.

    Mgao wa mwanamke kwa kawaida ni nusu ya ule (mgao) wa mwanaume. Lakini hii ni mantiki kabisa. Uislamu umemfanya mwanaume kuwa na jukumu la kutunza familia. Hakuna mzigo kama huo uliowekwa juu ya mwanamke.

    Hata mke tajiri anahusika kupata matunzo yake kutoka kwa mume wake ingawa anaweza kuwa ni masikini. Kwa vile matunzo ya familia ni jukumu la mwanaume, amepewa ngao marudufu karibu katika mirathi yote.

    Mwanamke hupata Mahr (sio bei ya kuziba pengo ambalo ni geni kwenye fikira za Ki-Islam) ambayo hutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke. Uwiyano wa mgao uliowekwa katika Qura’an Tukufu kwa hiyo ni wa haki zaidi.

    Sheria ya Uislamu ihusikanayo na Wosia hairuhusu mtu kuusia zaidi ya thuluthi moja ya mali yake kamili. Hivyo hali ya kifedha ya wale watakaokuwa warithi (pamoja) na mke siku zote inalindwa na kutwaliwa isivyo haki na yeyote. Usalama huo bado unakosekana katika jamii nyingi ambazo huruhusu mtu kutoa mali yake yote hata kwa mgeni.

    Sasa tukija kwenye waraka wa Serikali wenyewe, kuna pendekezo moja ambalo katika mfumo wake uliopo, hukata ndani kabisa kwenye mzizi wa dini zote. Ni ule ushauri wa kwamba, “kama mwanaume ana kaa na mke kinyumba kwa muda wa zaidi ya miaka miwili basi atachukuliwa kwamba amemoa mwanamke huyo, na kama wamepata watoto, (basi) watoto hao watachukuliwa kuwa watoto halali wa mume na mke huyo.”

    Kama nia ni kutoa usalama kwa mke halisi ambaye Ndoa yake haikusajiliwa au ambaye Cheti chake cha Ndoa kilipotea, neno kinyumba halileti maana.

    Itapaswa libadilishwe kwa (maneno), “Kuishi pamoja kama mume na mke katika mazingira ya kifamilia, mradi inawezekana kwa wao kuoana na mmoja wao akadai ndoa ambayo haikukataliwa na mwingine; au katika hali ya kifo cha mmojawapo, kwa kawaida inajulikana kwamba walikuwa wameoana na haithibitishwi kwamba hakukuwa na ndoa kabisa.”

    Vile vile, tulitaja mapema, katika Uislamu mke hana wajibu wa kumtunza mume. Hivyo, makusudio ya Waraka kumfanya mke apasike kumtunza mume wake inakwenda kinyume kabisa na mamrisho ya Qur’an Tukufu.

    Kwa vile mjadala unaendelea juu ya suala la mitala, ni muhimu kuthibitisha tena kwamba tumeridhishwa vya kutosha na hali yenye kutaka kwa hakika umuhimu wa mitala katika hali nyingi. Jamii ya ki-Afrika, kama Waraka kwa usahihi unavyothibitisha, ni jamii ya ki-Mitala. Uislamu unakubaliana nao. Lakini Uislamu umeweka mpaka kwa wake wanne kwa wakati mmoja na umeamrisha, kwa taratibu makhsusi, usawa katika huduma na haki ya wake wote kama waraka unavyotaka iwe.

    Inapasa ikumbukwe kwamba mitala sio kitu cha lazima wala hakitetewi. Ni ruhusa tu yenye mipaka fulani na mashariti. Na katika baadhi ya mazingira ruhusa hii imeonyesha kuwa yenye manufaa mno.

    Kwa mfano: kama mke ana ugonjwa sugu, au mgumba au kwa sababu nyingine fulani haiwezekani kwa wawili hawo kuishi kama mume na mke. Suluhisho litolewalo na jamii fulani ni kumtaliki mke na kuoa mwingine. Lakini, je ni haki? Je, ni wema au uadilifu kumfukuza mwanamke katika hali ya uzee, katika umri wake wa kati kutoka kwenye nyumba yake, kwa sababu amekuwa mgonjwa siku zote au ametokea kuwa mgumba?.

    Uislamu hupinga ukatili huo kwa kuruhusu mitala.

    Hii ni mbali kabisa na utafiti wa kitakwimu kwamba wanawake wanawazidi wanaume katika Tanzania, wanawake 100 kwa wanaume 95; au katika ile misiba fulani kama vita, wanaume hukumbana na kifo zaidi kuliko wanawake. Kama mitala hairuhusiwi na jamii, italazimisha aslimia tano ya wanawake nchini kujiingiza katika ukahaba.

    Tunafikiri kiasi hiki kitatosha kuonyesha hekima ya Waraka wa Serikali katika kutambua mitala kama halali na desturi yenye “manufaa”. Lakini, katika mfumo wake wa sasa, Waraka hautakidhi madhumuni yanayohitajiwa. Je, itatokea nini kama pamoja na hali kuruhusu ndoa ya pili, mke wa kwanza akakataa kwa “hiari na kwa uhuru kukubali kuigeuza ndoa ya mke mmoja” kuwa ya mitala? Je; haitamlazimisha mwanaume kuwa “kwenye hali ambapo amma amtaliki mke wake wa kwanza au akae kinyumba (isvyo halali) na mke mwingine”, pamoja na athari zake zote zisizofaa zisizoepukika?.

    Njia nzuri ni kumtaka mwanaume aende kwenye baraza (au mahakama) iliyopendekezwa ya ndoa au kamati ya jumuiya yake na kuwathibitishia haja zake. Kama wakikubali, kukataa kwa mke wa kwanza hakupasi kufikiriwa kabisa.

    Tunachukulia kwamba, kwa vile hakuna suala la kubadilisha asili ya ndoa katika ndoa ya Mwislamu, Mwislamu hatahitaji idhini ya mke wa kwanza (au wake) kabla ya kuoa mke mwingine.

    TALAKA: Hakuna haja ya kusisitiza kwamba katika hali fulani talaka ndio suluhisho pekee lililobaki kwa wanandoa. Manufaa ya mfumo wa talaka yanaweza kuonekana kutokana na ukweli kwamba hata mabaniani na wakristo wamelazimika kwa nguvu ya moja kwa moja isiyoepukika kutunga sheria za talaka. Waraka umetambua hoja hii. Vile vile lazima ikumbukwe kwamba Uislamu, wakati ambapo unakubali hoja hii katika hali fulani, umetamka kwamba ni “Sheria halali yenye kuchukiza mno”. (makuruhu), itumikayo tu katika hali zilizo ngumu mno.

    Qur’an Tukufu imeweka chombo cha usuluhisho na jumuiya nyingi za ki-Islamu zina kamati kama hizo. Kwa bahati mbaya baadhi ya pande fulani hawakupendelea kabisa mfumo huu muhimu. Matumizi haya mabaya ya uhalali wa talaka lazima yaachwe na jaribio la waraka kudhibiti hali hii linakaribishwa sana.

    Masharti ya Talaka: Lazima tuonyeshe katika mwanzo kwamba madhehebu ya Shia Ithan-asheri ya Sheria ya ki-Islamu imeweka kanuni ngumu zilizotegemezwa juu ya Qur’an Tukufu na Hadithi kuhusiana na talaka. Talaka inaruhusiwa mradi tu inatamkwa mbele ya watu wawili mashahidi “Adil” (watu waliothibitishwa uaminifu wao) ambao husikia maneno na kuelewa chanzo cha talaka. Talaka lazima itamkwe katika utaratibu uliothibitishwa.

    Zaidi, ni lazima vile vile kwamba mume awe mtu mzima, mwenye akili timamu na mwenye kuelewa vizuri, atendaye kwa utashi wa uhuru wake mwenyewe na sio katika mshituko wa hasira au kutishwa, na kwamba lazima awe na nia ya dhahiri ya kuvunja ndoa.

    Kwa kadiri mwanamke anavyohusika, yeye wakati wa talaka lazima awe katika hali ya tohara na kwamba talaka haiwezi kutamkwa hata wakati wa tohara ambao kwamba mume amekutana naye kimwili.

    Kama moja ya mashariti yaliyotajwa hapo juu yakivunjwa, talaka itakuwa batili na kutenguka.

    Sheria ya ki-Islam haimpi mwanamke haki ya kutoa talaka, maoni yoyote kwamba mwanamke apasa kupewa haki ya kumtaliki mumewe yatakuwa ni kuingilia maadili ya dini, ambayo waraka umekariri kusema, sio nia ya Serikali.

    Familia ni msingi wa jamii, na kama ilivyo kila jamii, huhitaji mamlaka ya mwisho kuhifadhi nidhamu na ustawi wa jamaa (wa familia). Uislamu umetoa nafasi hiyo kwa mume ambaye amepewa haki ya kutoa talaka.

    Lakini mwanamke wa ki-Islamu anapasika kutoa maombi ya kuvunja ndoa au kuibadilisha yeye mwenyewe katika mazingira yafuatayo:-

    • Anaweza kuomba (Khula) ambayo yaweza kukubaliwa juu yake na mume.
    • Anaweza kumuomba Mujtahid (ambaye ni Kadhi katika Sheriat za Shia Ithna – Asheri) kumpa talaka kama mume maetoweka, au anakataa kumtunza.
    • Anaweza kuifuta ndoa kama mume ni mwenda wazimu au akawa mwenda wazimu baada ya ndoa.
    • Na anaweza kuibatilisha ndoa (baada ya kupeleka suala lake kwa Mujtahid) kama mume ni hanithi.

    Itakuwa muhimu, wakati wa kuandika hati ya rasimu, kutambua talaka iliyotolewa na Mujtahid na ubatilisho wa ndoa kwa kadiri ambavyo ndoa za Shia Ithna-Asheri zinavyohusika.

    Hukumu zilizotajwa hapo juu zinauhusiano juu ya masharti ya waraka kuhusiana na mume aliyetoweka. Kutoa talaka kwa Mujtahid (au hakimu katika suala la wasio kuwa Shia Ithna – Asheri au wasiokuwa Waislamu) ni sahihisho bora zaidi kuliko kudhania kwamba mume kafa (kwa madhumuni ya ndoa yake) na kudhani anaishi (kwa madhumuni mengine, pamoja na ndoa nyingine kama ipo yoyote) wakati mmoja na huo huo!

    Kwa vile Waraka kwa usahihi hutambua talaka iliyotolewa na mume mwislamu kama mwisho (wa ndoa), na kuitaka mahakama kusajili talaka hiyo bila uchunguzi wowote zaidi, tunataka kusisitiza kwamba talaka kama hiyo iwe inafanya kazi kuanzia tarehe ya kutamkwa kwa utaratibu wa talaka na mume, na sio tarehe ya kusajiliwa.

    Waraka humtaka Mwislamu akusudiaye kutoa taarifa ya kusudio lake siku 21 kabla kwa “Sheikh aliyeruhusiwa na Waziri kufungisha Ndoa.”

    (Waraka) umepuuza ukweli kwamba Mvulana wa ki-Islamu na msichana wanaweza kufunga Ndoa wao wenyewe bila kuwa na haja ya “kumwita Sheikh na kumuomba afungishe ndoa”. Tuna hakika sio nia ya Serikali kutengeneza Sheria mpya ya Uislamu ambayo ingelianzisha wachungaji kama wa Kikristo. Basi nini hii maana ya kutajwa Sheikh aliyeruhusiwa na Waziri? Ni wazi kwamba wazo hili linakwenda kinyume kabisa na Uislamu.

    Vile vile tunashindwa kuona haja yoyote kwa ajili ya pendekezo hili la taarifa ya siku 21. Tuchukulie msichana kutoka Kigoma na mvulana kutoka Pangani (wote wanaishi Dar es Salaam). Wakamjulisha Sheikh wa Jumuiya yao mjini Dar es Salaam kwamba wanataka kuoana. Sheikh yule hatarajiwi kuchapisha au kutangaza kusudio la ndoa katika magazeti au radio. Basi, vipi ataweza kujua kama kuna kikwazo chochote cha halali dhidi ya ndoa ile?

    Na hata hivyo, hakutakuwa hata ndoa moja kama hiyo ya kusudio la kiharamu katika ndoa elfu moja. Tunafikiri, ni bora kuiondoa sheria hii na kuibadilisha na nyingine kwa maana kwamba kama itakuja kufahamika hata baada ya kuona kwamba wasingeweza kuona kihalali, ndoa itakuwa batili na kutenguka kuanzia mwanzo.

    Kwa kadiri usajili wa Ndoa na Talaka unavyohusika, katika Jumuiya yetu rejesta za ndoa zimekuwepo kwa zaidi ya miaka 125 na tunatoa vyeti kwa wanandoa.

    Lakini lazima tusisistize kwa nguvu sana kwamba uhalali wa ndoa au talaka hauwezi kufanywa kwa kupasishwa na usajili. Yaweza ikafanywa kuwa ni kosa kwa zile ambazo hazikusajiliwa; lakini isije ikaathiri uhalali wa ndoa au talaka.

    Hivyo hivyo, katika hali nyingine pia, kama ndoa ni sahihi kwa mujibu wa dini, isije ikachukuliwa kuwa ni batili kama inapingana na masharti yoyote yaliyowekwa na waraka. Vinginevyo, itakuwa ni uingiliaji wa moja kwa moja katika dini.

    Madhumuni ya muhtasari huu ni kuidhihirishia Serikali kwamba utungaji wa sheria lazima ufanye juhudi ya kuhifadhi sheria za dini za Jumuiya mbalimbali zinazoishi chini ya bendera moja, hususani wakati sheria hizo zikiwa ni zenye athari nyingi juu ya misingi hiyo kama ndoa na maisha ya kifamilia.

    Kama tulivyoonyesha mapema, katika Uislamu Sheria na dini havitenganishwi, kwa vile sheria zetu zimeanzia kutoka kwenye Qur’an Tukufu ni wazi kwamba kama sheria yoyote inatungwa ambayo imma hupingana na maamrisho ya Qu’ran au Hadithi; kwa kawaida itasababisha vurugu kubwa katika akili za Umma wa ki-Islamu na kwa hiyo Jumuiya yote ya Uislamu itakuwa katika usumbufu.

    Mwishoni, tunapenda kufanya muhtasari wa maoni yetu kwa ifuatavyo:

    Tunahitaji kwamba badala ya kutunga Sheria inayofanana kwa wote, “Amri ya Taarifa mpya ya Sheria za “ki-Islamu” lazima ziwe katika matumizi kwa ajili ya Waislamu na uandikwe muswada wa Sheria ndogo chini ya Amri hiyo, uchapishwe na ifanywe itumike kwa mapema iwezekanvyo.

    Kwa kadiri mapendekezo ya Waraka yanavyohusika tunakubali kabisa kwamba “Ndoa lazima iwe muungano wa hiari” (ibara ya 6 ya waraka maelezo ya Kiingerza) kwamba wanandoa wasije wakawa ndani ya hadhi iliyokatazwa ya undugu au unasaba (ibara ya 9); kwamba yeyote kati ya mume au mke anweza kumiliki mali yake mwenyewe.” (ibara ya 19); kwamba mke awe na uwezo wa kutoa ushahidi dhidi ya mumewe (ibara ya 21); kwamba kuwe na masharti ya talaka “kama ndoa imevunjika kabisa” na kwamba “Talaka zisishughulikiwe juu juu (ibara ya 24); na kwamba kuwe na mabaraza ya usuluhisho” na “utambulisho kamili upewe mabaraza kama hayo ambayo yapo katika Jumuiya mbali mbali kabla ya sheria hii mpya unayokusudiwa” (ibara 25).

    Tunakubaliana na mapendekezo yafuatayo pamoja na masharti na sifa fulani:-

    Umri wa chini wa miaka 15 na 18 kwa wasichana na wavulana mtawalia (ibara ya 7) na usajili wa ndoa (ibara ya 17), na wa talaka (ibara ya 27) ni mambo mazuri tunakubaliana nayo ilimradi, kuvunja au kukiukwa kwao hakufanyi ndoa au talaka batili na kutenguka.

    Matamshi ya Mwislamu ya Utaratibu (formula) ya talaka yanatambuliwa na Waraka kama ushahidi wa kuvunjika kabisa kwa ndoa na mahakama inapaswa “kutoa cheti cha kuvunja ndoa”.

    Tunakubali pendekezo hili, ilimradi cheti kinachosemwa kinaanzia nyuma kuanzia tarehe ya kutamkwa kwa utaratibu wa talaka na mume.

    Tuko katika maafikiano kamili na pendekezo kuruhusu Ndoa ya mke mmoja kubadilishwa kuwa ya mitala. Lakini hatufikirii kuwa ni busara kusisistiza juu ya idhini ya mke wa kwanza (ibara ya 12). Mume anapaswa kuwa na haki ya kwenda kwenye baraza la Ndoa lililopendekezwa na uamuzi wao utakuwa wa mwisho.

    Vile vile, tunaona kwamba Ndoa ya Mwislamu ikiwa yenye uwezekano wa mitala, mume wa ki-Islamu hatatawaliwa na sharti hili.

    Tunafikiri kwamba pendekezo la kudhania mume (aliyetoweka kwa muda wa miaka 5) kama aliyekufa sio la busara. Njia nzuri ni kumruhusu Hakimu (au Mujtahid) kutoa talaka kama mazingira yatahitajia hivyo.

    Haki ya mwanamke kudai talaka au kuvunja au kutengua ndoa lazima ikomee kwenye mazingira yaliyotajwa mapema katika muhtasaari huu. Utungaji wowote wa sheria uendao kupita mpaka huo, utakuwa ni uingiliaji wa moja kwa moja katika dini yetu.

    Tunakataa kwa nguvu pendekezo kwamba kukaa kinyumba na mwanamke kwa muda wowote (mpaka wa miaka 2 ni wa kiholela kabisa) huwafanya hao wawili mume na mke kihalali. Vinginevyo mpaka utamkaji unabadilishwa kama, ilivyopendekezwa katika ibara ya 11 ya muhtasari huu, pendekezo hili haliwezi kukubaliwa.

    Tunakataa kabisa pendekezo la kumfanya mke kuwajibika kumtunza mume wake (ibara ya 19).

    Tunafikiri kwamba pendekezo la kutaka taarifa ya siku 21 halina maana kabisa, na kuunganisha katika hali ya Waislamu pamoja na usemi “taarifa itapelekwa kwa Sheikh, ambaye ameruhusiwa na Waziri kufungisha ndoa” huhitaji kuangaliwa kwa tahadhari sana, kwani huonyesha kuanzishwa kwa sheria mpya ya uchungaji ambao ni kinyume kabisa na misingi ya Ki – Islamu. Kwa hiyo hatuwezi kukubaliana nalo.