ArticleIDPicAddressSubjectDate
{ArticleID}
{Header}
{Subject}

{Comment}

 {StringDate}
 
ViewArticlePage
 
  • UTETEZI WA SHERIA ZA KIISLAMU SEHEMU YA TATU  
  • Sendtofriend
  •  
  •  
  • (4)

    MUHTASARI JUU YA SHERIA YA HIJABU NA MIRATHI*

    Mheshimiwa Rais,

    1. Kwa niaba ya Jumuiya na mashirika mbali mbali ya ki-Islamu, tunachukua fursa ya kufanya wasilisho hili kwa ajili yako wewe Mheshimiwa kulifikiria kwa huruma.

    2. Kaika wasilisho hili tunakomea wenyewe kwenye masuala mawili ambayo yalikuwa yakikera akili zetu kwa muda mrefu. Nayo ni: Hijabu kwa ajili ya wasichana wa ki-Islamu katika taasisi za elimu na Sheria za ki-Islamu zinazohusu Wosia na Mirathi.

    3. Mheshimiwa: Sisi wote ni raia wa nchi huru, na tumejipa katiba ambayo, pamoja na mambo mengine kuhakikisha uhuru wa kuabudu, dini, muungano na kuzungumuza. Hususan tanarejea kwenye Ibara 18 (1), 19 (1) (2) na 20 (1) ya Katiba ambazo ni kama ifuatavyo:-

    18 (1) Bila chuki kueleza shria za nchi, kila mtu anao Uhuru wa kutoa maoni na kuzungumza, na kutaka, kupokea, kugawa au kusambaza habari na maoni kupitia chombo chochote cha habari bila kujali mipaka ya kitaifa, na vile vile ana haki kutokana na kuingiliwa mawasiliano yake.

    19 (1) Kila mtu ana haki ya Uhuru wa mawazo au dhamira, itikadi au imani, na hiari katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa kubadili dini au imani yake.

    19 (2) Bila chuki kwenye sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, taluma ya dini, ibada na utangazaji wa dini utakuwa huru na jambo la binafsi la mtu binafsi, na mambo na uendeshaji wa vyombo vya Dini hautakuwa sehemu ya shughuli za mamlaka ya Dola.

    20 (1) Kila mtu ana haki ya kupewa uhuru, kutegemea Sheria za nchi, kukusanyika kwa uhuru na kwa amani, kuunganika na kushirikiana na watu wengine, kutoa maoni hadharani, na muhimu zaidi kuunda au kujiuunga na mashirika au vyama (vikundi) vilivyoundwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza itikadi zake au masilahi yoyote mengine.

    4. Allah (SWT) amesema katika Qur’an Tukufu

    neno lake la mwisho: “Na sikuwaumba majini na watu isipokuwa kwamba wanitumikie mimi”. (Sura 51, aya 56) Waislamu wote kuanzia mwanzo kabisa wanakubali kwamba neno “li ya budun” ambalo linatokana na (neno) “Ibadah” na linatafsiriwa hapa kama “tumikia”, maana yake unyenyekevu kamili.

    Mheshimiwa: Hakuna awezaye kufahamu zaidi kuliko busara zako nzuri kwamba “Ibadah” katika Uislamu sio kawaida ya baadhi ya ibada zenye kutekelezwa katika nyakati au siku makhususi. Huzunguka maisha yote ya Mwislamu. Uislamu maana yake kujisalimisha kwenye majaaliwa ya Allah (SWT) na wakati tunapoahidi kufanya hivyo tunaitwa Waislamu (ili) kutuongoza katika maisha yetu ya kidunia, na kutusaidia kufika karibu Yake katika maisha ya kesho akhera Allah (SWT) ametuma kwetu kupitia kwa Mtume Wake wa mwisho (s.a.w.) mfumo wa sheria wenye mambo mengi unaojumuisha mambo yote ya maisha … ya nyumbani, ya kijamii ya kifedha, ya kimaadili na ya kiroho.

    5. Mheshimiwa unajua vizuri sana kwamba Qur’an Tukufu haikushughulikia suala lolote la sheria kwa ufafanuzi zaidi (na uanagalifu) na katika namna ya utaratibu kwama sheria ya ndoa, wosia, mirathi na mambo mengine yanayohusika nayo, pamoja na adabu ya mavazi kwa wanawake.

    6. HIJAB: Ni lazima iwekwe wazi kuanzia mwanzo kwamba hukumu zinazoelekeza Wanawake kuvaa katika namna ambayo hufunika mwili wote na kuhifadhi muruwa wao zimetajwa kwa wazi katika Qur’an Tukufu. Ni urithi wa kawaida kwa Waislamu wote na haukukomea kwenye madhehebu au Jumuiya fulani. Vile vile, sio mila ya kitamaduni, ni sheria ya lazima ya Mungu, na haiwezi kuachwa bila kupata hisia ya dhambi na hatia.

    7. Kuna aya si chini ya tisa katika sura mbali mbali za Qur’an Tukufu zinazofafanua hukumu ya Hijab. Kwa ruhusa yako Mheshimiwa tunanukuu mbili ya hizo hapa chini:-

    “Nasema (Ewe Mtume) kuwaambia waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika; na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao, na wasionyeshe mapambo yao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzi wao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, au watumishi wanaume wasio na matamanio ya kijinsia au watoto wadogo ambao hawajapata elimu ya siri za wanawake; wala wasipige miguu yao ili yajulikane wanayoyaficha katika mapambo yao; na tubieni nyote kwa Allah; enyi waumini, ili mpate kufudhu (kesho akhera)”. (Sura 24 Aya 31).

    ‘Ewe Mtume’. Waambie wake zako, na binti zako na wanawake wa waumini wateremshe chini “Jilbab” zao, ili kwamba wapate kuhishimiwa ….” (Sura 33, Aya 59).

    (Jilbab = Joho Kubwa kuliko shela na fupi kuliko kashida, ambayo hufunika kichwa na kifua cha mwanamke).

    8. Kwa kutegemea juu ya aya hizi na aya nyingine za Qur’an Tukufu na Hadithi sahihi za Mtukufu Mtume (SAW) Wanachuoni wa ki-Islamu, bila utengano wowote wa hitilafu, wameamuru kwamba:-

    (a) Wanawake wa ki-Islamu lazima wafunike mwili mzima wakati wanapotoka majumba yao. Uso tu (lakini sio kichwa na nywele ) na viganja vya mikono vinaweza kuwa wazi.

    (b) Kuna hukumu maalum nz za shuruti za mavazi kwa ajili ya Sala na Hajj.

    (c) Nguo isiwe yenye kubana kuonyesha mikunjo kunjo ya mwili, wala nyepesi, (na kuonekana) kuyashinda madhumuni ya vazi (kama ilivyokusudia).

    (d) Wanawake hawapaswi kuvaa vazi ambalo kwa ujumla hutumiwa na wanaume, wala wanaume kuvaa za wanawake.

    9. Mheshimiwa! Wizara ya Elimu katika nchi yetu imechagua sare kwa ajili ya wasichana wa shule za msingi, ambayo ni mfano wa vazi la kimagharibi. Tunashangaa kwa nini uamuzi kama huo ulichukuliwa. Blauzi na sketi sio vazi la ki-Afrika, wala si la kikristo au la ki-Islamu. Kwa nini mtindo huo ni mtakatifu mno kiasi kwamba hauwezi kubadilishwa? Ingelikuwa vizuri zaidi kuwa na hamu yetu yakitaifa badala yake kuamuru (kuvaa) gauni refu na bui bui. Kwa vile ni vazi linalovaliwa na mamilioni ya wanawake wa ki-Afrika. Je, si wakati muafaka kwamba wenyewe tunaondokana na tabia kwamba yote yale yanayokuja kutoka nchi za Ulaya (Magharibi) ni mazuri kwetu, ambapo maadili yetu wenyewe ni ya “kishenzi”?

    10. Kwa mtazamo wa ukweli hapo juu, kwa unyenyekevu Mheshimiwa tunaomba uielekeze Wizara ya Elimu kuagiza (uvaaji) wa sare kama hizo kwa wasichana wa shule zenye kufunika vichwa vyao na mwili mzima, kuacha wazi nyuso na viganja. Inaweza kurahisishwa kwa kuvaa: skafu, gauni, suruali na soksi.

    Tunaamini kwamba itakuwa ni sare yenye heshima zaidi, na itaruhusu hata wasichana kushiriki katika riadha na michezo kwa uhuru bila hofu ya kuonekana aibu yoyote.

    11. Mheshimiwa: Kama kwa sababu yoyote ni vigumu kuanzisha sare hizi kwa wasichana wote, basi wasichana wa ki-Islamu waruhusiwe nchi nzima kuvaa sare hizo bila pingamizi au kizuizi chochote, kwa vile ni sheria ya dini yao na sio kikabila au mila ya kitamaduni.

    12. Kabla hatujaendea masuala mengine, tungependa kwa huruma zako Mheshimiwa kutoa taarifa kwako kwamba wasichana wa ki-Islamu wanaoishi Uingereza na Ufaransa wamepata haki yao ya kuvaa Hijab mashuleni, ingawa ilichukuwa hatua za kimahakama (na katika suala la Ufaransa, uingiliaji kati ya Tume ya haki za binadamu ya Uingereza) kuipata haki hiyo. Karibu na nyumbani nchini Kenya,mwaka huu (1990) msichana Mwislamu wa ki-Afrika alishinda kesi mahakamani dhidi ya mamlaka za shule wakati zilipokataa kumruhusu kuingia shule na Hijab. Gazeti rasmi la KANU (liitwalo) the Kenya times (Nairobi) liliandika tahariri tarehe 2/2/1990 ambayo kwayo pamoja na mambo mengine liliandika:

    “ Kwa nchi ya Kidemokrasia kama hii yetu, ambako uhuru wa kuabudu kwa dini zote umehifadhiwa katika Katiba, ni vigumu kuamini kwamba baadhi ya watu wanaona ni sawa kuwanyima wengine uhuru huu”.

    “Dini, kama tujuavyo, ni jambo lililo karibu sana na mioyo ya baadhi ya watu kuwanyima uhuru wa kuelezea hisia zao wakati wowote wanapotaka kufanya hivyo ni kuwa dhidi ya juhudi zote katika kujenga jamii yenye amani na upendo”.

    “Chukuwa Uislamu kwa mfano, ni mfumo kamili wa maisha. Kumtaka mfuasi yeyote muaminifu wa dini hii kuacha baadhi ya mambo ya maisha haya, hakika ni kumuambia akatae yale yalioandikwa katika Qur’an Tukufu. Na sisi ni nani, katika wadhifa wowote ule uwao tunaoundesha, kuingilia maisha ya ndani ya watu wengine na dini zao? Suala la msichana huyu wa ki – Islamu kuambiwa afunue kichwa chake wakati akiwa katika eneo la Shule halipaswi kutokea. Hali kadhalika kuwanyima watoto haki yao ya elimu kwa sababu wanavaa vilemba si ya kuvumiliwa.”

    13. SHERIA YA KIISLAMU YA MIRATHI:

    Tumepata kuelewa kwamba Serikali inakusudia kufanya mabadiliko katika sheria ya ki-Islamu ya mirathi. Tulikerwa mno na habari hizi: Kama tulivyo wasilisha mapema, Qur’an Tukufu imeweka kwa usahihi na uwazi mno zaidi hukumu zinazohusiana na mirathi, kwa ufafanuzi kabisa ikitoa kwa warithi mbali mbali migao yao katika mali ya Mwislamu marehemu. Sheria ya ki-Islamu ni chombo kilichofumwa vizuri. Hatuwezi kubadilisha au kurekebisha moja au mbili ya mambo yake bila kuharibu ufumaji wote. Kwa mfano, katika sheria ya ki-Islamu mtu hawezi kutumia kitu kilichopatikana kiharamu (katika maana ya dini), amma kwa kidunia au kwa madhumuni ya kidini. Kwa hiyo kama madiliko yanafanywa katika Sheria ya mirathi, kwa maana hiyo mtu fulani kwa kawaida atapata zaidi kuliko mgao wake (ule ambao amegaiwa na Qur’an Tukufu). Pato hilo la haramu litafanya maisha yake yote kuwa duni. Maisha yake ya kila siku yatakuwa ni orodha ndefu ya madhambi na kuchupa mipaka. Sala zake zitakuwa batili; Hija yake itakuwa batili na kutenguka; hata chakula chake na mavazi vitakuwa haramu katika maana ya dini. Mtu kama huyo kamwe hawezi kutarajia amani katika maisha ya kesho akhera.

    14. Hatujui ni nini maana halisi ya zoezo hili. Kwa hiyo hatuwezi kusema zaidi kwa sasa. Lakini tunarudia kusema kwamba sheria hizi zimeegemezwa juu ya Qur’an Tukufu na haiwezekani kuweka mpaka baina ya Sheria hizi na Qur’an Tukufu. Jambo lolote la kubadilisha migawanyo ya ki – Qur’an itakuwa sawa na kubadilisha Qur’an Tukufu .

    15. Hata hivyo, katika mintaarafu hii, tungetaka kuvuta nadhari yako Mheshimiwa kwenye Amri ya Taarifa mpya ya Sheria ya ki-Islamu ya Serikali ya Tanzania (Na. 56 ya 1964), ambayo chini yake, kazi ilianzishwa ya kupanga kanuni za Sheria za ki-Islamu, ikitoa utambulisho halisi kwa madhehebu. Sura nne zinazo husika na Ndoa, Ulinzi wa watoto n.k. zilichapishwa pia kama sheria ndogo chini ya sheria hiyo katika nyongeza ya Gazeti Na 34 la 27 Juni 1967. Ilikuwa ni hatua ambayo ilifurahisha Umma wote wa Ki-Islamu wa nchi hii. Kwa bahati mbaya mpango ule uliachwa. Bado, kama mpango ule utahuishwa, ambao kwayo hukumu za kila Madhehebu zinatambuliwa kama Sheria zitumikazo kwenye Jumuiya hiyo, na sheria hizo zikapangiwa kanuni katika juzuu moja kwa rejea za urahisi kwa Mahakama za Sheria, itakuwa hatua ya kusifia sana ambayo kwamba Umma wote wa Waislamu wa Tanzania watakuwa siku zote na shukurani kwako wewe Mheshimiwa.

    (4)

    MAHAKAMA YA KADHI:BAADHI YA MAPENDEKEZO*

    Waislamu nchini kwa muda mrefu wamekuwa wakidai kuwepo na Mahakama ya Kadhi katika Tanzania itakayoangalia na kushughulikia mambo maalum ambayo yanajumuishwa zaidi na Sharia za Kiislamu kuliko Sheria za Mahakama za kawaida.

    Ukweli kwamba tayari ipo Mahakama ya Biashara (Uchumi), ni uthibitisho tosha kwamba mambo maalum (ya aina moja) yanahitaji kushughulikiwa na Mahakama maalum ambayo vitabu vya Sheria vya kawaida huyafafanua kwa nadra (uchache).

    Hata hivyo, tayari inakubalika kimsingi kwamba hakuna utata katika suala hili, kwani Rais Benjamin Mkapa ameshasema atayashughulikia matatizo yote yanayowakera Waislamu na kuhakikisha kuwa Waislamu wote nchini hawajisikii kunyanyaswa kwa vile sera ya Chama tawala (Serikali) ni Usawa miongoni mwa Wananchi wake, bila kujali jinsia, rangi (Utaifa), au Dini.

    Kwa mantiki hii, mapendekezo kadhaa yanatolewa kuisaidia Mahakama ya Kadhi iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi na kupatikana madaraka kamili ya kisheria ya Mahakama ya Kadhi.

    Ili Mahakama iweze kupata hadhi yake, haya ni mapendekezo ambayo yangeweza kusaidia kufikia lengo hilo.

    Mswada unalenga kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi katika kila Wilaya ya Tanzania, ili kuangalia mambo yote yahusianayo na Sharia ya Kiislamu katika masuala ya Ndoa, talaka, haki ya kulea watoto, mgawanyo wa mali, Urithi n.k. pale ambapo wahusika wa utata huo ni Waislamu, waliooana kwa mujibu wa sharia na desturi ya ndoa za Kiislamu.

    Ukweli ni kwamba makusudio ya mswada huu ni mazuri, lakini upo uwezekano mkubwa kwamba kutokana na ukosefu wa Kitabu makhususi cha Sheria za Kiislamu, Makadhi katika wilaya mbali mbali wakifikia kwenye uamuzi wa kesi zinazofanana, wanaweza wakatoa hukumu zinazopingana.

    Hivyo, upo umuhimu wa kukiandaa kitabu makhsusi kitakachotumika kama Mwongozo wa Makadhi ili kuiepuka migongano.

    Hapo zamani mwaka 1964, Bunge la Tanganyika kwa wakati huo lilipitisha “Sharia ya Kiislamu (Sheria ndogo)” iliyompa madaraka Waziri aliyehusika na mambo ya Sheria kuandaa na kuchapisha kipengele cha Sharia ya Kiislamu baada ya kushauriana na wanachuoni wa Sharia za Madh-hebu za Kiislamu.

    Katibu Mkuu wa Bunge wakati huo, alikamilisha kuandika Mswada wa ndoa wenye sehemu 4 (kama ulivyokubaliwa na wanachuoni wa Sharia za Kiislamu kutoka Madh-hebu matatu Kiislamu Shafi’i, Hanafi na Shia).

    Mswada huu uliotolewa kama Sharia ndogo chini ya kifungu kidogo cha Sharia ya Kiislamu (Na: 56 ya mwaka 1964) ikiwa ni sehemu ndogo ya Gazeti la Serikali na Na: 34 la tarehe 27, Juni, 1967.

    Ilifahamika kuwa sehemu zilizosalia, kuhusiana na kuwalea watoto na talaka n.k. zingechapishwa mapema. Lakini zoezi hili lilisitishwa na badala yake serikali ilitunga sheria ya ‘Ndoa’ kupitia Mswada wa Ndoa wa mwaka 1971.

    Hata hivyo, kanuni ya Sheria ya Ki-Islamu 1964 bado haijafutwa na bado ni sehemu ya Kitabu cha Bunge. Na kwa sababu sasa serikali inakusudia kuanzisha Mahakama za Makadhi katika kila Wilaya, ni wakati muafaka wa kufufua tena mswada wa sheria ya Kiislamu ya mwaka 1964 ili ufanyiwe kazi na kazi hii ianzie pale ilipoachiwa.

    Jambo muhimu hapa ni kuepusha uwezekano wa Makadhi kutoa hukumu zitakazoleta utata. Vinginevyo, mzigo wa kazi za Mahakama Kuu utaongezeka kwa kuwa rufani kutoka Mahakama za Makadhi zitajazana kwenye Mahakama ya Rufaa.

    Madhehebu za Makadhi wa Wilaya:

    Kwa vile Waislamu wengi wa Tanzania ni wafuasi wa Madhehebu ya Shafii ni vizuri makadhi wa Wilaya watokane na Madhehebu ya Shafii.

    Lakini iwapo wahusika au mhusika wa mgogoro ni wa Madhehebu isiyo ya Shafii, inapendekezwa kuwa Kadhi wa Wilaya asaidiwe na wanachuoni wa madh-hab inayohusika.

    Hii itafuta uwezekano wa kutolewa hukumu isiyo sawa na itawapa imani ya kutendewa haki wahusika au mhusika. Wasaidizi wa Kadhi wa Wilaya waliotajwa hapo juu itabidi watayarishwe katika kila Wilaya na wanaweza kuangaliwa upya (kuteuliwa) muda baada ya muda.

    Iwapo mapendekezo mawili muhimu yaliyotajwa hapo juu katika makala haya yatakubalika na kufanyiwa kazi, itakwenda hatua kubwa kuwatendea haki na usawa Waislamu wote nchini.