ArticleID PicAddress Subject Date
{ArticleID}
{Header}
{Subject}

{Comment}

 {StringDate}
 
 
 
 
 
 
 
ViewArticlePage
 
 
 
 • MATATIZO YA KIMAADILI SEHEMU YA PILI  
 • Sendtofriend
 •  
 •  
 • Sehemu ya pili

  Hulka Mbaya Husababisha Chuki

  Baadhi ya tabia na hulka zisizotakikana hudhoofisha misingi ya mapenzi, na wakati mwingine husababisha kuvunjika uhusiano mzuri kabisa. Watu wakali ambao hawawezi kuhifadhi mapenzi yao juu ya wengine, hujenga ukuta mgumu baina yao na jamii ambao huwazuia wasione mwanga wa mahaba. Kwa hivyo, tabia mbovu huharibu msingi wa furaha na hushusha thamani ya mtu.

  Hakuna anayekataa kwamba tabia mbaya huwatenganisha na kuwaweka watu mbalimbali, kwa sababu mtu mzuri huchukia kufanya urafiki na mtu mbaya mwenye tabia mbovu. Hivyo, tabia mbaya huwalazimisha wapoteze suhula nyingi ambazo zingekuwa na manufaa makubwa kwa ajili ya maendeleo ya maisha yao lau wangelikuwa na tabia njema na wenye adabu.

  Ni lazima kwa yule mtu anayetaka kuingiliana na jamii, kwanza ajifunze sanaa ya maingiliano, kisha akishaijua barabara, afuate kimatendo kufuatana na adabu za kijamii zinazokubaliwa. Bila ya njia hii, mtu hawezi kuishi kwa masikilizano na jamii yake, wala mwendo wake hauwezi kukamilika katika jamii hiyo. Kwa hivyo, mwendo mwema ni msingi mkuu wa furaha na ufanisi, vilevile, ni jambo muhimu katika kuboresha shakhsia na hadhi ya mtu.

  Kwa hakika, mwenendo mzuri humwezesha mtu atumie vipawa vyake na kuweza kufaa katika kiwango

  31

  chote cha uendeshaji na ustawi wa jamii na maisha. Hakuna mwendo wowote ulio sawa na tabia njema katika kuvuta mapenzi na mahaba ya watu na katika kupunguza maumivu yanayoweza kuyakabili maisha.

  Wale wanaobarikiwa tabia nzuri kama hizo hawadhihirishi kwa wengine hali yao ya huzuni; na huzuia isitoke nje ya maisha yao ya faragha. Watu kama hao hujitahidi kuleta mazingira ya furaha na ufanisi kati yao ili kwamba wale wanaoingiliana nao wasahau mashaka yao kwa kupewa hisia ya matumaini na utulivu. Wao pia huonyesha utulivu na raha yao ingawa wana matatizo, lakini kwa njia hii huzidisha uwezekano wao wa kupata ufanisi na ushindi.

  Tabia nzuri ni nguzo madhubuti kabisa ya kujipatia mafanikio kwa watu wengi. Hapana haja kusema kwamba mafanikio ya kibiashara ya mashirika yanahusiana moja kwa moja na mwendo mzuri wa wafanyakazi wake.

  Kwa kawaida, mkurugenzi wa shirika mwenye tabia nzuri huwa mwenye nishati na jitihada, na huvutia kwake maingiliano mengi. Kwa ufupi, hulka na tabia njema ni siri ya kupendwa na kukubaliwa na watu. Watu hawawezi kuwavumilia watu wenye tabia mbaya hata wawe na vyeo gani. Ukichungua mwenyewe utaona sababu ya baadhi ya watu kupendwa na wengine. Mwanachuoni mmoja wa Magharibi ameandika haya kuhusu uzoefu wake katika uwanja huu:

  "Siku moja niliamua kufanya uchunguzi vipi furaha na ubashasha wa uso wangu unavyoathiri maisha yangu. Kabla ya siku hiyo nilikuwa na huzuni; na asubuhi

  32

  iliyofuatia nikaondoka nyumbani nikiwa na nia ya kuwa mchangamfu. Nikafikiri moyoni mwangu kwamba nimeona mara kadhaa kwamba sura changamfu na za ucheshi za watu zilinipa nguvu na nishati. Nilitaka mwenyewe kugundua ikiwa mimi mwenyewe ningeweza kuwaathiri wengine kwa namna hiyohiyo. Nilipokuwa nikielekea kazini nikakariri mwenyewe kwamba azma yangu ni kuwa mcheshi na mchangamfu. Hata nikajiaminisha kwamba nilikuwa mtu mwenye bahati sana. Na matokeo yake, nikahisi raha mwilini mwangu. Nikahisi kana kwamba nataka kuruka. Nikatazama pande zote kwa uso wa bashasha sana; bado nikaona ziko nyuso nyingi zinazoonyesha huzuni. Moyo wangu ulinichoma kwa ajili ya watu hao, nikatamani lau ningeliweza kuwapa chembe za furaha ya moyo wangu.

  "Asubuhi hiyo niliingia ofisini na nikamwamkia mhasibu kwa namna ambayo hakuwahi kuamkiwa na mimi. Kabla yake sikuwa tayari kumwamkia kwa bashasha namna hiyo hata kwa kima cha kuokoa maisha yangu! Mhasibu hakuwa na budi ila kunijibu kwa ukunjufu na mapenzi. Wakati huo nikahisi kwamba furaha yangu imemuathiri barabara.

  "Rais wa shirika langu ninapofanya kazi ni mtu ambaye hakiinui kabisa kichwa chake anapozungumza na wengine ni mtu mchapwa sana. Siku hiyo alinitolea ukali sana kuliko siku nyingine yoyote. Nisingeweza kumstahamilia, lakini kwa kuwa niliamua nisikereke kwa jambo lolote, nikamjibu kwa namna ambayo ikafanya mikunjo ya kipaji chake iondoke. Huo ulikuwa mkasa wa pili siku hiyo. Baadaye siku hiyo, nikajaribu

  33

  kuendelea kutabasamu na kuchangamka na wafanyakazi wenzangu.

  "Kwa njia hiyo, nikaweza hutekeleza mbinu hiyo kwa familia yangu, na matokeo yake yakawa mazuri. Kwa hivyo, nikagundua kwamba ninaweza kuwa mchangamfu na mwenye furaha, na nikawafanya wenzangu wahisi vivyo hivyo.

  "Jambo hili linawezekana kwako pia. Onana na watu kwa hali hii, uso wako uwe na bashasha, na utaona maua ya furaha yakichanua katika maisha yako kama vile mawaridi yanavyochanua katika majira ya machipuo; na utapata marafiki wengi watakaokuletea amani na utulivu wa daima."

  Hakuna mtu anayekataa athari kubwa ya tabia hii katika kulainisha nyoyo za maadui. Heshima na tabia nzuri husaidia sana kuwasadikisha wapinzani wafuate itikadi fulani.

  Mwandishi mwingine wa Magharibi amesema haya kuhusu jambo hili:

  "Milango yote hufunguliwa yule anayetabasamu na akawa na tabia nzuri, lakini wale wenye tabia mbaya hubidi wagonge milango ili wafunguliwe kama vile wahuni. Mambo bora kabisa ni yale yanayohusiana na adabu, tabia nzuri na uchangamfu."

  Hata hivyo, ningependa kuongeza kwamba tabia njema hulazimu furaha na huwaongoza kwenye ukamilifu watu wenye hulka nzuri, lakini kwa sharti kwamba tabia hizo ziwe zinachimbuka ndani ya moyo wa mtu bila ya kuwepo unafiki au kujidai.

  Kwa maana nyingine, ni lazima hisia ya mapenzi

  34

  iwe ni madhihirisho ya yaliyomo moyoni. Uzuri wa nje peke yake si dalili ya ubora wa ndani na usafi wa mwendo wa mtu, kwa sababu inawezekana hiyohiyo mienendo mizuri ya kidhahiri ya mtu ikawa inakinzana na kuhitalifiana na moyo wake uliochafuka na uliopotea. Kwani kuna mashetani wengi wanaovaa nguo za malaika ili kuficha nyuso zao za kutisha nyuma ya pazia la uzuri.

  Mtume Mtukufu Hutoa Kielelezo

  Sote tunajua kwamba mojawapo kati ya sababu kubwa kabisa ya kuendelea Uislamu ni mwendo na tabia njema ya Mtume Mtukufu SAW. Kuenea Uislamu kutokana na maadili mema ya Mtume kumetajwa na Mwenyezi Mungu pia:                 '

  "Na kama ungelikuwa mkali na mwenye moyo mgumu, bila shaka (watu) wangekukimbia."

  (Aal 'Imraan, 3:159)

  Mtume Mtukufu aliwakunjulia watu wote moyo wa mapenzi. Upendo wake mkubwa juu ya watu, upole na mvutio wake ulikuwa ukidhihirika kwenye uso wake wa kimalaika. Alikuwa akiwatendea vizuri na kuwakirimu Waislamu wote sawasawa.

  "Mtume Mtukufu SAW alikuwa akiwashughulikia na akigawa wakati wake kati ya masahaba zake

  sawasawa/

  (Rawdhatu 'l-Kafi,uk. 268)

  35

  Mtume wa Uislamu alikuwa akikataza tabia mbovu, na alikuwa akisema:

  "Tabia mbaya ni kisirani, na mtu mwovu kabisa kati yenu ni yule mwenye tabia mbovu."

  (Nahju 'l-Fasahah.uk.. 311)

  Mahali pengine amesema:

  "Enyi wana wa Abdul Muttalib! Ninyi hamtaweza kamwe kuwaridhisha watu kwa mali zenu, hivyo, kutaneni nao kwa uso mchangamfu na mwendo mzuri." (Wasa'ilu 'sh-Shi'ah, jz. 2, uk. 222)

  Aliyekuwa mtumishi wa Mtume Mtukufu, Anas bin Malik, alikuwa daima akikumbuka hulka nzuri ya Mtume Mtukufu, na alikuwa akiwaambia watu kwamba katika kipindi cha miaka kumi aliyomtumikia Mtume Mtukufu, hakuwahi kabisa kumwona ameukunja uso wake unaonawiri, wala hakuwahi hata mara moja kumwona amepandisha nyusi zake au ameonyesha uso wa hasira kwa sababu ya kufanya jambo lisilopendeza.

  Tabia njema na uchangamfu ni katika sababu zinazozidisha umri wa mtu. Imam Sadiq AS amesema:

  "Wema na tabia nzuri hustawisha ardhi na huzidisha umri."

  (Wasa'ilu 'sh-Shi'ah, jz. 2, uk. 221)

  Dk. Sanderson ameandika yafuatayo kuhusu mada hii:

  "Uchangamfu ni mojawapo kati ya vitu muhimu vinavyozuia na kuponesha maradhi. Madawa mengi

  36

  baada ya kutoa nafuu ya haraka na ya juujuu tu huanza kuonyesha udhaifu wake, lakini ukunjufu na uchangamfu unaleta athari za kudumu ambazo huonekana mwilini mzima. Uchangamfu hunawirisha macho, huchangamsha viungo, huimarisha miguu na husafisha sauti. Watu wenye tabia nzuri na uchangamfu, furaha zao zote huzidi na hupata matumaini, damu huzunguka haraka sana viungoni mwao, hewa huingia kwa raha zaidi mapafuni mwao, afya na siha ya miili yao huimarika barabara na huvunja nguvu za ugonjwa!"

  (Pintzi Fikr)

  Jambo linalovutia katika usemi huo wa Imam Sadiq AS ni hili kwamba kutenda mema pamoja na tabia nzuri husababisha umri wa mtu kuzidi, kwa sababu mtenda mema katika kutenda mema na mazuri huhisi furaha na hupata ukunjufu maalumu katika nafsi yake, na kwa sababu hii kutenda mema kwa upande wa kiafya huleta athari na matokeo kama yale ya tabia njema. Vivyo hivyo, Imam ameihesabu sifa njema hii kuwa ni miongoni mwa vitu vinavyoleta bahati nzuri kwa binadamu:

  "Tabia njema ni miongoni mwa ufanisi wa mtu."

  (Mustadriku 'l-Wasa'il, jz. 2, uk.S3)

  Samuel Smiles ameandika haya kuhusu maudhui hii:

  "Kuna msemo maarufu unaosema kwamba  kadiri ustawi na ufanisi wa mtu katika maisha yake unavyohusiana na uwezo wa nafsi yake na kipawa chake cha kiasili, vivyo hivyo, kwa kadiri hiyohiyo huhusiana

  37

  na tabia njema, afya na siha yake pia."

  Hulka nzuri husababisha kupanuka maisha ya mtu, kuzidi riziki na kupatikana mapenzi na masikilizano.

  Imam Ali AS amesema:

  "Tabia nzuri hupanua riziki na huvuta (nyoyo za) urafiki."

  (Ghuraru 'l-Hikam, uk.279)

  Bwana S. Marden ameandika haya katika kitabu chake kiitwacho, Khawishtan Sazi:

  "Ninamjua meneja mmoja wa hoteli ambaye kutokana na mwendo na tabia yake nzuri amekuwa mashuhuri na amejipatia utajiri mwingi kwa kadiri kwamba wasafiri na watalii walikuwa wakifunga safari ndefu ili waje katika hoteli yake, kwa kuwa mazingira ya hoteli hiyo ilifanana na ya nyumbani kwao. Wageni wanapoingia katika hoteli hiyo hukaribishwa kwa furaha na tabasamu maalumu ambayo huoni katika hoteli nyinginezo. Kwa ufupi, hali ya kutokuwepo ukarimu na ubashasha katika hoteli nyinginezo haikuwepo hapo. Watumishi wa hoteli hiyo daima hujitahidi kama inavyomkinika kuweka uhusiano wa kiurafiki kati yao na washitiri. Watumishi huwahudumia washitiri wao kwa uso wa tabasamu na huwashughulikia kwa mapenzi yanayotokana na upendo wao. Huwafanya wageni wapendezwe na mwendo wao mzuri na waipende hoteli hiyo kwa kadiri kwamba watake kuja tena na wawasifie wenzao. Ni wazi kwamba mwendo huu huwavutia wageni wapya."

  Mwandishi ameongeza:

  38

  "Adabu na tabia nzuri hazikuwa na thamani kubwa katika zama zozote kama sasa zilivyo. Katika zama hizi kuwa na shakhsia (hadhi), haiba na tabia nzuri, na kujitahidi kuwasaidia watu kumekuwa ni rasilimali ambayo kila mtu anataka kuwa nayo ili apate mafanikio katika maisha yake."

  Kufuatana na maneno ya Imam Sadiq AS, uchangamfu ni alama ya uelevu na ukamilifu wa akili ya mtu. Amesema:

  "Watu wenye akili kamilifu kabisa ni wale wenye tabia nzuri kabisa."

  Watu wenye kutumia akili vizuri sana, tabia zao pia huwa ni bora zaidi kuliko watu wengine.

   

   

   

  Samuel Smiles amesema:

  "Kwa kadiri ambayo historia inavyoonyesha, jambo hili limethibitika kwamba wenye vipawa vikubwa wote walikuwa ni watu wenye furaha na wachangamfu, kwa kuwa wamefahamu maana halisi ya maisha na wakazidhihirisha roho zao katika kazi na athari zao. Wakati mtu anapozisoma athari zao (za utafiti), huona waziwazi humo alama za busara, roho safi, shauku na uchangamfu wao. Watu wote wenye roho bora kabisa na hekima kubwa huwa wana furaha na bashasha, na tabia zao ni viigizo ambavyo kila mtu akivutika navyo huvifuata na hupata mwanga wa furaha na uchangamfu halisi kutoka kwao."

  Mtume Mtukufu SAW amesema:

  "Vitakavyowaingiza kwa wingi umma wangu katika Pepo ni ucha Mungu na tabia njema."

  (Wasa'ilu 'sh-Shi' ah,jz. 2, uk. 221)

  39

  Kwa hivyo, mtu ambaye ameifanya akili yake kuwa ni kiongozi wake wa maisha, na anataka kuishi kwa heshima na hadhi, inampasa aitafute rasilimali hii ya kiruhani yenye thamani. Vivyo hivyo, mtu inampasa awe na shabaha madhubuti na uwezo mkubwa ili aweze kuing'oa mizizi ya sifa na tabia mbaya. Kuzingatia madhara yanayotokana na tabia mbaya kunatosha kumfanya mtu apigane dhidi yake.

  2 - DHANA NZURI

  43

  Matumaini na Utulivu wa Roho

  Katika uwanja wa misukosuko ya maisha, binadamu hahitajii kitu chochote isipokuwa utulivu wa moyo. Katika medani ya mapambano ya kimaisha, mtu asipokuwa na silaha hiyo, atashindwa katika mapambano mwisho wake. Kwa kadiri maisha yanavyokuwa magumu zaidi ndivyo mahitaji yanavyozidi kwa kadiri hiyohiyo. Tuangalie vipi tutaweza kujitoa katika fadhaa na misukosuko hiyo na tukafuzu kuingia katika mazingira ya utulivu.

  Kutafuta utajiri, madaraka, umaarufu, mambo na hali za kimaada na kidunia ili kujipatia raha na starehe ni kazi bure; kwa sababu chimbuko la raha linaanza katika umbile la mtu mwenyewe, kama vile ambavyo chanzo cha visirani kinaanza katika ulimwengu huohuo wa ndani. Kile kinachowezekana kutumiwa katika hazina za thamani za nguvu za ndani kwa madhumuni hiyo, hakipatikani katika mahitaji ya nje; kwa sababu machimbuko yote ya ustawi na raha ya nje na vilevile nyenzo na mategemeo yote yanayotumika katika njia hii, huwa ni ya muda na ya kupita mara moja tu, na ni muhali kwa binadamu kupata raha kamili. Utajiri wa tafakuri na sifa njema ni vitu vya pekee visivyoweza kuangamia ambavyo kwamba humtosheleza mtu kikamilifu asitegemee mambo yasiyokuwa na msingi.

  Apictatus, mwanafalsafa mashuhuri wa Kiyunani, amesema:

  44

  "Ni lazima tuwafunze watu kwamba hawawezi kupata ufanisi na bahati nzuri katika mahali wanapopatafuta ovyoovyo. Ufanisi halisi hauko katika nguvu na uwezo, kwa sababu Mirad na Angluis walikuwa ni watu wenye bahati mbaya ingawa walikuwa na nguvu na uwezo mkubwa sana. Ufanisi haupatikani kwa kuwa na vyeo na madaraka ya kisiasa, kwani makaizari (wafalme) wa Kirumi walikuwa na vyote lakini hawakuwa na furaha wala raha.

  "Kwa kweli, ufanisi hauwezi kupatikana kwa kuwa mashuhun na kuwa na neema na vipawa vyote hivyo, kwani Nero, Sandpapal na Aghamnin ambao walikuwa navyo vyote hivyo, lakini daima walikuwa na majonzi na wakilia, na kila msiba ulikuwa ukiwasibu wao. Kwa hivyo, ni lazima kila mtu atafute raha na ufanisi halisi katika nafsi na dhamiri yake mwenyewe."

  Ni lazima isemwe kwamba ufumbuzi wa siri na mafumbo mengi ya maumbile ya ajabu, na vilevile kuzidi na kukamilika kwa suhula za kimaisha katika zama hizi hakutoshi kumpatia mtu maisha yasiyokuwa na mashaka na matatizo. Licha ya hayo, teknolojia na suhula hizo zimemwongezea binadamu wasiwasi na mashaka mapyamapya. Kwa hivyo, ili kujiondoshea dhiki na mashaka ya daima ya maisha na mawingu mengi yanayothakilisha roho zetu, tunahitajia haraka fikra wazi na nyongofu; fikra ambayo ni nguvu amilifu kabisa katika dunia yetu iliyoweza kummilikisha binadamu ulimwengu wa kimaada na kuleta mabadiliko makubwa katika nyanja zote za maisha, inaweza pia kumpatia raha. Hapa ndipo panapobainika nafasi ya

  45

  kimsingi ya kutafakari na athari zake za kushangaza katika maisha ya binadamu.

  Akili ing'aayo ni chemchemi neemevu inayomwendeleza mtu mbele zaidi kuliko mahitaji ya kidunia na inamjulisha ulimwengu mwingine pia. Fikra nzito na aali humzuia mwerevu asidanganyike na ulimwengu. Yule aliyekikuza na kukiimarisha kipaji chake cha fikra (akili) na akakifanya kuwa ni kitovu cha uvutano katika maisha yake, atakapofikwa na matukio machungu na mabaya, atachukua hatua inayofaa ya kifikra badala ya kuyakabili vibaya, na atabaki imara kamajabali.

  Ili tujitoe katika mazingira ya fazaa najahazi la uhai wetu lisikumbwe na mawimbi makubwa na madogo, ni lazima tuzidhibiti fikra zetu mpaka tafakuri sahihi zishike uongozi wetu, na nguvu zetu zote za kiroho ziweze kujizatiti na kusimama dhidi ya vitu vinavyoleta madhara na vinavyosababisha wasiwasi.

  Mwanachuoni mmoja wa Magharibi amesema:

  "Huenda hatuna uwezo wa kuwachagua kati ya marafiki na wasio marafiki watu ambao wanaweza kufanana nasi kwa upande wa tabia, maadili au mambo mengineyo, lakini tuko huru katika kuchagua fikra, kwa sababu katika nchi ya akili sisi ndio watawala na watendaji wenye amri kamili. Hapo hapana taathiri, vishawishi au vitu vinginevyo kutoka nje ambavyo vingeweza kutuhukumu au kutulazimisha kuchagua fikra tusizozitaka. Kwa hivyo, ni lazima kwetu tuchague njia sahihi ya kufikiri na tuziweke kando fikra yoyote isiyofaa. Siku zote tunafuata njia ambayo fikra zetu

  46

  zinatuelekeza; na kwa maana nyingine fikra zetu ndizo zinazotuongoza popote tunapopataka. Hivyo, inatulazimu tusiruhusu kufikiria fikra yoyote iliyo mbaya, wala tusiiruhusu akili yetu ishughulishwe na mambo tunayoyachukia, kwa sababu fikra kama hizo ndizo zinazotutia katika balaa. Ni lazima daima tufikirie kujipatia ukamilifu, si upungufu! Ni lazima tufikirie kupata matumaini bora kabisa na kufikia malengo ya juu kabisa, kwa sababu siri ya kila ufanisi na mafanikio iko katika kufikiri kwa njia sahihi tu."